Serikali ipambane Gharama za Bima ya kuisafirisha mizigo zilipwe kwa kampuni za Tanzania kuongeza pesa za Kigeni

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
4,958
12,556
Katika biashara ya kuagiza na kusafirisha mizigo nje ya nchi kuna gharama za bima ya mzigo (Insurance). Kwenye terms za kimataifa za usafirishaji kipengele cha CIF (Cost Insurance and Freight). Mnunuzi au muuzaji hukubali kulipa bima ili mzigo usafiri salama na kukingwa na majanga yoyote safarini.

Tanzania na nchi za Africa Mashariki ni waagizaji wa bidhaa mbalimbali kutoka pande tofauti duniani na tumekuwa tukilipa Insurance kwa mizigo mingi tunayoagiza kwa kampuni za nje.

Kama gharama hizi zikilipiwa kwa kampuni za ndani itasaidia kuongeza pesa ya kigeni.

Wiki iliyopita nimeona ISCOS (Intergovernmental Standing Committee On Shipping) wakitangaza kupitia ITV kuhamasisha kutumia kampuni za ndani kulipa Freight Insurance.

ISCOS ni chombo chenye wanachama wa mataifa 5 ambayo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Malawi na DRC. Moja ya kazi yake ni kuishauri serikali kuhusu masuala ya usafirishaji wa njia ya maji na kupanga sera za usafirishaji baharini.

Tangazo lao lilikuwa limepoa. Je, ISCOS imeshindwa kuishauri serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kuwezesha hiyo sera yao, kipindi hiki ambacho nchi ina uhaba wa pesa za Kigeni?
 
Back
Top Bottom