Serikali ipo tayari kukutana na Chadema...kulikoni?

Wazee, nawambieni Mataifa Wahisani wanatema cheche balaa huko nyuma ya pazia. Yote tunayafahamu, na bado patamu zaidi panakuja!!! Wanaoshinwa kuaminika na watu anaowaongoza 'Wapende Wasipende' ataaminika vipi nje ya nchi??

CHADEMA si mahala pa CCM kuja kuoshea mikono yake michafu kiujanjaujanja, tuunde kwanza chombo cha kitaifa cha kushughulikia maswala ya kupatikana KATIBA MPYA halafu sisiemu tutakutana huko huko mkutanoni chini ya chombo hiki.

Maadam walishatia mioyo yao migumu, Wananchi Uwezo Tunao wa kujiletea aina ya mabadiliko yanayoendana na maslahi yetu kama taifa.
 
Thanks luteni, And U Dar Es salaam u have mental disorder, almost chizi ww,
but luteni the biggest, wrong defined & misused word here is MASLAHI YA TAIFA MBELE, tena najisikia vibaya sana
wanatamka hovyo theoretically while they do opposite, kama maslahi ya Taifa yangewekwa mbele kusingekuwa
na ufisadi, worst contracts, magari luxury ya bei ya uongo, ATC, TRL, EPA tusingekuwa nayo, na watu wa kuwalaumu ni CCM na serikali yake, sasa Wasira kwanza he should know practical definition what is Maslahi ya Taifa,(najua anajua ila yy anaongea maneno, vitendo tofauti) kila wakati, Maslahi ya taifa, maslahi ya Taifa, but for them opposite is true, no faith on him

hata ccm kunyanganya kura za opposition ni maslahi ya taifa?. Hatuoni yaliyo tokea kwa pwani ya ndovu?!
 
So MAKAMBA katofautiana na WAZIRI that means kuna mmoja yupo sawa na Mwingine Wrong...Mimi hapa sijui nani yupo sahihi katika maamuzi though naweza tumia uzoefu wa nani huwa anakua wrong most of the times ( MAKAMBA) koz ndiyo mlopo.....lakini nani ni BOSS kati Ya Katibu wa CHAMA na WAZIRI???? Its time up tuanze kuchukuliana hatua on every stupid mistakes hata kama oral Mistakes.......................
 
SERIKALI imesema iko tayari kukaa meza moja na chama cha upinzani cha Chadema au taasisi nyingine yoyote itakayotaka kujadiliana kuhusu mustakabali wa taifa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira alisema kuwa serikali iko tayari kwa mazungumzo hayo iwapo yataweka mbele maslahi ya taifa.
Kauli ya Wassira imetolewa wakati Chadema ikiendelea na msimamo wake wa kutoyatambua matokeo ya uchaguzi wa urais, ikitaka kuundwa kwa tume huru ya kuchunguza utangazaji wa matokeo hayo; kuandikwa kwa katiba mpya na kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi.

Chadema, ambayo ilitangaza msimamo huo mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu, ilithibitisha kwa vitendo kauli hiyo wakati wabunge wake walipotoka kwenye ukumbi wa Bunge wakati Rais Jakaya Kikwete akianza kukihutubia chombo hicho.
Baadaye, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza kuwa chama hicho kiko tayari kukaa meza moja na serikali au taasisi yoyote kujadili suala hilo kwa kuzingatia maslahi ya taifa.
Lakini katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alibeza kauli hiyo ya Mbowe kwa kusema kuwa chama hicho tawala hakina muda wala sababu ya kuketi pamoja na wapinzani hao na kwamba baada ya rais kupatikana, siasa sasa zinahamia bungeni.

Jana Waziri Wassira alitoa kauli tofauti na ya katibu wake mkuu alipoiambia Mwananchi kuwa wako tayari kukaa meza moja na Chadema, chama au taasisi yoyote ikiwamo za dini na kwamba mazungumzo watayoyalenga ni yale yatakayohakikisha yanaweka mbele maslahi ya taifa.
“Lakini nasisitiza serikali haina mgogoro na viongozi wa dini au chama chochote bali milango ipo wazi kwa vyama vyote 18 na taasisi zote," alisema waziri huyo ambaye aliwahi kuwa kwenye upinzani baada ya kuihama CCM na kujiunga na NCCR-Mageuzi miaka ya tisini.

