Serikali: Kichwa cha Treni kilichopata ajali Kigoma si moja ya vilivyokutwa Bandarini Dar

singojr

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
5,308
6,884
Leo kupitia taarifa ya habari ya Azam two waziri Mbarawa amekanusha uvumi unaoendelea mitandaoni kuwa kichwa cha treni kilichopinduka sio vile vilivyokamatwa na Rais Magufulu bandari.

Awali kuliibuka mjadala JF ikihusisha kichwa cha treni kilichopata ajali Kigoma chenye namba 9001 kuwa ni moja kati ya vichwa vilivyokuwa bandarini Dar ambavyo havikuwa na mmiliki na Serikali kusema itavinunua. Zaidi soma => Maajabu ya CCM: Kichwa cha treni kilichookotwa bandarini ndio kimepata ajali Kigoma. Hivi kumbe walishanunua kimyakimya?

Pia soma...
- Vichwa 15 vya treni kununuliwa na Serikali
- Ununuzi wa vichwa vya treni: Waziri Mbawara katofautiana na bosi wake?

My Take:

Viongozi mnadhani kwa elimu mbovu tuliyoipata hata haya yanayoonekana mtatudanganya?
 
Dharau hizi, eti vichwa vinafanana series wakati inaonekana namba nzima. Hii kuwafanya wananchi mazuzu ndio itawaangusha siku moja.
Duh, Basi Ndugu yangu Bwana Mabawa, ni kweli nitofauti! Yaishe hahahahaha
0cafc65b6e582f89e3bf5ee1ec5d3a7f.jpg
 
Back
Top Bottom