Serikali yafunga kesi ya Mramba na Yona

Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
59,167
79,331
Wajameni mie nashindwa kuelewa maana ya kufunga! ina maana watuhumiwa hawana kesi ya kujibu au? na kama ni hivyo zile billioni 11 zilienda wapi? Naomba kueleweshwa!
 
SOURCE:
MICHUZI

Mi nilijua hii ni danganya toto tu maana wahisani waliposikia kashfa za EPA waligoma kuchangia badget ya mwaka 2009/10 ndo maana ikawakamata yona na mramba ili kuwadanganya kuna uwajibikaji.

Pia ukifuatilia huyo jaji aliyekua amekabidhiwa hiyo kesi bwana Utamwa mi namjua vizuri alikua mkoani kwenye mahakama za rufaa ila kwa muda wa mwaka mmoja amepandishwa vyeo mara tatu...kapandishwa kua msajili wa mahakama kuu kabla hata mwaka haujaisha kapandishwa kua jaji wa mahakama kuu na hapo ndipo alipokabidhiwa kesi ya yona na mramba.
KWELI HII NCHI INA WENYEWE!!
Mpaka mkwere amalize muda wake tutakula nyasi.
 
Wajameni mie nashindwa kuelewa maana ya kufunga! ina maana watuhumiwa hawana kesi ya kujibu au? na kama ni hivyo zile billioni 11 zilienda wapi? Huu usanii ni Mungu anajua

ina maana upande wa serikali umemaliza kuwasilisha ushahidi wke dhidi ya watuhumiwa, kinachofuatia nikwa mahakama kupitia ushahidi huo na kuona kama watuhumiwa wana kesi ya kujibu, ikiwa ipo basi mahakama inatoa nafasi kwa watuhumiwa kujitetea na kisha hukumu kutolewa, so mambo bado magumu kwa akina Mramba.... punguza jazba comrade!
 
Hapo sasa ndio wananchi tujue ya kwamba akina Rostam Aziz, Basil Mramba, Daniel Yona wote ni mashujaa kule CCM.

Ukizungumzia ufisadi huo unaujua wewe tu, siku nyingi walishaa takashwa midhambi yote na wote ni weupe kama sufu.
 
Kwa hiyo mawaziri hawa wataidai fidia serikali.

Hapo mkuu ndo nashindwa kupata picha.
Hivi mkwere ameamua kutukomoa coz anajua ashaingia madarakani hawezikutolewa kirahisi au?
ILA WA KULAUMIWA ZAIDI HAPA NI TUME YA UCHAGUZI AMBAYO MPAKA SASA HAIJUI KURA ZA URAIS ZILIKUA NGAPI!!!!
 
ina maana upande wa serikali umemaliza kuwasilisha ushahidi wke dhidi ya watuhumiwa, kinachofuatia nikwa mahakama kupitia ushahidi huo na kuona kama watuhumiwa wana kesi ya kujibu, ikiwa ipo basi mahakama inatoa nafasi kwa watuhumiwa kujitetea na kisha hukumu kutolewa, so mambo bado magumu kwa akina Mramba.... punguza jazba comrade!
asante mkuu huruma ilikuwa ishaniporonyoka nilikuwa najua Dowans style mambo ya serikali kususia kesi duh hiki kiswahili nacho! BTW naona Daily News limekuwa linalisifia jimbo la Rombo hata kurudia habari sijui kunani huko? au ndo mambo ya kusafishana taratibu....
 
DUh nilijua ile ilikuwa danganya toto tuuu, maana ingekuwa kweli wale jamaa wangefunguka sana tu kwenye vyombo vya habari na che Nkapa na yeye moja kwa moja alikuwa anahusikaaaaaa.
 
we mkuu unalosema ni la kweli ama uzushi?
kama ni kweli,basi walipanga iwe hivyo ndio maana ccm waliwasimamisha kugombea ubunge wakitambuwa kuwa watatoka tuu
jamani hii nchi mbona ipo hivi?
haya jamani maamuzi sahihi tunayo wananchi wakati ndio huuuuuuu

mapinduziiii daimaaaaaaaaa:plane:
 
Jk kwenye kampeni wakati anamnadi Mramba kule Rombo aliwambia Mramba ni Panga lenye incha kotekote.
Ulitegemea nini hapa?
JK na wenzie wanafanya kazi yao na bado!
 
