Serikali iyafanyie kazi maoni ya HakiElimu

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Serikali iyafanyie kazi maoni ya HakiElimu
ban.blank.jpg

Janet Josiah

amka2.gif
WALIMU ni kiungo muhimu katika sekta ya elimu nchini kuanzia ngazi ya masomo ya awali, msingi, sekondari na vyuo. Umuhimu elimu unaonekana pale mwalimu anapomfundisha mtu ambaye hapo baadae anafanikiwa kimaendeleo kutokana na elimu aliyoipata.
Kutokana na mwalimu kuwa nguzo katika maendeleo ya elimu, itakuwa ndoto kwa serikali kufanikiwa katika nyanja ya elimu nchini kama itawaacha walimu bila kuwapa mafunzo katika vituo vyao vya kazi.
Sababu kubwa ya kutoa mafunzo kwa walimu waliopo kazini ni kutaka kuwabadilisha ili awaweze kutumia mbinu mpya za kazi zinazotokana na kukua kwa teknolojia.
Kukua kwa teknolojia ni pale ambapo mwalimu ataweza kupata mafunzo ya kuijua na kuitumia kompyuta pamoja na kupata mbinu za kisasa za kumfundisha mwanafunzi ili asiweze kuchoka.
Kwa mfano mwalimu aliyemaliza chuo miaka ya 1960, hawezi kufanana kiutendaji na mwalimu aliyemaliza chuo miaka mitano au kumi iliyopita.
Mashirika na asasi mbalimbali zinazojihusisha na masuala ya elimu zimekuwa zikitoa semina, warsha na hata makongamano kuhusu changamoto zitokanazo na sekta ya elimu kwa walimu na wanafunzi.
Aprili 30 mwaka huu HakiElimu kwa kushirikiana na Taasisi ya Vituo vya Walimu Tanzania (TRCC) ilizindua shindano la insha na michoro linalouliza: “Je, mafunzo ya walimu kazini yana umuhimu gani katika kuboresha elimu Tanzania?”
Lengo lilikuwa ni kupata mawazo na maoni ya wananchi juu ya umuhimu wa mafunzo ya walimu kazini; na kama yanatolewa kwa kiwango
 
Kutokana na mwalimu kuwa nguzo katika maendeleo ya elimu, itakuwa ndoto kwa serikali kufanikiwa katika nyanja ya elimu nchini kama itawaacha walimu bila kuwapa mafunzo katika vituo vyao vya kazi.
Sababu kubwa ya kutoa mafunzo kwa walimu waliopo kazini ni kutaka kuwabadilisha ili awaweze kutumia mbinu mpya za kazi zinazotokana na kukua kwa teknolojia.

Hivi serikali hii ya mafisadi inajali haya? Wao wanataka kutambia idadi ya wanafunzi wanaohitimu bila ya kujali wamejifunza nini...................Hiyo ndiyo CCM ya leo.......................
 
That's a situation everywhere! there is no seriousness on the end-product quality! sio kiwandani,shuleni wala vyuoni!
 
Back
Top Bottom