Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar yazikwa

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,975
Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) iko njia panda kutokana na matokeo yaliyotangazwa jana na ZEC kuonesha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) peke yake ndicho chenye haki ya kuunda Serikali.

Ni CCM pekee ambayo mgombea wake wa urais amepata zaidi ya asilimia 10 ya kura na ndiyo imezoa wawakilishi karibu wote na hivyo kubaki chama pekee chenye sifa ya kuingia kwenye serikali ya umoja wa kitaifa.

Mshindi wa pili wa matokeo ya kura za urais ni Hamad Rashid Mohamed aliyeambulia kura 9,734 sawa na asilimia3.

Akizungumzia hatma ya SUK, alisema serikali hiyo itaendelea kuwepo kwani Rais aliyepo madarakani lazima ateue watu kutoka kwenye vyama vya upinzani kuunda serikali hiyo. Alisema kwamba yeye ana matumaini makubwa kuwa Dk Shein atamteua yeye awe makamu wa kwanza wa rais kwa sababu katiba inaelekeza kuwa mshindi anayefuatia kwa kura za urais ndiye mwenye sifa.

Mwanasheria wa ZEC, Issa Khamis alisema kwamba Katiba ya Zanzibar iliyofanyiwa marekebisho inafafanua kuwa mgombea aliyepata kura sio chini ya asilimia 10 ndiye ataingia kwenye serikali hiyo na akaongeza kuwa Katiba hiyo iko kimya kama sifa hiyo haitakuwepo. Alifafanua kuwa kutokana na hali hiyo kuundwa kwa Serikali hiyo kutategemea na maamuzi na utashi wa Rais aliyeshinda kwenye uchaguzi huo.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alikiri kuwa kwa kuwa hakuna chama ambacho kimefikisha asilimia 10 ya kura za urais isipokuwa CCM kama inavyotamkwa na Katiba ya Zanzibar.

Vuai alisema serikali ya kitaifa inaundwa kikatiba na kama hakuna chama ambacho kina sifa za kuingia kwenye serikali hiyo ni wazi kuwa hapo uundwaji wake unategemea busara na maamuzi ya Rais aliyepo madarakani.

“Katiba ya Zanzibar inasema chama chenye sifa ya kuingia kwenye serikali ya umoja wa kitaifa kimewekewa kifungu maalum kuwa ni lazima kipate kura za urais walau asilimia 10 kwa matokeo ya leo hakuna chama kilichopata asilimia hiyo isipokuwa Chama Cha Mapinduzi. “Kwa hiyo kwa haraka haraka unapata majibu hiyo maana yake nini na huko mbele katiba hiyo inasema kama hujapata hiyo asilimia 10 basi upate viti vingi kwenye baraza la wawakilishi, lakini katika uchaguzi huu viti vyote vimechukuliwa an CCM.

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Mtungi alipoulizwa kuhusu maoni yake kama kwa matokeo hayo nini hatima ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa alisema hawezi kuzungumzia jambo hilo. Aliyekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria wa Zanzibar, Awadhi Said, alisema suala la uwepo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni la kikatiba na kwamba muundo na uwepo wake umeidhinishwa kikatiba.

Akizungumza jana kwa simu, alisema katiba inatamka wazi matakwa ya atakayekuwa Makamo wa Kwanza wa Rais lazima apate asilimia 10 ya kura za urais na huo ndiyo msingi wa awali na sio kusubiri busara ya Rais.

Muundo wa SUK
Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) imetamkwa katika Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 Toleo la 2010 Kifungu cha 9(3). Kifungu hicho kinasema “ Muundo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar utakuwa wa Umoja wa Kitaifa na utendaji wa kazi zake, utafanywa katika utaratibu utakaohakikisha kuendelezwa kwa umoja nchini na lengo la kufikia demokrasia”.

Katiba hiyo ilianzisha cheo cha Makamu wa Kwanza wa Rais na Makamu wa Pili na kufuta wadhifa wa Waziri Kiongozi.

Kwa mujibu wa Marekebisho ya 10 ya Katiba, Makamo wa Kwanza wa Rais atateuliwa na Rais baada ya kushauriana na chama cha siasa kilichopata nafasi ya pili katika matokeo ya kura ya uchaguzi wa Rais.

