Serikali: Tunaandaa Muongozo wa Kulipa "Extra Duty" Kwa Walimu

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
44,613
51,456
Serikali mbioni kuanza kuwalipa Walimu posho ya masaa ya ziada yaani Extra duty kama Watumishi wengine..

Kwa hili Samia anazidi kuchukua pointing tatu muhimu na hii ni kuanzia mwaka wa Fedha ujao.

======
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Deogratias Ndejembi amesema Serikali haina posho ya mazingira magumu kwa walimu lakini iko katika maandalizi ya mwongozo wa ulipaji posho ya masaa ya ziada.

Pia amewaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa ya Tanzania Bara kufanya msawazo wa walimu kutoka shule zenye ziada na kuwapeleka katika shule zanye upungufu zaidi.

Ndejembi ameyasema hayo jana bungeni wakati wa kujibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Kunti Majala (CCM). Katika swali lake Majala alitaka kujua ni lini serikali itatoa posho ya mazingira magumu kwa walimu waliovijijini hususani walimuwa wanawake.

Akijibu swali hilo, Njejembi alisema Serikali inaweka uwezeshaji kwa walimu kwa kujenga nyumba karibu na shule na kuwa hakuna posho mahususi ya mazingira magumu inayotolewa.

“Kwa sasa tunaendelea na kazi ya kuandaa mwongozo wa ulipaji posho kwa masaa ya ziada.”

Katika swali la nyongeza, Majala alitaka kujua mpango wa serikali wa kupeleka walimu wa kike katika shule za sekondari na msingi wilayani Chemba.

Akijibu swali hilo, Ndejembi alisema Serikali imekuwa ikitoa ajira ili kukabiliana na upungufu wa walimu shuleni unaotokana na walimu kustaafu, kuacha kazi, kufukuzwa, kufariki na ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa.

Alisema kwa mwaka 2021/22, Serikali imeajiri jumla ya walimu 26,598 wakiwemo 16,640 wa shule za msingi na 9,958 wa shule za sekondari.

Ndejembi alisema kwa upande wa ajira zilizotangazwa 2021/22, Halmashauri ya Wilaya ya Chemba ilipata walimu 46 wakiume na walimu 49 wa kike kwa shule za msingi na sekondari.

“Ofisi ya Rais-TAMISEMI imetoa maelekezo kwa makatibu tawala wa mikoa wote Tanzania Bara kufanya msawazo wa walimu kutoka shule zenye ziada na kuwapeleka katika shule zanye upungufu zaidi kwa kuzingatia jinsia ili kuwa na uwiano wa walimu wa kike na kiume kwenye shule zetu mbalimbali.”
 
Sijasoma habari yote ila bado naona ombwe la kutotaka kuboresha kile tunachokitaka haswa, tunachofanya ni kupiga plasta na chokaa kwenye nyumba iliyojengwa kwa mbolea ya ng'ombe na miti!
Mnakitaka kipi hicho?

Serikali inajengea walimu nyumba,

Walimu ni Kati ya kada Zenye salary kubwa.

Na Sasa kutakuwa na posho sijui wewe unataka kuwa mtumishi au mfujaji.
 
Ni Jambo nzuri kuleta motisha kwa walimu, lakini Mimi Nina mtazamo tofauti , Hizo fedha ambazo zitatumika kulipa extraduty , kwa Nini serikali isiongeze idadi ya kuajiri watumishi WALIMU walioko mtaani miaka mingi ili kuwapunguzia ukalli na ugumu wa maisha!!!!
 
Serikali mbioni kuanza kuwalipa Walimu posho ya masaa ya ziada yaani Extra duty kama Watumishi wengine..

Kwa hili Samia anazidi kuchukua pointing tatu muhimu na hii ni kuanzia mwaka wa Fedha ujao.

======
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Deogratias Ndejembi amesema Serikali haina posho ya mazingira magumu kwa walimu lakini iko katika maandalizi ya mwongozo wa ulipaji posho ya masaa ya ziada.

Pia amewaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa ya Tanzania Bara kufanya msawazo wa walimu kutoka shule zenye ziada na kuwapeleka katika shule zanye upungufu zaidi.