"Majadiliano yasichukue sura ya kisiasa au udini kwa kuwa kufanya hivyo hakutafanikisha kufikiwa kwa maslahi bora ya baadaye ya nchi.
“Lengo la serikali ni kuhakikisha taifa hili linalifikishwa mahali ambapo amani na utulivu itaendelea kuwepo.”
Hata hivyo, Waziri huyo alisema kama kutatokea matatizo au kutoelewana, serikali ina njia na taratibu zake inazozitumia kukutana na walengwa kutatua hali hiyo na kwamba hatua hizo huwa hazitangazwi kwenye vyombo vya habari.

Wakati akifafanua msimamo huo wa Chadema kwa waandishi wa habari, Mbowe alisema mazungumzo watakayoyalenga ni yale yatakayohakikisha kuwa madai yao yanafikiriwa kwa kina huku maslahi ya taifa yakiwekwa mbele.
Mbowe alisema wanafurahi kuona kuwa kitendo chao cha kutoka bungeni wakati wa hotuba ya Rais Kikwete kimesaidia kuibua mjadala mzito nchini ambao iwapo utapewa nafasi ya kujadiliwa bila kuweka ushabiki wa kisiasa, nchi inaweza kupata mabadiliko makubwa siku za usoni.

Alitoa mfano kauli ya waziri mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba na Jaji Mkuu Augustino Ramadhani ambao walikaririwa wakisema kuwa suala la katiba mpya ni muhimu.
“Maoni kama haya, ambayo yanatoka kwa watu wazito kama hawa, yanaonyesha kuwa kitendo chetu kimeamsha mjadala wa maana kwa taifa hili,” alisema.
Chadema, ambayo ilionekana kama haingesimamisha mgombea urais baada ya Mbowe kuamua kugombea ubunge wa Jimbo la Hai, iliibukia kuwa mpinzani mkuu wa CCM baada ya kumtangaza mbunge wa zamani wa Karatu, Dk Willibrod Slaa kuwa mgombea urais.

Dk Slaa, ambaye alikuwa akivutia maelfu ya watu kwenye mikutano yake ya kampeni ambako alikuwa akihubiri elimu ya bure na upunguzaji wa bei za vifaa vya ujenzi, alitangaza kutokubaliana na mwenendo wa utangazaji matokeo ya uchaguzi wa rais na kuitaka Tume ya Uchaguzi (Nec)kusimamisha zoezi hilo.
Lakini Nec iliendelea na utangazaji matokeo na baadaye kumtangaza Jakaya Kikwete kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais, tamko ambalo liliifanya Chadema kutangaza msimamo wake wa kutotambua matokeo ya uchaguzi wa rais
 
I guess you might be right; these thugs must have been squeezed somewhere.

Huo ndio ukweli. Alichokuwa anakiongea Makamba ndio msimamo wa chama na walikuwa wamepanga kupiga danadana hi issue mpaka 2015. Lakini baada ya serikali kukalishwa kitako na balozi wa EU na mabalozi wengine na kuambiwa waache hamnazo ndio wanaanza kuja na kauli zinazokinzana. Lakini hii mie naona ni geresha tu sidhani kwa wanao dhamira ya kweli ya kutatua hili suala. Wanapoanza kugusia amani na utulivu na kusema hawana ugomvi na viongozi wa dini wala mgogoro na vyama vya siasa nashindwa kuelewa. Itakuwaje hawana mgogoro wakati CDM wamesusia hotuba ya ufunguzi wa bunge kwa kudai hawatambui matokeo ya uchaguzi wa rais? Kama hamna mgogoro kwanini mkutane? Halafu kumalizia kwa kusema kuna njia za siri za kumaliza matatizo yanayowahusu Watanzania wote??? Ina maana huo mchakato wa kupata katiba mpya utakuwa wa siri??
 
Kinachotakiwa ni kuanika uchafu wote wa sisiem na sirikali yake hadharani haswa mitandaoni maana hawa donners wanasoma na wanawauliza hizi habari kulikoni? ndio maana hawa mafisadi wanatumia ujanja wa media kwa ripoti kama za redet na kama walivyowatumia wajinga wachache wa udom kutoa maelezo ya kuwapamba sisiem na sirikali ili kupitia media hizo mabwana wakubwa huko walipo waone wako safi ila sababu ya wapenda maendeleo kuanika uchafu wao ndio wanakutana na vikwazo wanarudi kua wapole ila ni kuwapa sura mbuzi tuu mpaka kieleweke.
 