Kifungu cha 39(3) cha Katiba hiyo kinasema kuwa Makamo wa Kwanza wa Rais atatakiwa awe na sifa za kumwezesha kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi ; na atateuliwa na Rais baada ya kushauriana na chama kilichopata nafasi ya pili katika matokeo ya kura ya uchaguzi wa Rais, kama chama hicho kilichopata nafasi ya pili katika matokeo ya kura ya uchaguzi wa Rais, kitapata asilimia kumi ya kura zote za uchaguzi wa rais.

Katiba hiyo inasema Makamu wa Pili wa Rais atateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka katika chama cha siasa anachotoka Rais.
Kwa hisani ya habarileo
 
Dhambi ya kuandika Katiba huku wakiwa na chuki kwa Watanganyika inazidi kuwatafuna Wazanzibari.

Waliandika Katiba haraka haraka mpaka wakasahau kuweka mazingira ya uwepo wa hali iliyojitokeza katika Uchaguzi uliomalizika jana!

Walidhani adui wao ni Tanganyika. Walidhani anayewafanya wabaguane na kutengana ni Tanganyika!

Wakadhani wakisema kwenye Katiba kuwa Zanzibar ni nchi watakuwa wamemaliza matatizo yao.

Walisahau kuisoma historia yao na kutafuta majibu kwa kutumia historia yao badala yake wakajikita kutafuta majibu ya matokeo ya historia yao. Kama sio historia yao, mwaka 1964 Tanzania isingepeleka wanajeshi zaidi ya 300 kuyalinda mapinduzi, na kwa maana hiyo, hata muungano usingekuwepo.

Kwa sasa wamerudi kule kule ambako hawakutaka kutafuta majibu. Katiba yao kwa sasa inaonekana ni kaput.

Hii dhambi ya ubaguzi na utengano itaendelea kuwatafuna!
 
Alisema kwamba
yeye ana matumaini
makubwa kuwa Dk Shein
atamteua yeye awe
makamu wa kwanza wa
rais kwa sababu katiba
inaelekeza kuwa mshindi
anayefuatia kwa kura za
urais ndiye mwenye sifa...Hamad Rashid kadata?
 
Ukweli ni kwamba zanzibar ni koloni la tanganyika na ipo siku zanzibar itakuwa huru,ni jambo la muda tu.
 
Wewe msemajiuongo so msemaji kweli kama huna cha kuandika tulia, umetolewa ufafanuzi wa kisheria na were Njoo kisheria sio kumwaga povu
 
Nimefurahi kusikia kuwa serikali ya Zanzibar itakuwa ya umoja wa kitaifa
Hivyo basi serikali yoyote ambayo haitakuwa na makamu wa kwanza wa rais ni kinyume cha katiba.
ni pishane na hao wachambuzi wanao tumia neno utashi wa rais..... wapi katika katiba panampa shein maanuzi ya kufanya anavyoona inafaa. in fact najua katiba ya Zanzibar inatamka ukuu wa katiba si ukuu wa rais hivyo no means uchaguzi urudiweee!!!
poleni Sana CCM
 
hawa wazenji hawajitambui... wataendelea kuwa koloni la wadanganyika hadi kizazi hiki kipite..
 
Dhambi ya kuandika Katiba huku wakiwa na chuki kwa Watanganyika inazidi kuwatafuna Wazanzibari.

Waliandika Katiba haraka haraka mpaka wakasahau kuweka mazingira ya uwepo wa hali iliyojitokeza katika Uchaguzi uliomalizika jana!

Walidhani adui wao ni Tanganyika. Walidhani anayewafanya wabaguane na kutengana ni Tanganyika!

Wakadhani wakisema kwenye Katiba kuwa Zanzibar ni nchi watakuwa wamemaliza matatizo yao.

Walisahau kuisoma historia yao na kutafuta majibu kwa kutumia historia yao badala yake wakajikita kutafuta majibu ya matokeo ya historia yao. Kama sio historia yao, mwaka 1964 Tanzania isingepeleka wanajeshi zaidi ya 300 kuyalinda mapinduzi, na kwa maana hiyo, hata muungano usingekuwepo.

Kwa sasa wamerudi kule kule ambako hawakutaka kutafuta majibu. Katiba yao kwa sasa inaonekana ni kaput.

