Serikali isilaumiwe kwa hali ngumu ya maisha-JK

Naomba hotuba za Kikwete zikome mana hana jipya. Tusubiri November mosi au akizungumza na Wahariri.

Naomba kuwakilisha....
 
Hii 'Global credit crunch' ni kitu cha hivi karibuni ambacho athari zake bado hazijafika hapa kwetu,walichotaka kujua wana Mbeya hiyo miaka 3 ya utawala wa Kikwete mbona wanazidi kutaabika na hawaoni maisha bora aliewaahidi? FOOLSTOP!

NB:Sisi tunauza dhahabu inabidi tuchekelee kwakua bei inazidi kupanda kila kukicha.Tungepata kilicho haki yetu kutokana na madini mbona tungekua mbali kama Botswana.
 
Hivi huyu Kikwete ni rais gani ? anafikiri kweli kabla ya kuzungumza ? Hivi kweli tunategemea nchi yetu itaendelea wakati Rais anazungumza vitu kama yuko kijiweni ?
 
Muungwana ndivyo alivyo. Hajifanyishi. Yawezekana tulikuwa hatujui au hatuamini vile alivyo ndivyo alivyo katika maana halisi.

TUMUOMBE TU MUNGU. KAZI IPO!!!!!!!!!!
 
Serikali isilaumiwe kwa hali ngumu ya maisha-JK

2008-10-13 10:24:10
Na Thobias Mwanakatwe, Kyela

Rais Jakaya Kikwete amesema kushuka kwa uchumi wa dunia hivi sasa ni lazima kutaathiri uchumi wa taifa, na hivyo hakuna sababu kwa wananchi kulaumu kwamba serikali inawatesa kutokana na hali ngumu ya maisha.

Akiwahutubia wananchi wa mji wa Kyela juzi, alisema hivi sasa uchumi wa dunia umekumbwa na msukosuko mkubwa kuliko yote katika historia toka mwaka 1930 ambapo hali hiyo haijawahi kujitokeza.

Alisema pamoja na kuwepo kwa msukosuko huo wa uchumi wa dunia, hata hivyo serikali bado haijaanza kujipanga kukabiliana na hali hiyo lakini baada ya miezi michache ijayo athari zitaanza kujitokeza.

Hata hivyo, Rais Kikwete alisema serikali inaendelea kutafakari ni jinsi gani itaikabili hali hiyo ili kusijitokeze athari zaidi katika uchumi.

Alisema hivi sasa kutokana na msukosuko wa uchumi, serikali ya Marekani imetenga Dola 700 bilioni kujaribu kuokoa mabenki yanayofilisika, mkakati ambao pia unafanywa na Uingereza,Ujerumani, Japan pamoja na nchi nyingine.

``Wenzetu wanao uwezo mkubwa wa kiuchumi sijui yakitufika sisi itakuwaje, tunaendelea kutafakari ili na sisi yatakapotukuta tufanye nini lakini siyo kazi rahisi,`` alisema Rais Kikwete.

Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo hakuna sababu kwa wananchi kulalamika kuwa serikali inatutesa kwa sababu kushuka kwa uchumi wa dunia athari zake zinazikumba nchi maskini ikiwemo Tanzania.

SOURCE: Nipashe

Binafsi simwelewi
 
Alisema pamoja na kuwepo kwa msukosuko huo wa uchumi wa dunia, hata hivyo serikali bado haijaanza kujipanga kukabiliana na hali hiyo lakini baada ya miezi michache ijayo athari zitaanza kujitokeza.

Hata hivyo, Rais Kikwete alisema serikali inaendelea kutafakari ni jinsi gani itaikabili hali hiyo ili kusijitokeze athari zaidi katika uchumi."

WADAU MNAONA KIINI MACHO HIKI??
Tunashukuru sana kwa mkuu wa nchi yetu KUKIRI KWA KINYWA CHAKE kwamba bado hawajajiandaa wala kujipanga katika kukabiliana na umaskini nchini JAMANI WATANZANIA BADOOOOO MUWE MNAMUELEWA KIONGOZI WENU.
KIKWETE mwaka wa nne huo unaingia wa utawala wako BADO TU MNATAFAKARI??
 
"Nilifika Kenya nikakuta kila mtu amekata tamaa lakini nikaleta matumaini" Wakati wa kuunda coalition government hapo.

"Sijui kwa nini Tanzania ni maskini".Raisi huyo tena wa Tanzania akiwa Paris.

"Huu ni ukumbi wenye Vionjo na burudani zote stahiki". Duh,Rais akifungua ukumbi mpya wa bunge hapo.
 
