Serikali inakosea sana kuwatenganisha Kikazi Wanandoa

Mimi ni mfanyakazi wa Serikali na ni mtumishi wa muda mrefu nimebakiza miaka mitatu kustaafu. Mkewe wangu nae ni mfanyakazi wa Serikali ila yeye alibaki Dar. Tumetenganishwa kwa nguvu na hili la Dodoma. Tumebahatika kupata watoto.
a nawatupia Serikali kwa kukatisha ndoa yangu na pengine itakatisha maisha ya mke wangu aliyeondoka kwa kuchanganyikiwa. Hili la Dodoma linaonekana kama masihara lakini ni janga kubwa sana. Tumejichimbia kaburi kimzaha.
Duh pole sana maisha lazima yaendelee ila kama ni msaliti hapo hekima zako na maamuzi yako ndio yataamua.. maana nyie ni watu wazima teyari.
 
Mimi ni mfanyakazi wa Serikali na ni mtumishi wa muda mrefu nimebakiza miaka mitatu kustaafu. Mkewe wangu nae ni mfanyakazi wa Serikali ila yeye alibaki Dar. Tumetenganishwa kwa nguvu na hili la Dodoma. Tumebahatika kupata watoto.
Pole sana mkuu.

Ila ulioa mke mwenye tofauti kubwa sana ya kiumri.

Yeye bado damu ya moto kuliko wewe hata kama ng'ombe hazeeki maini.

Hapo Gavo utailamu bure tu(tungepata takwimu za ndoa zilizotenganishwa na Gavo na zikaingiwa na msala kama wako, ndipo tungeweza kuhitimisha) mlaumu mkeo kwa kupiga mbizi ovyo ovyo tena bila kuwa na maboya.
 
Sijajua naweza kumuacha au yeye kuondoka mwenyewe (isije ikawa ndo mwenyewe unataka kujua status)
Kuna wazee mnazeeka halafu life skills ndogo. Kwa namna wewe ulivyopanic huyu mama hawezi kuwa salama kimawazo. Hivi mwanaume umewezaje kumwacha mkeo kwenye matatizo afunge safari arudi Dar?

Usichojua ni kwamba kwa wakati huu huyo yupo kwenye Denial, hakubaliani na kilichompata, anaomba angalau Mungu angetoa nafasi ya upendeleo kwake atubu. Sasa kumpa pressure ktk wakati huu umemfanya ajihisi mkosaji mkubwa kuliko wote Duniani.

Nakushauri japo umeamua ndoa itavunjika lakini isiwe mapema hivyo mwache mpaka afikie hatua ya kujikubali na Kisha mtaamua ulitakalo. Kingine nenda hospital mfundishwe njia sahihi ya kushiriki tendo la ndoa pasipo kuambukizwa ili angalau msubiriane mpaka mmoja atangulie ndio uwe mwisho mwenu.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Kushiriki tendo la ndoa?....
 
Yaani serikali isitekeleze sera zake kwa kuhofia kuwa ndoa zitavunjika?
Nchi za wengine, ndoa ni kitu Cha muhimu sana kuliko hata sera na kazi. Ndo inahusu hasa jamii hiyo hiyo unayoitungia sera. Wakati wa Mwalimu walijali sana ndoa. Je hawa watoto wanaolelewa bila wazazi wao umewawekea sera gani. Naona kama hatutazingatia ndoa sioni mbele iliyonjema
 
Kachepuka labda angekuwa nesi kaupata kwa bahat mbaya yani apo tu dom anashindwa kuja kukupa mbususu anaenda kuwap watu wa ovyo tena bila kujijali, uyo mzee we mpe pole wala usimwambie kama umemwacha ila mkatae kisailensa mpaka ajiongeze mwenyewe

Kiatu chako kikubwa kivae mwenyewe ila mkeo kakukosea sana usilaumu sirikali dom to dar si mbali
 
Aje
Nakiri suala lako linaumiza sana, pole sana.