Ndejembi ameyasema hayo jana bungeni wakati wa kujibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Kunti Majala (CCM). Katika swali lake Majala alitaka kujua ni lini serikali itatoa posho ya mazingira magumu kwa walimu waliovijijini hususani walimuwa wanawake.

Akijibu swali hilo, Njejembi alisema Serikali inaweka uwezeshaji kwa walimu kwa kujenga nyumba karibu na shule na kuwa hakuna posho mahususi ya mazingira magumu inayotolewa.

“Kwa sasa tunaendelea na kazi ya kuandaa mwongozo wa ulipaji posho kwa masaa ya ziada.”

Katika swali la nyongeza, Majala alitaka kujua mpango wa serikali wa kupeleka walimu wa kike katika shule za sekondari na msingi wilayani Chemba.

Akijibu swali hilo, Ndejembi alisema Serikali imekuwa ikitoa ajira ili kukabiliana na upungufu wa walimu shuleni unaotokana na walimu kustaafu, kuacha kazi, kufukuzwa, kufariki na ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa.

Alisema kwa mwaka 2021/22, Serikali imeajiri jumla ya walimu 26,598 wakiwemo 16,640 wa shule za msingi na 9,958 wa shule za sekondari.

Ndejembi alisema kwa upande wa ajira zilizotangazwa 2021/22, Halmashauri ya Wilaya ya Chemba ilipata walimu 46 wakiume na walimu 49 wa kike kwa shule za msingi na sekondari.

“Ofisi ya Rais-TAMISEMI imetoa maelekezo kwa makatibu tawala wa mikoa wote Tanzania Bara kufanya msawazo wa walimu kutoka shule zenye ziada na kuwapeleka katika shule zanye upungufu zaidi kwa kuzingatia jinsia ili kuwa na uwiano wa walimu wa kike na kiume kwenye shule zetu mbalimbali.”
Sisi wakulima inatusaidia nini hii
 
Kwani huoni watu wamekaa miaka 9 bila kupandshwa vyeo Ila chini ya uongozi wa mama wamepanda wote hakuna aliyeachwa
kwani unaongelea nchi mbili tofauti
sisi wakulima tunalaani maamuzi ya nchi nzima kuwa chini ya mtu mmoja, ni aibu
pia tunalaani wakuu wa vyama vya wafanyakazi kukaa kimya kipindi cha hiyo miaka 9, walaaniwe kabisa
 
Ni Jambo nzuri kuleta motisha kwa walimu, lakini Mimi Nina mtazamo tofauti , Hizo fedha ambazo zitatumika kulipa extraduty , kwa Nini serikali isiongeze idadi ya kuajiri watumishi WALIMU walioko mtaani miaka mingi ili kuwapunguzia ukalli na ugumu wa maisha!!!!
Kaaah....ila jamani
 
bajeti itusaidie wakulima, hata kutufanyia utafiti wa ardhi yetu tunayolima
Kwani haifanyi hivyo? Hujaskia maafisa ugani wamegawiwa kits Zenye vifaa vya kupima Ardhi,wamepewa pikipiki na kuanzia mwaka huu nyumba 4000 zitajengwa kwenye kata Ili wakae huko huko..
 
Kwani huoni watu wamekaa miaka 9 bila kupandshwa vyeo Ila chini ya uongozi wa mama wamepanda wote hakuna aliyeachwa
Kuna muda nasema Bora ht mwendazake alivoenda Kwa kweli daahhh...Kwa hili la madaraja nashindwa msameh Mimi mwenzenu
Tena Maza Sio TU kupanda ila kama ulikaa more than six years hujapanda unapandishwa mara ya kwanza na after two years wapanda Tena
Huyu mama Ana madhaifu but at least ana utu wake
Mungu amuweke Kwa ajili yetu
Mimi nilitakiwa niingie G last year ila yule mwenda zake sina hamu NAE,malimbikizo nimelipwa mwaka jana na Maza!!!
Toka enzi hizoo
Mimi mama Samia Kwa Sasa namuelewa mnooo ,then kingine kizuri madaraja ukipandishwa within two months unakua ushalipwa tayari

Maza Kwa Sasa namuelewa mnooo....Hakuna mkamilifu ila at least yeye ana utu
 
Back
Top Bottom