Serikali IMEWEZA... Serikali IMESHINDWA...

Eng. Y. Bihagaze

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
1,488
908
Wadau Wa Jukwaa makini tuache viuvivu Jumamosi hii, tuchangamkie topic hii ya Kiswahili kutunga sentensi kutumia maneno SERIKALI IMEWEZA.. SERIKALI IMESHINDWA ..wacha mkufunzi nianze

1. Serikali IMEWEZA kuwafukuza watanzania wafanya biashara zaidi ya 800 eneo la Ubungo lakini Serikali IMESHINDWA kumwondoa mfanya biashara mmoja Wa kiasia aliyejenga kiholela fukweni mwa Bahari.

2. Serikali IMEWEZA kupiga marufuku mikutano yoote ama ya kisiasa au kijamii Tanzania yote wakati Wa zoezi la sensa ya Makazi Lakini Serikali IMESHINDWA kupiga marufuku mkutano Wa kisiasa wa CCM kwenye kitongoji kidogo sana Cha BUBUBU

3. serikali IMESHINDWA kuwakamata waliomsulubu Ulimboka, walioua Iringa (mwagosi), Morogoro (Ally Hassan Singano (Zona), waliochinja Arumeru (Mwenyekiti wa Chadema, Kata ya Usa River, wilayani Arumeru, Mkoa wa Arusha, Msafiri Mbwambo), walioua Igunga ( Mbwana Masoud Mbwana) Na mengineyo lakini Serikali IMEWEZA
Kuwatia nguvuni wote waliokomba vijidude vyote vya Naibu Waziri wa Nishati na Madini Adamu Kighoma Malima vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 15 katika hoteli ya kitalii ya Nashera ya mjini Morogoro.

Ukiuliza unaambiwa nchi ipo na serikali Ipo, Na watu wapo wamepiga kimya tu, maisha yanasonga..

ENDELEA..
 
Serikali IMEWEZA kukamata wezi na mateja lakini IMESHINDWA kuwakamata Mafisadi wa EPA and the like kwa kisingizio kwamba uchumi utayumba.
 
Serikali ya CCM imeweza kupeleka mafisadi nje ya nchi kutibiwa kwa mamilioni ya fedha lakini imeshindwa kuboresha huduma katika hospitali zetu hata panadol hazipo.

Serikali ya CCM imeweza kuongeza masilahi wa wabunge mpaka mil10 lakini imeshindwa kuwaongezea madaktari/walimu nyongeza ndogo wanayodai kwenye mishahara yao.
 
Serikali IMEJITAHIDI Na KUWEZA kuwatia nguvuni majangili yoote yaliyomuua Faru mmoja aliyejulikana Kwa jina la George, lakini maskini serikali hii hii IMESHINDWA kabisa kumtia nguvuni hata kiumbe mmoja anayeendesha mazoezi ya kuwaua Watanzania wenzetu Albino, zaidi ya 85 Sasa ..
 
Serikali imepigia Biti nzito Kwa wale wanaonyemelea uongozi Kwa njia Za hongo lakini imeshindwa kuwawajibisha watafuna hongo inaowafaham Kwa majina..
 
Back
Top Bottom