Waziri wa katiba na sheria amesema hakuna budget ya katiba mpya,bt budget ya sensa ipo,kati ya katiba na sensa kip ni cha muhmu sana kwa maslahi ya Taifa,ivi akisema kombani ,kikwete anaweza akapinga?tafakari kuhusu mustakabali wa nchi na chukua hatua.
 
chadema wasije wakachakachuliwa kwa vijisenti? mnakumbuka ya mtikila na maalim seif?
 
Hatutaki mambo ya CUF kuolewa AMA kuwa vimada wa CCM!

wameesha anza kijiba cha roho najua hao ni kafu upemba na kafu udini acheni hizo ni mazungumzo ! kwa ajili ya manufaa ya mama yetu TANGANYIKA
 
viongozi wa chadema mkitaka watanzania walioanza kuwakubali wawakatae nendeni huko kwenye vikao mkadanganywe na ccm baada ya kukataliwa na wahisani sasamaji yamewafika shingoni muone nguvu ya uma inavyofanya kazi.
nawapa masharti ya kukaa na hao mafisadi.
1.kipaumbele ni katiba mpya

2.waandishi wa habari ndio jicho la wananchi(na hao wahisani waliowashinikiza
3.makamba asiwepo.
4.mazungumzo yasiwe yakuwalainisha wafadhili bali yalenge kulikomboa taifa
peopless powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
 
Waziri wa katiba na sheria amesema hakuna budget ya katiba mpya,bt budget ya sensa ipo,kati ya katiba na sensa kip ni cha muhmu sana kwa maslahi ya Taifa,ivi akisema kombani ,kikwete anaweza akapinga?tafakari kuhusu mustakabali wa nchi na chukua hatua.

Sensa ni muhimu zaidi. Ukichakachua ukapitiliza idadi ya watu inakuwa nomaaaaa.
 
chadema wasije wakachakachuliwa kwa vijisenti? mnakumbuka ya mtikila na maalim seif?

Bahati nzuri ukimwacha Zitto Kabwe viongozi wa juu wa Chadema wana msimamo. Nilifadhaishwa sana na Zitto kummwabia Maria Kejo wa Sheria ( soma Mwanahalisi wiki hii) kwamba 'hana pesa"! What do you expect from such a politician?
 
SERIKALI imesema iko tayari kukaa meza moja na chama cha upinzani cha Chadema au taasisi nyingine yoyote itakayotaka kujadiliana kuhusu mustakabali wa taifa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira alisema kuwa serikali iko tayari kwa mazungumzo hayo iwapo yataweka mbele maslahi ya taifa.

Kauli ya Wassira imetolewa wakati Chadema ikiendelea na msimamo wake wa kutoyatambua (kupinga) matokeo ya uchaguzi wa urais, ikitaka kuundwa kwa tume huru ya kuchunguza utangazaji wa matokeo hayo; kuandikwa kwa katiba mpya na kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi.

Chadema, ambayo ilitangaza msimamo huo mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu, ilithibitisha kwa vitendo kauli hiyo wakati wabunge wake walipotoka kwenye ukumbi wa Bunge wakati Rais Jakaya Kikwete akianza kukihutubia chombo hicho.

Baadaye, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza kuwa chama hicho kiko tayari kukaa meza moja na serikali au taasisi yoyote kujadili suala hilo kwa kuzingatia maslahi ya taifa.

Lakini katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alibeza kauli hiyo ya Mbowe kwa kusema kuwa chama hicho tawala hakina muda wala sababu ya kuketi pamoja na wapinzani hao na kwamba baada ya rais kupatikana, siasa sasa zinahamia bungeni.

Jana Waziri Wassira alitoa kauli tofauti na ya katibu wake mkuu alipoiambia Mwananchi kuwa wako tayari kukaa meza moja na Chadema, chama au taasisi yoyote ikiwamo za dini na kwamba mazungumzo watayoyalenga ni yale yatakayohakikisha yanaweka mbele maslahi ya taifa.

“Lakini nasisitiza serikali haina mgogoro na viongozi wa dini au chama chochote bali milango ipo wazi kwa vyama vyote 18 na taasisi zote," alisema waziri huyo ambaye aliwahi kuwa kwenye upinzani baada ya kuihama CCM na kujiunga na NCCR-Mageuzi miaka ya tisini.

"Majadiliano yasichukue sura ya kisiasa au udini kwa kuwa kufanya hivyo hakutafanikisha kufikiwa kwa maslahi bora ya baadaye ya nchi.

“Lengo la serikali ni kuhakikisha taifa hili linalifikishwa mahali ambapo amani na utulivu itaendelea kuwepo.”

