Serikali kuwalipa Posho na kuwalinda Watoa Taarifa na Mashahidi wa Mahakamani

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Una hofu ya usalama katika ushahidi? Huna sababu tena ya kujenga wasiwasi baada ya Serikali kuweka wazi mwongozo wa kuwajali na kuwalinda mashahidi kabla na baada ya kutoa ushahidi mahakamani.

Kwa sasa mtoa taarifa aliyejitambulisha kutoa ushirikiano, atahakikishiwa kutunziwa siri ya taarifa zote alizotoa. Pili, atasafirishwa kwa gharama za Serikali kutoka mahali aliko na kuhifadhiwa katika makazi yenye faragha bila kuathiri uhuru wake wakati wa utoaji wa ushahidi.

Pia, mwongozo huo unaelekeza kuwajali watu wenye mahitaji maalumu kabla na baada ya kutoa ushahidi bila kuathiri utu wao.

Waathirika, wakiwamo waliofanyiwa vitendo vya ubakaji au kujeruhiwa vinginevyo wanahakikishiwa usalama usiosababisha madhara zaidi na kuathiri uhuru wao wakati wa ushahidi mahakamani na baada ya kutoa ushahidi watawekewa mazingira ya kufuatiliwa usalama wao.

Mwongozo huo chini ya Sheria ya Ulinzi wa Mtoa taarifa na mashahidi Sura 446 ulikuwa ni sehemu ya miongozo mitatu iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Pindi Chana.

“Shahidi wamekuwa wakiogopa kutoa ushahidi kwa sababu mazingira yote yanakuwa yakionyesha anaonekana kwenda kutoa ushahidi, kwa hiyo mwongozo huu umeweka ulinzi wa kutosha kuhakikisha anatoa ushirikiano kwa kulinda usalama wake,” alisema Dk Pindi.

Dk Pindi alitoa wito kwa Watanzania wote kutokuwa na hofu tena wanapohitajika kutoa ushahidi mahakamani, akisema ushahidi husaidia kupunguza matukio ya uhalifu nchini.

Naye Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP), Slyvester Mwakitalu, alisema mwongozo huo kuanzia hatua ya upelelezi, shahidi ataanza kuhusishwa ili kuwezesha viwango vya uchunguzi na mashtaka kabla ya kuamua kufungua shtaka au la.

“Kwa hiyo miongozo hii itakuwa msaada mkubwa katika kurahisisha, kuongeza ufanisi wakati wa mashtaka na kuimarisha mfumo wote wa hakijinai.”

Julai mwaka huu, Tume ya Kuboresha mfumo wa Hakijinai iliwasilisha ripoti yake kwa Rais Samia Suluhu Hassan, aliyeiteua Januari mwaka huu kwa lengo la kuimarisha mfumo huo.

Kwanini miongozo

Kabla ya kuzindua, Dk Pindi alisema pamoja na kuwepo kwa sheria husika, ilionyesha uhitaji mkubwa wa kuanzisha miongozo hiyo ili kuongeza ufanisi zaidi katika ushirikiano wa shahidi.

Kuhusu mwongozo unaoweka taratibu za ushirikiano wa kimataifa Mwakitalu alisema licha ya sheria kutoa mwelekeo katika ukusanyaji wa ushahidi na vielelezo lakini yako maeneo hayakubainishwa. “Kwa mfano namna ya kupokea na kutoa ushahidi nchi zinazoomba, muda wa uchunguzi.”

MWANANCHI
 
Siku zote hili kwa nini lisingekuwa linafanyika ,sasa tutaanza kufunguka ,na posho ya ushuhuda iwe wazi kama zilivyo wazi faini za makosa
 
Labda kama siyo bongo! Jichanganye uone!
Tangu lini wabongo wanatunza siri? Fikiria kwa nini wamesema mahakama inatenda haki, kinyume chake haki ya bongo inakuwa determined na pesa.

Bongo ni minyeyusho tu.
 
Labda kama siyo bongo! Jichanganye uone!
Tangu lini wabongo wanatunza siri? Fikiria kwa nini wamesema mahakama inatenda haki, kinyume chake haki ya bongo inakuwa determined na pesa.

Bongo ni minyeyusho tu.
Miyeyuso kutoa ushahidi au? watu mbona wanatoa ushahidi muda tu, na watu wanafungwa kabla hata ya hiyo posho sijui kutunza Siri.
 
Wit sec kama ya Marekani ndo yatakiwa
Mtu apewe ID mpya na maisha mapya
 
Back
Top Bottom