Zombe anaidai serikali fidia ya bilioni tano, dowans, bado iptl tunailipa kila builioni 5, hawa wakina yona nao watataka tuwalipe mabilioni, liyumba naye akitoka.....
Jamani hii nchi inakwenda wapi?
 
Zombe anaidai serikali fidia ya bilioni tano, dowans, bado iptl tunailipa kila builioni 5, hawa wakina yona nao watataka tuwalipe mabilioni, liyumba naye akitoka.....
Jamani hii nchi inakwenda wapi?
Serikali imekua ikiendeshwa kikomedian sana mkuu.
Ndo maana mkuu wa TAKUKURU alisema kigezo cha kushughulikia rushwa ni kikwete.
 
SOURCE:
MICHUZI

Mi nilijua hii ni danganya toto tu maana wahisani waliposikia kashfa za EPA waligoma kuchangia badget ya mwaka 2009/10 ndo maana ikawakamata yona na mramba ili kuwadanganya kuna uwajibikaji.

Pia ukifuatilia huyo jaji aliyekua amekabidhiwa hiyo kesi bwana Utamwa mi namjua vizuri alikua mkoani kwenye mahakama za rufaa ila kwa muda wa mwaka mmoja amepandishwa vyeo mara tatu...kapandishwa kua msajili wa mahakama kuu kabla hata mwaka haujaisha kapandishwa kua jaji wa mahakama kuu na hapo ndipo alipokabidhiwa kesi ya yona na mramba.
KWELI HII NCHI INA WENYEWE!!
Mpaka mkwere amalize muda wake tutakula nyasi.

Mkuu punguza jazba, kufunga kesi na kuachiwa huru ni vitu viwili tofauti, kufunga kesi maana yake ni kuwa upande wa mashtaka umekamilisha ushaidi wake sasa kinachosubiliwa ni mahakama kuja na kauli kama watuhumiwa wana kesi ya kujibu au hawana kesi ya kujibu. huyo michuzi uliyemkoti kichwani bure kabisa inaonekana hata yeye hiyo habari kaipata kwa text msg. kama yeye ni mwandishi makini angalau angeandika kesi ya Mramba ushaidi wakamilika, hao ndio waandishi wetu hata akiwa chooni anataka yeye ndio aonekane ndio mtoa habari wa kwanza. pumba.
 
Hivi kuna chuo cha ufisadi ama! Kama kipo nijuzeni jamani! Ahhhhhhhhhh nimechoka kwelikweli.
From top to the bottom all CCM leaders are fisadi.
Mwisho wa mwanzo unawadia sasa.
 
Mkuu punguza jazba, kufunga kesi na kuachiwa huru ni vitu viwili tofauti, kufunga kesi maana yake ni kuwa upande wa mashtaka umekamilisha ushaidi wake sasa kinachosubiliwa ni mahakama kuja na kauli kama watuhumiwa wana kesi ya kujibu au hawana kesi ya kujibu. huyo michuzi uliyemkoti kichwani bure kabisa inaonekana hata yeye hiyo habari kaipata kwa text msg. kama yeye ni mwandishi makini angalau angeandika kesi ya Mramba ushaidi wakamilika, hao ndio waandishi wetu hata akiwa chooni anataka yeye ndio aonekane ndio mtoa habari wa kwanza. pumba.
Kama ndo hivi nashukuru mkuu ila tusubirie tuone hukumu maana bado siamini kama hukumu itakua ya halali au yenye ukweli ndani yake.
 
we mkuu unalosema ni la kweli ama uzushi?
kama ni kweli,basi walipanga iwe hivyo ndio maana ccm waliwasimamisha kugombea ubunge wakitambuwa kuwa watatoka tuu
jamani hii nchi mbona ipo hivi?
haya jamani maamuzi sahihi tunayo wananchi wakati ndio huuuuuuu

mapinduziiii daimaaaaaaaaa:plane:
Ndio nchi ilivo, maamuzi tulikuwa nayo nov. hatukuamini tulipoambiwa.... hawa na wenyewe kama Zombe, watashinda na kudai kiinua mgongo chao.... Chama cha kijani juu!!!!!!:welcome:
 
Back
Top Bottom