tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,246
- 4,467
Kenya kuna makampuni mengi makubwa ya madawa, ambayo mengi yao ni innovators wa dawa mbalimbali (brands), ambazo nchi nyingine hususani India huja kuzalisha baadaye kama generic.
Kwa wasiojua brands huuzwa ghali, ila ni bora zaidi, wakati ni generic huuzwa kwa bei ya kutupwa, nyingi zikiwa na ubora unaopungua zaidi ya 80% ya brand yake.
Kampuni kubwa kama Novartis, Merck, Johnson & Johnson, Roche, Sanofi, Bristol Myers, Lilly, AstraZeneca, Gilead, Novo Nordisk, Bayer, GSK, Takeda n.k zote zipo kwenye soko la Kenya. Madaktari wa Kenya, wanaandika dawa kwa kutumia brands, tanzania wanatumia zaidi Generic.
Mwisho wa siku mtanzania atapata dawa za kiwango cha chini, hususani toka India na mara nyingi zitafanya kazi kwa kiwango duni na zimejaa maudhi lukuki. Najua kuna watu watapinga, ila ni sawa na kutumia Iphone au Samsung Galaxy vs Tecno Phantom.
Kuna mfamasia mwenzangu hapa Nairobi, aliniuliza kulikoni Tanzania mnauziwa dawa za kiwango duni za Kihindi? Mbona kampuni kubwa za madawa zinawakimbia? Nikamwambia sisi Tanzania kitu cha kwanza tunaangalia price, issue za quality sisi hatuzijui. Akaniuliza wewe uko radhi kutibiwa na Ceftriaxone ya kihindi inayouzwa Ksh 100, au kutibiwa na Rocephin, ambayo ni Ceftriaxone original iliyovumbuliwa na Roche, inayouzwa kwa KSh 1,500?
Nilimjibu ningetumia Rocephin. Akaniuliza mbona watanzania mnatumia zaidi dawa za kihindi kwa wagonjwa wenu? Sikuwa na jibu, maana mimi siandiki prescriptiom. Mimi natoa dawa iliyoandikwa na daktari.
Madaktari wa Tanzania, mjitafakari. Hayo mambo ya cheap cheap, kuna wakati wagonjwa wenu hawaponi.