Hii dhambi ya ubaguzi na utengano itaendelea kuwatafuna!
utumbo mtupu hayo matokeo yamepangwa na usalama wataifa na wanoichafua zanzibar ndio hawo hawo watanganyika wa ccm na toka lini ccm wakaheshimu katiba
 
Alisema kwamba
yeye ana matumaini
makubwa kuwa Dk Shein
atamteua yeye awe
makamu wa kwanza wa
rais kwa sababu katiba
inaelekeza kuwa mshindi
anayefuatia kwa kura za
urais ndiye mwenye sifa...Hamad Rashid kadata?
Alihaidiwa akaingia kichwakichwa,Huyu ndo alitumika na CCM kushawishi vile vijivyama kutogomea uchaguzi kwa ahadi ya kugawiwa umakamo,sasa wamechukua kura zote ili kumnyima uhalali wa kuteuliwa waongoze wenyewe.
 
Eti mnasemaje!?

Kwamba hata viti vyote vya BLW imechukua CCM? Na madiwani wote?

Mbona ni kitu ambacho ni impossible hata kwa akili ya kawaida tu!!

Haiwezekani mtu aliyekuwa ameshinda kiti cha Urais (Maalim Seif Shariff Hamad na CUF) na viti vya BLW zaidi ya nusu leo eti akose vyote!!

Utaongozaje nchi ktk mazingira ya kuonesha kuwa umeiba haki ya kuchagua ya watu waziwazi? Utawaongoza kina nani hao?
 
utumbo mtupu hayo matokeo yamepangwa na usalama wataifa na wanoichafua zanzibar ndio hawo hawo watanganyika wa ccm na toka lini ccm wakaheshimu katiba
Wakati kina maalim wameshupaa koo, wakasema zanzibar ni nchi yenye kamili walipangiwa na ccm?
Kinara wa kudai na kutamba kuhusu utaifa wa zanzibar ni nani?

Alikuja kugundua kachemsha baada ya Jecha kupiga tukio akakimbilia kwa kikwete. Kufika huko akakuta hakuendeki...Kikwete akamwambia hayanihusu akampa mkuu wa majeshi aseme naye.

Alivoapishwa JPM, ilibidi Maalimu ameze mate na kufutilia mbali zile kauli za ukawa kuwa hawautambui ushindi wa JPM. Akafunga safari kwa unyenyekevu. JPM naye akamwambia hainihusu, hii ni juu yenu na mamlaka yenu Zanzibar. Siingilii.

Hadi sasa Maalim anapiga Selfie pale Serena. Yuko kimyaaaaaaa.
 
Nimefurahi kusikia kuwa serikali ya Zanzibar itakuwa ya umoja wa kitaifa
Hivyo basi serikali yoyote ambayo haitakuwa na makamu wa kwanza wa rais ni kinyume cha katiba.
ni pishane na hao wachambuzi wanao tumia neno utashi wa rais..... wapi katika katiba panampa shein maanuzi ya kufanya anavyoona inafaa. in fact najua katiba ya Zanzibar inatamka ukuu wa katiba si ukuu wa rais hivyo no means uchaguzi urudiweee!!!
poleni Sana CCM
Nikupe pore kama unafikiri hicho kitu kinawaumiza vichwa ccm..

Kama waliweza kufuta uchaguzi bila aibu basi hata hilo kuna kitu watafanya na wataendelea kutawala huku wamelilaksi... Hutaamin macho yako
 
Nikupe pore kama unafikiri hicho kitu kinawaumiza vichwa ccm..

Kama waliweza kufuta uchaguzi bila aibu basi hata hilo kuna kitu watafanya na wataendelea kutawala huku wamelilaksi... Hutaamin macho yako
 
Dhambi ya kuandika Katiba huku wakiwa na chuki kwa Watanganyika inazidi kuwatafuna Wazanzibari.

Waliandika Katiba haraka haraka mpaka wakasahau kuweka mazingira ya uwepo wa hali iliyojitokeza katika Uchaguzi uliomalizika jana!

Walidhani adui wao ni Tanganyika. Walidhani anayewafanya wabaguane na kutengana ni Tanganyika!

Wakadhani wakisema kwenye Katiba kuwa Zanzibar ni nchi watakuwa wamemaliza matatizo yao.

Walisahau kuisoma historia yao na kutafuta majibu kwa kutumia historia yao badala yake wakajikita kutafuta majibu ya matokeo ya historia yao. Kama sio historia yao, mwaka 1964 Tanzania isingepeleka wanajeshi zaidi ya 300 kuyalinda mapinduzi, na kwa maana hiyo, hata muungano usingekuwepo.

Kwa sasa wamerudi kule kule ambako hawakutaka kutafuta majibu. Katiba yao kwa sasa inaonekana ni kaput.