Hata hivyo, Waziri huyo alisema kama kutatokea matatizo au kutoelewana, serikali ina njia na taratibu zake inazozitumia kukutana na walengwa kutatua hali hiyo na kwamba hatua hizo huwa hazitangazwi kwenye vyombo vya habari.

Wakati akifafanua msimamo huo wa Chadema kwa waandishi wa habari, Mbowe alisema mazungumzo watakayoyalenga ni yale yatakayohakikisha kuwa madai yao yanafikiriwa kwa kina huku maslahi ya taifa yakiwekwa mbele.

Mbowe alisema wanafurahi kuona kuwa kitendo chao cha kutoka bungeni wakati wa hotuba ya Rais Kikwete kimesaidia kuibua mjadala mzito nchini ambao iwapo utapewa nafasi ya kujadiliwa bila kuweka ushabiki wa kisiasa, nchi inaweza kupata mabadiliko makubwa siku za usoni.

Alitoa mfano kauli ya waziri mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba na Jaji Mkuu Augustino Ramadhani ambao walikaririwa wakisema kuwa suala la katiba mpya ni muhimu.

“Maoni kama haya, ambayo yanatoka kwa watu wazito kama hawa, yanaonyesha kuwa kitendo chetu kimeamsha mjadala wa maana kwa taifa hili,” alisema.

Chadema, ambayo ilionekana kama haingesimamisha mgombea urais baada ya Mbowe kuamua kugombea ubunge wa Jimbo la Hai, iliibukia kuwa mpinzani mkuu wa CCM baada ya kumtangaza mbunge wa zamani wa Karatu, Dk Willibrod Slaa kuwa mgombea urais.

Dk Slaa, ambaye alikuwa akivutia maelfu ya watu kwenye mikutano yake ya kampeni ambako alikuwa akihubiri elimu ya bure na upunguzaji wa bei za vifaa vya ujenzi, alitangaza kutokubaliana na mwenendo wa utangazaji matokeo ya uchaguzi wa rais na kuitaka Tume ya Uchaguzi (Nec)kusimamisha zoezi hilo.

Lakini Nec iliendelea na utangazaji matokeo na baadaye kumtangaza Jakaya Kikwete kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais, tamko ambalo liliifanya Chadema kutangaza msimamo wake wa kutotambua matokeo ya uchaguzi wa rais.

CHANZO: Mwananchi

Hapo kwenye RED, nafikilri HUWA NDO MNAPOTOSHA SAAAAAAANA wananchi... Ipo tofauti kubwa sana kati ya KUTOTAMBUA/kupinga MATOKEO YA RAIS na KUPINGA MCHAKATO ULIOMUWEKA RAIS MADARAKANI.

CHADEMA hawajasema hawatambui matokeo ya urais BALI WANAOPINGA/HAWAKUBALIANI na mchakato uliomuweka RAIS madarakani... ndo maana wanakubali ipo serikali..... walipigakura katika uchaguzi wa PM na Spika na wanaitambua serikali LAKINI SIO MCHAKATO ULIOMUWEKA MKUU WA SERIKALI (rais).

Kabla hujajibu kwa kukurupuka naomba RUDI nyuma anza na vyanzo ndo ujibu

Nawasilisha
 
SERIKALI imesema iko tayari kukaa meza moja na chama cha upinzani cha Chadema au taasisi nyingine yoyote itakayotaka kujadiliana kuhusu mustakabali wa taifa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira alisema kuwa serikali iko tayari kwa mazungumzo hayo iwapo yataweka mbele maslahi ya taifa.

Kauli ya Wassira imetolewa wakati Chadema ikiendelea na msimamo wake wa kutoyatambua matokeo ya uchaguzi wa urais, ikitaka kuundwa kwa tume huru ya kuchunguza utangazaji wa matokeo hayo; kuandikwa kwa katiba mpya na kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi.

Chadema, ambayo ilitangaza msimamo huo mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu, ilithibitisha kwa vitendo kauli hiyo wakati wabunge wake walipotoka kwenye ukumbi wa Bunge wakati Rais Jakaya Kikwete akianza kukihutubia chombo hicho.

Baadaye, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza kuwa chama hicho kiko tayari kukaa meza moja na serikali au taasisi yoyote kujadili suala hilo kwa kuzingatia maslahi ya taifa.

Lakini katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alibeza kauli hiyo ya Mbowe kwa kusema kuwa chama hicho tawala hakina muda wala sababu ya kuketi pamoja na wapinzani hao na kwamba baada ya rais kupatikana, siasa sasa zinahamia bungeni.

