Sakata la Jerry Silaa kuvunja majumba ya watu nchi nzima: Johnson Mahululu aidai serikali ya Tanzania bilioni 20

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,003
20,681
Source: Youtube-wakiliTv, taarifa ya Wakili Dickson Matata

Nilisema kwamba haya mambo ya kujifanya mwendesha mashitaka na hakimu anayofanya Jerry Silaa yasipoangaliwa, ataitia nchi hasara kubwa sana.

Sasa watanzania wataingia hasara ya bilioni 20 ili kumlipa Johnson Mahululu baada ya Jerry Silaa kuvunja ghorofa lake, kumdhalilisha kumuita tapeli wakati hana hukumu ya mahakama iliyompata na hatia ya utapeli, na kumharibia jina na biashara zake.

Niliwahi kuonya humu kwamba wizara kubwa na nzito wasipewe watoto, hawa watoto waanzie wizara ya michezo, utamaduni na kwingine.

Nimefuatilia kule Mwanza, anatangatanga na Polisi kwemye mikutano, na wale ambao hawajaelewa maelezo yake, anatoa amri wakamatwe na Polisi. Kimsingi, analeta chaos kubwa sana.

Ameenda kuonana na RPC na kutoa amri (udikteta ambao samia hataki) kwamba Johnson Mahululu anyimwe dhamana, ana siku tano hajatoka.

Tunajua weekend iliyoisha ilibidi awahi kikao mahali akutane na bosi wake mkubwa., tunaipa angalizo serikali dhidi ya Jerry Silaa.

Kuhusu nyumba kuvunjwa, soma Aliyevamia Kiwanja cha mwingine kwa miaka 20 Mbezi Africana avunjiwa ghorofa

Pia soma Serikali impe angalizo Jerry Silaa, namuona anaiingiza Serikali katika mgogoro mkubwa wa kulipa fidia!
 
Ina semekana Johnson yuko selo ya polisi ostabey leo siku ya tano bila dhamana wala mawakili na ndugu zake kuruhusiwa kumuona.
Pia kuna tetesi za kumfungulia kesi ya uhujumu uchumi.
Jerry Silaa anashinikiza ifunguliwe kesi ya criminal trespass wakati msimamo wa Mahakama za Tanzania ni kwamba hiyo ni civil case, kama kuna dispute ya umiliki ni lazima kwanza mahakama ya madai ithibitishe nani mmiliki ndipo ujue nani kafanya criminal trespass.

Pengine Mwendesha Mashtaka wa Mkoa kawagomea kupeleka jalada Mahakamani kwa sababu hiyo

Anajua hiyo bili ya bilioni 20 lazima aitolee maelezo Baraza la Mawaziri, au kabla,kwa Waziri Mkuu
 
Nilisema kwamba haya mambo ya kujifanya mwendesha mashitaka na hakimu anayofanya Jerry Silaa yasipoangaliwa, ataitia nchi hasara kubwa sana.

Sasa watanzania wataongia hasara ya bilioni 20 ili kumlipa Johnson Mahululu baada ya Jerry Silaa kuvunja ghorofa lake, kumdhalilisha na kumharibia biashara zake.

Niliwahi kuonya humu kwamba wizara kubwa na nzito wasipewe watoto, hawa watoto waanzie wizara ya michezo, utamaduni na kwingine.

Nimefuatilia kule Mwanza, anatangatanga na Polisi kwemye mikutano, na wale ambao hawajaelewa maelezo yake, anatoa amri wakamatwe na Polisi. Kimsingi, analeta chaos kubwa sana.

Ameenda kuonana na RPC na kutoa amri (udikteta ambao samia hataki) kwamba Johnson Mahululu anyimwe dhamana, ana siku tano hajatoka.

Tunajua weekend iliyoisha ilibidi awahi kikao mahali akutane na bosi wake mkubwa., tunaipa angalizo serikali dhidi ya Jerry Silaa
Umejikanyaga Kanyaga na hujatueleza Jerry Slaa amekosea wapi na huyo Mahululu anavyo vielelezo gani hadi wewe utowe hukumu dhidi ya Waziri Jerry Slaa?

