A
Anonymous
Guest
Kuna jambo ambalo nimekutana nalo nikiwa likizo huku Mkoa wa Songwe, Wilaya ya Mbozi, kuna baadhi ya Shule za Msingi, Walimu wanamiliki mashamba na kuwafanyisha kazi Wanafunzi.
Nimezungumza na baadhi ya Watoto wanasema ikifika Januari msimu wa kilimo shule wanatega na kwenda siku ambazo hakuna ratiba ya kuwapeleka shamba.
Kama ni mafunzo ya vitendo basi ingekuwa inafanyika shuleni au kwenye mashamba ya Shule lakini kibaya zaidi ni kuwa wanalazimika kwenda kulifuata shamba la Mwalimu au Walimu umbali wa Kilometa 2 ikiemo kuvuka mito.
Ujumbe huu uwafikie Wizara ya Elimu wajue hiki kinachoendelea kuhusu watumishi wao.