Jana Waziri Wassira alitoa kauli tofauti na ya katibu wake mkuu alipoiambia Mwananchi kuwa wako tayari kukaa meza moja na Chadema, chama au taasisi yoyote ikiwamo za dini na kwamba mazungumzo watayoyalenga ni yale yatakayohakikisha yanaweka mbele maslahi ya taifa.

"Lakini nasisitiza serikali haina mgogoro na viongozi wa dini au chama chochote bali milango ipo wazi kwa vyama vyote 18 na taasisi zote," alisema waziri huyo ambaye aliwahi kuwa kwenye upinzani baada ya kuihama CCM na kujiunga na NCCR-Mageuzi miaka ya tisini.

"Majadiliano yasichukue sura ya kisiasa au udini kwa kuwa kufanya hivyo hakutafanikisha kufikiwa kwa maslahi bora ya baadaye ya nchi.

"Lengo la serikali ni kuhakikisha taifa hili linalifikishwa mahali ambapo amani na utulivu itaendelea kuwepo."

Hata hivyo, Waziri huyo alisema kama kutatokea matatizo au kutoelewana, serikali ina njia na taratibu zake inazozitumia kukutana na walengwa kutatua hali hiyo na kwamba hatua hizo huwa hazitangazwi kwenye vyombo vya habari.

Wakati akifafanua msimamo huo wa Chadema kwa waandishi wa habari, Mbowe alisema mazungumzo watakayoyalenga ni yale yatakayohakikisha kuwa madai yao yanafikiriwa kwa kina huku maslahi ya taifa yakiwekwa mbele.

Mbowe alisema wanafurahi kuona kuwa kitendo chao cha kutoka bungeni wakati wa hotuba ya Rais Kikwete kimesaidia kuibua mjadala mzito nchini ambao iwapo utapewa nafasi ya kujadiliwa bila kuweka ushabiki wa kisiasa, nchi inaweza kupata mabadiliko makubwa siku za usoni.

Alitoa mfano kauli ya waziri mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba na Jaji Mkuu Augustino Ramadhani ambao walikaririwa wakisema kuwa suala la katiba mpya ni muhimu.

"Maoni kama haya, ambayo yanatoka kwa watu wazito kama hawa, yanaonyesha kuwa kitendo chetu kimeamsha mjadala wa maana kwa taifa hili," alisema.

Chadema, ambayo ilionekana kama haingesimamisha mgombea urais baada ya Mbowe kuamua kugombea ubunge wa Jimbo la Hai, iliibukia kuwa mpinzani mkuu wa CCM baada ya kumtangaza mbunge wa zamani wa Karatu, Dk Willibrod Slaa kuwa mgombea urais.

Dk Slaa, ambaye alikuwa akivutia maelfu ya watu kwenye mikutano yake ya kampeni ambako alikuwa akihubiri elimu ya bure na upunguzaji wa bei za vifaa vya ujenzi, alitangaza kutokubaliana na mwenendo wa utangazaji matokeo ya uchaguzi wa rais na kuitaka Tume ya Uchaguzi (Nec)kusimamisha zoezi hilo.

Lakini Nec iliendelea na utangazaji matokeo na baadaye kumtangaza Jakaya Kikwete kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais, tamko ambalo liliifanya Chadema kutangaza msimamo wake wa kutotambua matokeo ya uchaguzi wa rais.

CHANZO: Mwananchi
Hapo kwenye red, kuna haja gani ya kusubiri mpaka WATAKE?? Serikali inatakiwa ikinge, izuie, iponye, na kuratibu harakati zote kwa umakini kwa ustawi wa taifa. Ndiyo maana waheshimiwa wetu mnapewa stahili zote. Kelelekelele zilizopo ni dalili mbaya kwa mstakabali wa taifa. Amkeni.
 
Tayari Dhamiri zimeanza kuwasuta Kikwete na serikali yake!!!!! Wanaona mbele giza zito!!!!!, ndiyo maana wameanza kutafuta pa kupumulia na kutokea!!! Wasubiri vikao vya bunge vianze basi, mbona mapema mno?????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!Inafikia mahali mwizi anajuta kwa nini ameiba!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Kikwete tayari ameanza kuona dalili mbaya si mbali kutoka hapa! Yeye akitaka watanzania wamsamehe na kusahau, afanye haraka kutekeleza sera ya Chadema kuhusu kuundwa Tume Huru ya Uchaguzi, na mchakato wa dhati Kuandika Katiba Mpya!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! ili kabla ya 2015 tuwe na Tanzania Mpya!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom