Serikali: Marufuku wananchi kulipishwa kipimo na kuuziwa dawa za malaria

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Amebainisha hayo jana Julai 14,2023 wakati akizungumza na Wananchi alipotembelea kituo cha Afya Negezi wilayani Kishapu.

Alisema ni marufuku mwananchi kulipia kipimo cha malaria kile cha kudungwa kidole, dawa ya Alu, SP, na Sindano ya malaria kali, isipokuwa kipimo cha BS ndicho wanapaswa kulipia.

"Mwananchi ukitozwa hela yoyote nipigie simu, hakuna kutoa pesa matibabu ya Malaria ni bure, isipokuwa kipimo cha BS," alisema Waziri Ummy.

Aidha, aliwataka wananchi kuendelea kumuombea Afya njema Rais Samia, ili aendelee kuwaletea maendeleo watanzania ikiwamo kuboresha huduma za Afya na kupata matibabu bora.

Alisema serikali kupitia Wizara hiyo ya Afya,itaendelea kutatua changamoto moja baada ya nyingine katika huduma za Afya, likiwamo la upungufu wa watumishi, Magari ya Wagonjwa pamoja na kuongeza Majengo yakiwamo ya huduma ya Mama na Mtoto.

"Katika wilaya hii ya Kishapu tutaendelea kuboresha huduma za Afya, pamoja na kutoa Magari Matatu ya Wagonjwa, mawili yatatolewa na TAMISEM na Moja kwenye Wizara yangu," alisema Waziri Ummy.

Naye Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo, alimpongeza Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi wilayani humo na kuboresha utolewaji wa huduma za Afya ikiwamo na kujengwa vituo vya Afya na Zahanati.

Nao baadhi wa Wananchi wilayani Kishapu akiwamo Ester Lugangeka, wameishukuru Serikali kwa ujenzi wa huduma hizo za Afya kuwa karibu na makazi yao zikiwamo huduma za upasuaji na kuokoa Afya zao.


Chanzo: Nipashe
 
Hayo yote wanataka kuturudisha nyuma imapambano kuhusu DPW?,wambie wametoa Tozo ila bado tunataka bandari yetu,na ili la kipimo bure wambie bado tunataka Bandari yetu...wameleta mademu wa sudani ila bado tukataka bandari yetu...wakataka liishe Samia haachie nchi yetu na afute mkataba huo wa kijinga na kitapeli.
 
Ni miye tu ambaye naona kama kuna ukinzani na yale ya kuwachia Madaktari wafanye biashara kwenye mali za umma/hospitali za Serikali? Watakuwa wanachaji nini?

Hili suala lipelekwe mahakamni na yeyoye yule atakayechajiwa na Daktari yeyote yule anayetumia eneo la Umma/Ofisi ya Serikali!

au Nimejichanganya hapa.
 
Back
Top Bottom