Tafakari yetu
JF-Expert Member
- Apr 19, 2021
- 1,502
- 4,408
Kuna dhuluma kubwa na utapeli mwingi unatendeka kwenye kipimo cha futi kinachotumiwa katika upimaji na ugawaji kwa wasiojua. Kipimo cha futi ni cha kufikirika tu na zaidi kinatumika kipimo hicho kuficha ukweli halisi wa udogo wa viwanja vinavyotolewa.
Kwa mfano, unakuta kiwanja unaambiwa kina ukubwa futi 50 kwa 40 ambacho ni sawa kusema futi za mraba 2000 ambazo ni sawa na mita za mraba 186. Kipimo cha futi kimetumika kuficha ukweli halisi wa mita za mraba 186 ambacho ni kidogo mno.
Pia, kipimo cha futi ni hatari katika upangaji wa miji kisasa. Kinachochea ujenzi holela kwa sababu ya ufinyu wa kiwanja mtu alichonacho.
Ombi kwa serikali kabla hatujawa na miji mingine kama Manzese, Gongolamboto na mingine, upimaji na ugawaji wa viwanja wa namna hii upigwe marufuku.