Lakini Mkuu, kwanini kabla ya kuilaumu serikali usiangalie kwanza nyie wenyewe mliteleza wapi kama wanandoa?
Njia za maambukizi zipo nyingi lakini kwakuwa hii ni ndoa tuongelee uzinifu/uchepukaji.

Kwanini usimpe lawama mkeo kwa kushindwa kuwa kuwa mwaminifu mpaka kufikia kulikwaa gonjwa?

Mlijiwekea utaratibu gani wa kukutana kutokana na umbali huo ulioletwa na mabadiliko hayo serikalini?

Kabla ya kuitupia lawama serikali angalieni nyie mmeteleza wapi kwanza kama wanandoa.
Ila poleni na Mungu awape hekima ya kukabiliana na hili.
Apa ajibu intaviuu
 
Hilo ni jambo la kawaida, ukimwi siku hizi sio ugonjwa mzee wangu, ogopa kansa, pressure, nk! Wewe unaogopa jamii na wattoto wenu, mtaenda kuwatangazia?? Kuna watu wanashida nyingi kuliko hata zako wamekaa nazo kimya na maisha yanaenda, hivyo tuliza akili na chukulia ukimwi na ugonjwa mwingine na mtakula bata mpaka miaka 100 mzee wangu!! Ndo maana ya kiapo cha ndoa kwenye shida na raha! Mtie moyo mkeo , wewe kwa sasa ndo faraja yake! Sio wewe tena mwanaume kuanza kupaparika, simama kiume mzee!! Ukihitaji msaada zaidi njoo pm
Umeongea kikubwa sana nimewahi kuona documentary Moja nadhani uingereza mzungu mmoja alikuwa na maambukizi ya HIV Kisha mwandishi akamuuliza unajisikiaje
Akasema angalau sio Kansa maana hiyo ndio inatisha
 
Mimi ni mfanyakazi wa Serikali na ni mtumishi wa muda mrefu nimebakiza miaka mitatu kustaafu. Mkewe wangu nae ni mfanyakazi wa Serikali ila yeye alibaki Dar. Tumetenganishwa kwa nguvu na hili la Dodoma. Tumebahatika kupata watoto.

Baadhi ya watoto wetu wako kwenye ndoa na wengine wako vyuoni nasi. Mke wangu bado ana miaka 13 kazini kabla ya kustaafu. Majuzi amenitembelea hapa Dodoma, alifika akiwa anajisikia vibaya na tukafanya utaratibu wa kwenda hospital. Tulikutana na Dr mstaarabu na akatushauri tupime Ukimwi kwa pamoja.

Majibu yalitoka na mke wangu akiwa Chanya + tulipima tena hospital nyingine na bado ilibaki vilevile. Sasa nabaki najiuliza, jamii itatuelewaje? Watoto watatuelewaje? Wakwe watatuelewaje? Nimekata tamaa na nimebaki bila majibu.

Jamani wenzangu mkae mkijua kuwa hili limetokea kwangu, ukweli wenyewe wengi mko kwenye maisha hayo. Serikali imefanya makosa makubwa sana kutenganisha ndoa za watu kwa makusudi. Watoto wengi walioko mitaani hawana maadili kwa kukosa malezi ya baba na mama.

Hapa tunajenga taifa au tunabomoa. Nimebaki njia panda. Nimfukuze? Nimuue? Au nifanyeje. Huu ni utumishi Serikalini au ni utumwa serikalini. Nimeshindwa kula hata kazini sijaenda. Mke wangu karudi Dar nae sijui anaenda kujiua!

Mbali na lawama kwa mke wangu bado zigo la lawama nawatupia Serikali kwa kukatisha ndoa yangu na pengine itakatisha maisha ya mke wangu aliyeondoka kwa kuchanganyikiwa. Hili la Dodoma linaonekana kama masihara lakini ni janga kubwa sana. Tumejichimbia kaburi kimzaha.
Pole sana,lakini kama wote ni watumishi si ungehama nae mkuu!!!
 
Sera ya Serikali kutojali ustawi wa familia ni janga kubwa sana.

Wafanyakazi ni kama hawastahili kuishi kwenye ndoa.
 
Back
Top Bottom