Hii dhambi ya ubaguzi na utengano itaendelea kuwatafuna!

Hapana Kiongozi,pamoja na mapungufu mengi ya kisheria yaliyomo katika katiba ya Zanzibar,suala la serikali ya umoja wa kitaifa lipo "very clear "kwenye katiba yao.Tukiachana na yaliyotokea na kufuta tongotongo kwenye macho yetu,hakuna chama kinachoweza kupata ushindi wa >90% kwenye chaguzi za Zanzibar isipokuwa pale ambapo " wahafidhina" wa Bara wametia mikono yao.

Ipo dhahiri na wala haihitaji msaada wa kurunzi kuuona ukweli wa ubakwaji wa demokrasia uliofanyika Zanzibar.Uchaguzi uliopita wa 25,Oktb,CUF ilidhinda viti vyote vya Pemba na ikafanikiwa kujipenyeza na kushinda viti 9 Unguja.
Kama si kufutwa kwa uchaguzi huo kusingekuwa na kigugumizi cha kikatiba cha kuunda SUK.

Alichokosea jecha ni kuwapa CCM 91.4%,pamoja na kutimiza lengo lao la kuvitawala viwiliwili vya Wazanzibar,nasema viwiliwili kwa Maana Wazanzibar kwa kauli moja waliamua kuipumzisha CCM Oktoba 25 kwa kuichagua CUF,jecha alipaswa kuzigawa kura kwa uwiano utakaowezesha kuundwa kwa SUK.Lakini kwa sababu alipigwa upofu,sasa wanaanza kujiuliza namna watakavyotimiza takwa la kikatiba la kuunda SUK.

Jambo la kukumbukwa na Wazanzibar wote ambalo pia litakuwa ni Mitihani mgumu sana kwa "Dk.Sheitwan" ni namna atakavyoongoza Umma wa Wazanzibar waliomkataa.Pamoja na matokeo kumpa ushindi lakini matokeo hayo hayauondowi Ukweli mchungu unaotambulika hata katika korido za CCM pale Kisiwandui hadi Lumumba kuwa CCM ilikataliwa na wananchi wa Zanzibar lakini kwa kiburi cha kidora,ikagoma kukabidhi nchi kwa walioshinda.

Sasa leo CCM imekabidhiwa Ikulu na jecha,nje ya Ikulu yupo Mh.Maalim Seif Sharif Hamad akiwa na serikali kivuli inayoungwa mkono na mioyo ya Wazanzibar tena bila kujali tofauti zao za kisiasa,je "Sheitwan" atawaweza kuwaunganisha Wazanzibar bila ya kutumia Seif? Kukitokea mkwamo wa kisiasa huko Zanzibar katika wakati ambao mmoja wa watu wenye ushawishi na ufuasi mkubwa haitambui serikali wala uchaguzi uliyoiweka serikali madarakani,watamtumia nani kutuliza hasira za Wazanzibar?

Hapo ndipo CCM ilipowafikisha wazanzibar,ni Mungu tu aonaye sirini ndiyo anayejuwa kishindo kitakacholetwa na uporaji huu wa Demokrasia uliofanywa na CCM kwa kupitia "Bedui" aitwaye JEHCHER.

Ili CCM iweze kuvitawala viwiliwili vya Wazanzibar waliowakataa mioyoni haina chaguo lingine zaidi ya kuunda SUK inayohusisha vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wale mazombie,vifaru mizinga na siraha zote za kijeshi.Ni kwa kupitia mkono wa chuma tu ndipo "Sheitwan" ataweza kuikalia kimabavu Zanzibar,bila hivyo Zanzibar haitatawalika.KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI,CCM HOYEEE,JECHA HOYEEEE!!!!,ASANTENI SANA.
 
Nikupe pore kama unafikiri hicho kitu kinawaumiza vichwa ccm..

Kama waliweza kufuta uchaguzi bila aibu basi hata hilo kuna kitu watafanya na wataendelea kutawala huku wamelilaksi... Hutaamin macho yako
wewe Crimea acha ujinga tumia kiswahili fasaha kwenye maandiko yako,

Pore = POLE
wamelilaksi = wamerilaksi(relax) shwain
 
Naona kuna kila dalili ya katiba ya Zanzibar kusiginwa na kulazimisha upatikanaji wa makamu wa kwanza wa raisi kutoka upinzani(ADC).
 