Ndugu zangu msitegemee makubwa kutoka kwa JK. Raisi wetu ni mtupu kichwani. Sana sana yeye alitaka kuupata uraisi. Ndio lengo hilo. Sidhani kama aliwazia kuwatumikia watanzania kupitia uraisi.
 
Siku watoto wa shule za msingi walipo andamana kupinga nauli yao kuongezwa kutoka 50/= mpaka 100/= walibeba mabango ambayo mengine yalisema,'maisha bora kwa kila fisadi','serikali gani inakaba mpaka penati','mshahara wa baba 120,000/= anatakiwa kutupa malazi,chakula, mavazi,dawa,nauli na mengineyo mama hafanyi kazi Kikwete panga bajeti'.Haya wameyaona watoto wetu wa shule za msingi!!
 
Do we have (Tanzania) any share in FTSE or Newyork stock exchange? I hope we dont, so how come Tanzania Economy will be affected?

I know, may be because we will no longer receiving grant; that why Mr JK worry about that.
But he (JK ) need to be specific about that.
 
..ziara moja ya kikwete ulaya inagharimu tzs bilioni moja ...thats true...kikwete huyu ndie aliyemchafua sumaye alipofanya ziara ya siku 10 marekani iliyogharimu milioni 500[ambako alifanikiwa kuingia mkataba wa ujenzi wa chuo kikuu na refferal hospital inayomilikiwa na kanisa anglikan dodoma st john,at least alirudi na kitu]..that was 4 years ago.....LEO GHARAMA ZIMEPANDA KIASI ZIARA YA WIKI MOJA YA RAIS MAREKANI INAGHARIMU 1 MILLION DOLLARS...SASA UKIZINGATIA ZIARA ZAKE NYINGINE ZINAFIKIA HADI WIKI 3......NA AMESHASAFIRI MARA NANE KWA MWAKA HUU TU............INAKADIRIWA KUWA MWAKA HUU PEKEE KIKWETE AMESHATUMIA DOLA MILIONI KUMI[USD 10,000,000]...HIYO NI KWENDA MAREKANI TU......SIJAONGELEA ZIARA ZA ULAYA ,ASIA,AFRIKA,ETS................

IKULU TUAMBIENI FUNGU LA ZIARA ZA RAIS PEKEE KWA MWAKA NI DOLA MILIONI 100???...SAY SHILINGI BILIONI 120..............................PESA ANAZOTUMIA RAIS KWA ZIARA ZA NJE ZINATOSHA KUGHARIMIA BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI...ANATUMIA PEKE YAKE............TUNAFAIDIKA NINI!!!!
 
Serikali isilaumiwe kwa hali ngumu ya maisha-JK

2008-10-13 10:24:10
Na Thobias Mwanakatwe, Kyela

Rais Jakaya Kikwete amesema kushuka kwa uchumi wa dunia hivi sasa ni lazima kutaathiri uchumi wa taifa, na hivyo hakuna sababu kwa wananchi kulaumu kwamba serikali inawatesa kutokana na hali ngumu ya maisha.

Akiwahutubia wananchi wa mji wa Kyela juzi, alisema hivi sasa uchumi wa dunia umekumbwa na msukosuko mkubwa kuliko yote katika historia toka mwaka 1930 ambapo hali hiyo haijawahi kujitokeza.

Alisema pamoja na kuwepo kwa msukosuko huo wa uchumi wa dunia, hata hivyo serikali bado haijaanza kujipanga kukabiliana na hali hiyo lakini baada ya miezi michache ijayo athari zitaanza kujitokeza.

Hata hivyo, Rais Kikwete alisema serikali inaendelea kutafakari ni jinsi gani itaikabili hali hiyo ili kusijitokeze athari zaidi katika uchumi.

Alisema hivi sasa kutokana na msukosuko wa uchumi, serikali ya Marekani imetenga Dola 700 bilioni kujaribu kuokoa mabenki yanayofilisika, mkakati ambao pia unafanywa na Uingereza,Ujerumani, Japan pamoja na nchi nyingine.

``Wenzetu wanao uwezo mkubwa wa kiuchumi sijui yakitufika sisi itakuwaje, tunaendelea kutafakari ili na sisi yatakapotukuta tufanye nini lakini siyo kazi rahisi,`` alisema Rais Kikwete.

Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo hakuna sababu kwa wananchi kulalamika kuwa serikali inatutesa kwa sababu kushuka kwa uchumi wa dunia athari zake zinazikumba nchi maskini ikiwemo Tanzania.

SOURCE: Nipashe

what about EPA,RICHMOND KIWIRA NA RADDER MR PRESIDENT??
 
Back
Top Bottom