Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 32,479
- 34,319
Unazungumzia Dodoma na Dar lakini wapo watumishi wengine wengi zaidi ya hao katoka mikoa na maeneo mengineMimi ni mfanyakazi wa Serikali na ni mtumishi wa muda mrefu nimebakiza miaka mitatu kustaafu. Mkewe wangu nae ni mfanyakazi wa Serikali ila yeye alibaki Dar. Tumetenganishwa kwa nguvu na hili la Dodoma. Tumebahatika kupata watoto.
Baadhi ya watoto wetu wako kwenye ndoa na wengine wako vyuoni nasi. Mke wangu bado ana miaka 13 kazini kabla ya kustaafu. Majuzi amenitembelea hapa Dodoma, alifika akiwa anajisikia vibaya na tukafanya utaratibu wa kwenda hospital. Tulikutana na Dr mstaarabu na akatushauri tupime Ukimwi kwa pamoja.