ubarinolutu
JF-Expert Member
- Oct 22, 2012
- 1,973
- 3,906
Biteko anawaambia TANESCO kuwa wananchi wanataka umeme, wananchi hawataki kusikia sijui kuna mipango na porojo gani kama alivyokuwa anasema Makamba, lakini hata akiwaambia wananchi wanataka umeme huo umeme utatoka wapi? Kwanini wananchi tusiwapime CCM kwa kutumia umeme?
Jinsi na kadiri siku zinavyoenda tatizo la upatikanaji umeme linazidi kwasababu;
1. Mahitaji ya umeme kwa wananchi yameongezeka kwasababu ya kujua kiuchumi, mahitaji ambayo uzalishaji uliopo umefeli. Ndio maana toka Makamba ameingi mpaka leo Biteko yupo mgao wa umeme upo kila siku.
2. TPDC wana uhaba mkubwa wa gesi, hivyo kupelekea baadhi ya mitambo ya gesi mara kwa mara kuwa nje, ila TPDS wamejaa kimya ili hali wanajua kuna uhaba na upungufu wa gesi, na uwezo wa kutatua tatizo hawana mpaka wazungu waingilie kati.
3. Maji ni shida kwenye mabwawa, uzalishaji wa mabwawa hautoshelezi, na nashangaa kwanini mama amemtoa Kalemani, kamtoa Makamba, kaja Biteko lakini kwa tatizo hili ya umeme nchi hii halitakuwa rahisi kwake.
4. Makamba kasaini mikataba ya trilioni 1.9 kuimarisha upatikanaji wa umeme ambao haupo, pamoja na fedha nyingi kutolewa matatizo ya umeme bado ni makubwa, umeme unakatika katika, kwasababu ya ubovu wa miundombinu na uzalishaji usiojitosheleza.
Lengo la uzi huu ni kuiomba Serikali Sasa ifikirie njia rahisi ya kutatua tatizo la umeme Kwa kununua umeme kutoka Ethiopia kupitia Kenya, kwani Ethiopia wana umeme mwingi wa bwawa la grand.
Kwakuwa upungufu wa Dolla utasababisha Stiglers kuchelewa kukamilika basi tufanye mpango tununue umeme Ethiopia. Japo serikali imeishiwa fedha za kumaliza mradi wa njia kubwa kilo volt 400 kutoka namanga kwenda Arusha, Babati, basi ikakope na tuhakikishe tunajenga miundombinu ya kununua umeme Ethiopia, hizi shida za mgao hazivumiliki.