Serikali ipo tayari kukutana na Chadema...kulikoni?

kiherehere said:
...CHADEMA hawajasema hawatambui matokeo ya urais BALI WANAOPINGA/HAWAKUBALIANI na mchakato uliomuweka RAIS madarakani... ndo maana wanakubali ipo serikali..... walipigakura katika uchaguzi wa PM na Spika na wanaitambua serikali LAKINI SIO MCHAKATO ULIOMUWEKA MKUU WA SERIKALI (rais).
CDM hawana haja ya kuogopa kama wanataka kusimamia mitazamo yao; hakuna sababu ya kusema hampingi uwepo wa Rais aliyewekwa kwa mchakato mnaoupinga?!?!?!?!?!
 
Kwa kuwa katiba inaandaliwa na wananchi, ni lazima CHADEMA na taasisi nyingine zote zinazopigania demokrasia, kabla ya kukutana na serikali wafanye kazi kubwa ya kuwaelimisha wananchi juu ya 'kwa nini inahitajika katiba mpya'. Hii itasaidia sana wakati wa majadiliano na serikali kuwa na uhakika wa kila kitu kutendeka kama inavyotakiwa na kwa muda unaotakiwa. Serikali ya CCM kila mara haiendeshwi wala kufanya mambo kwa dhamira njema bali kwa hila. Mazungumzo yakianza sasa itakuwa ndiyo njia ya kuzima nguvu na speed ya mjadala wenyewe.

Tunachotaka ni wananchi kwa kupitia vyombo mbalimbali kuamua kuwa, 'tunataka katiba mpya', na kisha kuiagiza serikali ije na mpango wa utekelezaji.
 
Kama hakuna mgogoro kwanini waseme wako tayari kukutana na vyama vya upinzani? Wassira inatakiwa awe wazi na kusema wanataka kukutana na CHADEMA na suala hapa ni mgogoro wa uchaguzi uliopelekea JK kurudi magogoni! Makamba siku zote ni mropokaji na hajawahi kuwa serious na issues muhimu. Katiba mpya ni muhimu na ya lazima serikali iache usani!!
 
CDM hawana haja ya kuogopa kama wanataka kusimamia mitazamo yao; hakuna sababu ya kusema hampingi uwepo wa Rais aliyewekwa kwa mchakato mnaoupinga?!?!?!?!?!

JK amerudi madarakani kwa mchakato mchafu, kwa msingi huu JK sio chaguo la watanzania bali Ni CHAGUO la mchakato mchafu wa NEC! Kwa vile CHADEMA na wapenda demokrasia wanapinga mchakato mchafu, ni wazi pia wanampinga Kikwete na ni haki yao na hakuna cha kuogopa. Kama Kikwete ni makini, mwenye kujali maslahi ya Taifa hii ni fursa ya pekee kwake kuandika historia ya kuruhusu katiba mpya Tanzania!!
 
Hata hivyo, Waziri huyo alisema kama kutatokea matatizo au kutoelewana, serikali ina njia na taratibu zake inazozitumia kukutana na walengwa kutatua hali hiyo na kwamba hatua hizo huwa hazitangazwi kwenye vyombo vya habari.
Wassira na CCM wasitufanye wote wajinga siri gani tena kwenye mazungumzo ya katiba, huu si mwafaka wa Maalim Seif na Karume kuwa ni ya kujificha kama wanafanya unyago tunataka yawe ya wazi, Mwafaka wa Karume na Seif ulijengwa kwenye misingi ya uroho wa madaraka, sidhani kama madai ya Chadema ni cheo bali ni katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
 
Kutengeneza katiba mpya ni gharama na inachukua muda sio chini ya miaka 10, kwa hiyo msijidanganye kuwa 2015 tutakuwa na katiba mpya. Suala la katiba mpya halikuwa kwenye ilani ya CCM , na wao hawafanyi mambo kwa shinikizo za watu wasio itakia mema nchi hii

kweli ujinga ni mzigo. hapo kwenye red hebu nijibu zile pesa za EPA na walizokuwa wanalipwa Richmonduri kila siku sh 152,000,000, gharama ni ipi hapo? na hizo bilioni 187 za kuwalipa kina Rost tamu lahazizi zinztoka wapi?
 
Uundaji wa Katiba mpya hauhitaji pesa nyingi wala mijdala ya siri. Kauli za viongozi wa CCM zimekaa kisanii tu lkn hazijadhamiria kuleta mabadiliko ya kweli.
 
Nilidhani cdm wana mawzo mbadala,kumbe ni yaleyale ya kutegemea wahisani! Hawana hisani yoyote ni ukoloni tu
Na yote haya ni tumbo ndilo linalosumbua.Njaa mbaya,we acha tu!
 
Kwanza kabla ya mazungumzo pawepo msingi wa majadiliano, yaani 'guidelines'

Bila msingi imara itakuwa danadana kama ilipofanyika kwa CUF mwaka 2000 - 2005.

Hivyo Msingi wa Kwanza Tume ya Uchaguzi Ivunjwe au Jaji Makame na Kiravu waresign kwanza.

Na mengine wana JF mchangie
 
Back
Top Bottom