Amesikika mheshimiwa SSH jana akiongelea tozo za miamala na bei za mbolea. Akijinasibu kuwa huko ndiko kusikia kwa serikali yake sikivu.
Ikumbukwe kuwa za moto zaidi kwenye ajenda zimekuwa:
1. Ongezeko la kodi na tozo mbalimbali.
2. Vita dhidi ya Corona ikiwamo chanjo na tahadhari husika.
3. Mahitajio ya katiba mpya.
(a) Kodi na Tozo:
Ongezeko la tozo za miamala na bei za mbolea yalikuwa ni sehemu ndogo sana ya hoja hii. Kodi kwenye mafuta ya magari imepelekea gharama zaidi katika nyanja zote (ikiwamo mbolea).
Tozo za miamala ni msumari wa ziada tu kwenye maswahiba ya kadhia hizi dhidi ya maisha ya mtanzania huyu.
Kwa uchumi wa mwananchi yupi kustahili maongezeko ya kodi au tozo zozote ndani ya janga hili la Corona? Vipi gharama za matibabu ya ugonjwa huu kuwa kwetu? Vipi vigogo kutolipa kodi? Vipi wizi kwa mujibu wa ripoti za CAG? Nk.
Kwa aliyoyaongelea SSH, hoja hii hadi sasa itakuwa imesikika kiwango kidogo sana.
(b) Vita dhidi ya Corona:
Hili lilikuwa la dharura na kipaumbele sana. Mengine yote yanakuwa na maana iwapo tu tuko hai. Pamoja na mapungufu yote, la msingi zaidi hapa ni kuwa, hatimaye chanjo inaanza kutolewa leo.
Kwa vile tokea pale mtu atakapokuwa ameipokea, Corona itakuwa imegeuka kuwa historia kwake, basi hili litakuwa liko pazuri.
Inatia moyo kuwa hoja hii imesikika.
(c) Katiba mpya:
SSH hakugusia lolote kuhusu katiba mpya, kadhia ya Mwanza wala lolote kuhusiana na maridhiano.
Mama hajasikia na hafahamu lolote lililotokea Mwanza wala mwendelezo wake.
Mama hatambui kuwa tuna tatizo lolote katika umoja wetu linalomhitaji yeye kwa dharura kama kiongozi wa taifa.
Hoja hii haijasikika kabisa.
Sauti itakuwa haitoshi.
Asilaumiwe msikilizaji kwa usikivu kwake kuwa mdogo.
Sauti haitoshi!
Ninawasilisha.