Hapana Kiongozi,pamoja na mapungufu mengi ya kisheria yaliyomo katika katiba ya Zanzibar,suala la serikali ya umoja wa kitaifa lipo "very clear "kwenye katiba yao.Tukiachana na yaliyotokea na kufuta tongotongo kwenye macho yetu,hakuna chama kinachoweza kupata ushindi wa >90% kwenye chaguzi za Zanzibar isipokuwa pale ambapo " wahafidhina" wa Bara wametia mikono yao.

Ipo dhahiri na wala haihitaji msaada wa kurunzi kuuona ukweli wa ubakwaji wa demokrasia uliofanyika Zanzibar.Uchaguzi uliopita wa 25,Oktb,CUF ilidhinda viti vyote vya Pemba na ikafanikiwa kujipenyeza na kushinda viti 9 Unguja.
Kama si kufutwa kwa uchaguzi huo kusingekuwa na kigugumizi cha kikatiba cha kuunda SUK.

Alichokosea jecha ni kuwapa CCM 91.4%,pamoja na kutimiza lengo lao la kuvitawala viwiliwili vya Wazanzibar,nasema viwiliwili kwa Maana Wazanzibar kwa kauli moja waliamua kuipumzisha CCM Oktoba 25 kwa kuichagua CUF,jecha alipaswa kuzigawa kura kwa uwiano utakaowezesha kuundwa kwa SUK.Lakini kwa sababu alipigwa upofu,sasa wanaanza kujiuliza namna watakavyotimiza takwa la kikatiba la kuunda SUK.

Jambo la kukumbukwa na Wazanzibar wote ambalo pia litakuwa ni Mitihani mgumu sana kwa "Dk.Sheitwan" ni namna atakavyoongoza Umma wa Wazanzibar waliomkataa.Pamoja na matokeo kumpa ushindi lakini matokeo hayo hayauondowi Ukweli mchungu unaotambulika hata katika korido za CCM pale Kisiwandui hadi Lumumba kuwa CCM ilikataliwa na wananchi wa Zanzibar lakini kwa kiburi cha kidora,ikagoma kukabidhi nchi kwa walioshinda.

Sasa leo CCM imekabidhiwa Ikulu na jecha,nje ya Ikulu yupo Mh.Maalim Seif Sharif Hamad akiwa na serikali kivuli inayoungwa mkono na mioyo ya Wazanzibar tena bila kujali tofauti zao za kisiasa,je "Sheitwan" atawaweza kuwaunganisha Wazanzibar bila ya kutumia Seif? Kukitokea mkwamo wa kisiasa huko Zanzibar katika wakati ambao mmoja wa watu wenye ushawishi na ufuasi mkubwa haitambui serikali wala uchaguzi uliyoiweka serikali madarakani,watamtumia nani kutuliza hasira za Wazanzibar?

Hapo ndipo CCM ilipowafikisha wazanzibar,ni Mungu tu aonaye sirini ndiyo anayejuwa kishindo kitakacholetwa na uporaji huu wa Demokrasia uliofanywa na CCM kwa kupitia "Bedui" aitwaye JEHCHER.

Ili CCM iweze kuvitawala viwiliwili vya Wazanzibar waliowakataa mioyoni haina chaguo lingine zaidi ya kuunda SUK inayohusisha vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wale mazombie,vifaru mizinga na siraha zote za kijeshi.Ni kwa kupitia mkono wa chuma tu ndipo "Sheitwan" ataweza kuikalia kimabavu Zanzibar,bila hivyo Zanzibar haitatawalika.KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI,CCM HOYEEE,JECHA HOYEEEE!!!!,ASANTENI SANA.
Mkuu umemaliza kila kitu.ambaye yupo tayari kuelewa ameelewa.
 
Naona kuna kila dalili ya katiba ya Zanzibar kusiginwa na kulazimisha upatikanaji wa makamu wa kwanza wa raisi kutoka upinzani(ADC).
Nani kakudanganya ADC ni chama cha upinzani?kile ni tawi la ccm na hamad rashid ni mamluki anayetumiwa na ccm kuuvuruga upinzani.
 
Ukweli ni kwamba zanzibar ni koloni la tanganyika na ipo siku zanzibar itakuwa huru,ni jambo la muda tu.
Kuendelea kutafuta wachawi wakati wachawi mnao wenyewe ni kupoteza muda.

Mchawi wenu ni fikra za kibaguzi.

Mpaka pale mtaacha kubaguana, mtaendelea kuwa katika hali kama iliyojitokeza katika uchaguzi.
 
Back
Top Bottom