Umejithibitusha kwamba kila anaefungua madai dhidi ya serikali ni lazima ashinde?
Au kwa sababu ya land grabers kuwa na Cartel inayowashirikisha watu wa kwenye mfumo wao?

Huko Mwanza woote tumeiona ile Clip ambayo mama yule Maskini alirudishiwa viwanja vyake viwili baada ya kushinda kesi hadi mahakama ya rufaa Tanzania.
Wale matapeli walikuwa wanamzingua na rundo la makaratasi.
Aliwauliza mara kadhaa tena mbele ya ma Afisa ardhi kama nyaraka walizo nazo na za yule mama kama sio zilizotumika mahakamani?
Wakajibu ndio hizo!
Akawauliza tena...
Kesi hii si ndio imetoka mahakamani kwenye mahakama kuu ya rufaa wakajibu ndio!
Sasa kama walitaka avunje sheria kwa jambo ambalo tayari limeamriwa na mahakama ya rufaa mara mbili.....

Wewe mleta mada ni sehemu ya matapeli wa ardhi nchi hii.
Mpuuzi unayejifanya kujua kumbe hujui.
Nchi hii wafuatiliaji sio wewe au genge fulani pekee.tuko wengi na tunaona haki zikiporwa na majizi ya sampuli yako.
Acha kuwa mjuaji saaana!
 
Yawezekana ni mbinu ya kuchota hela za serikali iliyoandaliwa vema na vigogo wa serikali kwa kuwatumia Johnson Mahululu na waziri Slaa.

Ghorofa libomolewe, Mahululu aende mahakamani halafu adai fidia ya mabilioni. Serikali ilipe hayo mabilioni kisha Mahululu apozwe kwa bilioni 2 au 4.

Script hii ya kuchota hela za serikali imeandaliwa kwa ustadi mkubwa sana. Mpk uwe umesoma Cuba ndiyo utaielewa.
 
Yawezekana ni mbinu ya kuchota hela za serikali iliyoandaliwa vema kwa kumtumia Johnson Mahululu.

Ghorofa libomolewe, Mahululu aende mahakamani halafu adai fidia ya mabilioni. Serikali ilipe hayo mabilioni kisha Mahululu apozwe kwa bilioni 2 au 4.

Script hii ya kuchota hela za serikali imeandaliwa kwa ustadi mkubwa sana.
Ninadhani maelezo yako yana ulweli zaidi maana nchi hii huo mdio mfumo wanaoutumia hawa "state capture" wa msoga.
Naikumbuka ile skendo ya mzee Bilionea wa Arusha "Verani"
Kikwete alimtumia akachota mabilioni na analipwa mpaka wa leo.
 
Umejikanyaga Kanyaga na hujatueleza Jerry Slaa amekosea wapi na huyo Mahululu anavyo vielelezo gani hadi wewe utowe hukumu dhidi ya Waziri Jerry Slaa?

Umejithibitusha kwamba kila anaefungua madai dhidi ya serikali ni lazima ashinde?
Au kwa sababu ya land grabers kuwa na Cartel inayowashirikisha watu wa kwenye mfumo wao?

Huko Mwanza woote tumeiona ile Clip ambayo mama yule Maskini alirudishiwa viwanja vyake viwili baada ya kushinda kesi hadi mahakama ya rufaa Tanzania.
Wale matapeli walikuwa wanamzingua na rundo la makaratasi.
Aliwauliza mara kadhaa tena mbele ya ma Afisa ardhi kama nyaraka walizo nazo na za yule mama kama sio zilizotumika mahakamani?
Wakajibu ndio hizo!
Akawauliza tena...
Kesi hii si ndio imetoka mahakamani kwenye mahakama kuu ya rufaa wakajibu ndio!
Sasa kama walitaka avunje sheria kwa jambo ambalo tayari limeamriwa na mahakama ya rufaa mara mbili.....

