Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,502
- 9,281
WAZIRI wa Afya nchini Kenya, Wafula Nakhumicha amesema Serikali ya Kenya imeomba msaada dawa za Kifua Kikuu kutoka nchini Tanzania ili kukabiliana na uhaba wa dawa za Kifua Kikuu nchini humo.
Waziri Nakhumicha amesema ombi hilo limekuja baada ya nchi hiyo kukumbwa na uhaba wa dawa hizo kuanzia Oktoba 2023.
"Mwishoni mwa mwezi Septemba na Oktoba mwaka jana tulikuwa na uhaba wa dawa za Kifua Kikuu, lakini tulijitahidi kwa kiasi ambacho tulipata msaada kutoka nchi jirani ya Tanzania na tulipata akiba ya kutosha ambayo sasa imesambazwa," amesema Waziri Wafua.