Serikali imeingia kwenye mtego wa kina Dkt. Slaa mazima, wametimiza lengo la kufungua maandano yao!

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Salam wa nyuki wa mama na team kupinga ubadhirifu, unyanyasaji na mikataba yenye kuleta hasara kwa nchi.

Akina Slaa na Mwabukusi safari hii wamecheza kama pele, wametumia mtandao vizuri kucheza na akili za viongozi wa serikali na wamefanikiwa kwenye hilo. Sasa mapambano yanafanywa 'kisayansi' kama wenyewe wanavyosema. Wamevaa matisheti meupe yenye ujumbe wanaendelea na mambo yao bila wasiwasi.

Polisi wamefika kwenye maeneo toka usiku kusubiri waandamanaji, kumbe wao ndio wanaandamaji wenyewe waliokwenda kufanya ufunguzi wa maandamano hayo.

Wamekuwa wa kwanza kuonesha chuki dhidi ya mkataba wa bandari, na hitaji la kupatikana kwa katiba mpya.

Ila serikali mnatia aibu, ninyi kitu wakifanya upinzani tu mnareact tu kama wajinga bila kuangalia picha kubwa, halafu watafanya hayo hayo CCM mnaacha vifanyike, si hata mtoto anaweza kupanga mambo vizuri kuliko hivi mnavyotekeleza mikakati. Mambo ya kijinga kabisa.

Halafu kila kukicha mnatuambia serikali inahakikisha uhuru wa kujieleza, kutoa maoni, huku mnazuia raia kutekeleza haki zao kwa amani? Maandamano ni haki ya kikatiba, na kazi yenu polisi ni kuhakikisha ulinzi wa kila anayeshiriki sio kuwatisha wasishiriki.
 
Naona umeamua kujifarijo na kujiliwaza kutokana na msongo wa mawazo vipi maandamano leo nasikia kulikuwa na watu wanne tu Mdude mwenye kajificha.
😂😂😂 wapi nimesema nilitaka kwenda kuandamana? Huo ni mpango wao, je umefanikiwa au la?
 
Dr Slaa akiwa kwenye maandamano leo.
 
Attachments

  • IMG_5992.jpeg
    IMG_5992.jpeg
    99.6 KB · Views: 4
Salam wa nyuki wa mama na team kupinga ubadhirifu, unyanyasaji na mikataba yenye kuleta hasara kwa nchi.

Akina Slaa na Mwabukusi safari hii wamecheza kama pele, wametumia mtandao vizuri kucheza na akili za viongozi wa serikali na wamefanikiwa kwenye hilo. Sasa mapambano yanafanywa 'kisayansi' kama wenyewe wanavyosema.

Polisi wamefika kwenye maeneo toka usiku kusubiri waandamanaji, kumbe wao ndio wanaandamaji wenyewe waliokwenda kufanya ufunguzi wa maandamano hayo.

Wamekuwa wa kwanza kuonesha chuki dhidi ya mkataba wa bandari, na hitaji la kupatikana kwa katiba mpya.

Ila serikali mnatia aibu, ninyi kitu wakifanya upinzani tu mnareact tu kama wajinga bila kuangalia picha kubwa, halafu watafanya hayo hayo CCM mnaacha vifanyike, si hata mtoto anaweza kupanga mambo vizuri kuliko hivi mnavyotekeleza mikakati. Mambo ya kijinga kabisa.

Halafu kila kukicha mnatuambia serikali inahakikisha uhuru wa kujieleza, kutoa maoni, huku mnazuia raia kutekeleza haki zao kwa amani? Maandamano ni haki ya kikatiba, na kazi yenu polisi ni kuhakikisha ulinzi wa kila anayeshiriki sio kuwatisha wasishiriki.
Serikali imeoza asee
 
Back
Top Bottom