Wewe mleta mada ni sehemu ya matapeli wa ardhi nchi hii.
Mpuuzi unayejifanya kujua kumbe hujui.
Nchi hii wafuatiliaji sio wewe au genge fulani pekee.tuko wengi na tunaona haki zikiporwa na majizi ya sampuli yako.
Acha kuwa mjuaji saaana!
Sheria ina utaratibu, kama kashinda mahakamani, aliyeshinda aende mahakamani akabidhiwe alichoshinda, na kama walioshindwa wamesharau mahakama, sheria ina maelekezo, unamkamata wewe Waziri ili iweje?
 
Jerry Silaa anashinikiza ifunguliwe kesi ya criminal trespass wakati msimamo wa Mahakama za Tanzania ni kwamba hiyo ni civil case, kama kuna dispute ya umiliki ni lazima kwanza mahakama ya madai ithibitishe nani mmiliki ndipo ujue nani kafanya criminal trespass.

Pengine Mwendesha Mashtaka wa Mkoa kawagomea kupeleka jalada Mahakamani kwa sababu hiyo

Anajua hiyo bili ya bilioni 20 lazima aitolee maelezo Baraza la Mawaziri, au kabla,kwa Waziri Mkuu
Siyo lazima.
 
Yawezekana ni mbinu ya kuchota hela za serikali iliyoandaliwa vema na kigogo wa serikali kwa kuwatumia Johnson Mahululu waziri Slaa.

Ghorofa libomolewe, Mahululu aende mahakamani halafu adai fidia ya mabilioni. Serikali ilipe hayo mabilioni kisha Mahululu apozwe kwa bilioni 2 au 4.

Script hii ya kuchota hela za serikali imeandaliwa kwa ustadi mkubwa sana. Mpk uwe umesoma Cuba ndiyo utaielewa.
Naomba nielimishwe, fedha za fidia za namna hii utolewa fungu gani ndani ya Wizara husika? Je zinakuwa allocated ndani ya bajeti ya Mwaka wa Fedha husika?
 
Kwa Nini asingeongeza nguvu kwenye issue za kupanga miji yenye wakazi wengi kama Dar es salaam na kuondoa makazi holela kuliko nguvu hizi anazotumia!? Kamalizana na Petro station Sasa karudi Huku Tena!?
 
Nilisema kwamba haya mambo ya kujifanya mwendesha mashitaka na hakimu anayofanya Jerry Silaa yasipoangaliwa, ataitia nchi hasara kubwa sana.

Sasa watanzania wataingia hasara ya bilioni 20 ili kumlipa Johnson Mahululu baada ya Jerry Silaa kuvunja ghorofa lake, kumdhalilisha kumuita tapeli wakati hana hukumu ya mahakama iliyompata na hatia ya utapeli, na kumharibia jina na biashara zake.

Niliwahi kuonya humu kwamba wizara kubwa na nzito wasipewe watoto, hawa watoto waanzie wizara ya michezo, utamaduni na kwingine.

Nimefuatilia kule Mwanza, anatangatanga na Polisi kwemye mikutano, na wale ambao hawajaelewa maelezo yake, anatoa amri wakamatwe na Polisi. Kimsingi, analeta chaos kubwa sana.

Ameenda kuonana na RPC na kutoa amri (udikteta ambao samia hataki) kwamba Johnson Mahululu anyimwe dhamana, ana siku tano hajatoka.

Tunajua weekend iliyoisha ilibidi awahi kikao mahali akutane na bosi wake mkubwa., tunaipa angalizo serikali dhidi ya Jerry Silaa
Huyo Jery Silaa Hana chochote anachojali, maana serekali hii haijali Sheria. Unapokuta serekali Iko juu ya Sheria usitegemee hata mtu akishinda kesi atalipwa. Isitoshe Silaa hata huyo mtu akilipwa yeye hasikii maumivu ya deni maana fedha ni za mabwege, yeye hapotezi chochote.
 
Back
Top Bottom