Serikali ‘yaangukia’ hospitali binafsi kutoa kuduma ya afya bure

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Saturday, 22 October 2011 09:31

Patricia Kimelemeta

SERIKALI imezitaka hospitali na taasisi binafsi zinazotoa huduma ya afya nchini kutoa bure kwa wazee, walemavu, watoto chini ya miaka mitano na wananchi wasiokuwa na uwezo wa kulipia huduma hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuwapo kwa malalamiko kwa hospitali hizo kudaiwa kutoza kiwango kikubwa cha fedha jambo ambalo limesababisha wananchi wengi kushindwa kumudu na kukimbilia kwenye hospitali za Serikali.

Akizungumza kwenye Mkutano wa Chama cha Watoa Huduma ya Afya Binafsi (APHFTA) Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Lucy Nkya, alisema kutokana na hali hiyo, hospitali na taasisi hizo zinapaswa kupunguza gharama ili kila mmoja aweze kupata matibabu hata kama maeneo hayo hakuna hospitali au vituo vya afya vya Serikali.

Dk Nkya alisema ili kufikia malengo ya milenia mwaka 2015, Serikali imepanga kuboresha sekta ya afya ikiwamo kutoa huduma bure kwa makundi maalum ambayo ni walemavu, wazee, wasiojiweza na watoto chini ya umri wa miaka mitano.

“Gharama zinazotozwa na hospitali, taasisi na vituo binafsi vya afya ni kubwa, wananchi wengi wanashindwa kumudu jambo ambalo limesababisha kwenda umbali mrefu kutafuta hospitali za Serikali, kutokana na hali hiyo Serikali imewataka kupunguza gharama hizo,” alisema Dk Nkya.

Aliongeza kuwa hadi sasa idadi ya hospitali na taasisi hizo ni kubwa, hivyo basi kwa pamoja wanaweza kutoa huduma hiyo na kupunguza mrundikano wa wagonjwa katika hospitali za Serikali.

Waziri alisema ili kuyafikia malengo ya milenia, ni wajibu wa sekta binafsi kushirikiana na Serikali kwa suala zima la utoaji huduma bora za afya, iwe mijini au vijijini, jambo ambalo linaweza kuleta maendeleo na wananchi kuwa na imani na Serikali yao.

 
Ubovu wa Mipango ya Serikali ya CCM; Haikuangalia Mbali
 
Haya ni maonezi makubwa sana... Kama tumeshindwa Ubepari basi watangaze tu kwamba tumerudi ktk Ujamaa maana CCM inajulikana na ni Liberal - for Ujamaa na Kujitegemea na Against watu wachache kumiliki Utajiri wa nchi yetu. Sasa kwa nini msirudi ktk basic iliyowapa jina hilo?..Huduma za Afya fedha yote inatokana na makundi haya ya watu maanake vijana na wa makamo wengi sii wagonjwa wa mara kwa mara..Wataweza vipi kuendesha biashara zao ikiwa serikali itawawekea masharti hali wao wenye uwezo wanaenda kutibiwa India!

Kama kuna huduma za bure zinatakiwa zitolewe basi ni hizo shule na Hospital za NGos, Bakwata ni makanisa kwa sababu wamesamehewa hawalipi kodi na wanatakiwa ku run huduma hizi bila faida, Hizi ada kubwa za shule wanazotoza wanafunzi tena kubwa kuliko shule za watu binafsi ni kwa matumizi gani?
 
Back
Top Bottom