Serikali imefuta pia adhabu ya 10% inayotozwa na Bodi ya Mikopo kwa wanaochelewa kulipa deni

Waziri wa Elimu Prof.Joyce Ndalichako leo Bungeni tarehe 4 Mei 2021. Ameiagiza Bodi ya mikopo elimu ya juu kuondoa adhabu ya asilimia 10 ya mkopo inayotozwa na kwa wanafaika wa mikopo elimu ya juu wanaochelewa kulipa mikopo hiyo baada ya miaka miwili kupita tangu kuhitimu kwao chuo.

Kwaniaba ya Ngome ya vijana Act Wazalendo, napenda kuishukuru na kuipongeza serikali kwa maamuzi haya makubwa na ya kupongezwa.

Ngome ya vijana Act Wazalendo tumekuwa mstari wa mbele haswa kusemea changamoto zote kuhusu urejeshaji wa mikopo elimu ya juu.

Mbali na kusemea tozo ya ongezeko wa thamani ya fedha (Value Retention fee 6%) mbayo tayari imefutwa na Mh.Rais Samia.Pia tumekuwa tukishauri na kutaka kufutwa kwa penalti ya 10% inayotozwa mara moja na Bodi ya mikopo kwa wanufaika ambao wamechelewa kulipa mikopo yao miaka 2 tangu kuhitimu kwao.

Tarehe 20/Januari /2021 tuliandikia barua wizara ya elimu yenye kumb Na:ACT/HQ/Vijana/001, nakala tukapeleka Ofisi ya Rais Ikulu,Ofisi ya waziri mkuu na Bodi ya mikopo. Iliyoandikwa na katibu wa Ngome wetu Mwanaisha Mndeme yenye kichwa cha habari SERIKALI KUFANYA MAREJEO NA TATHIMINI MPYA JUU YA VIWANGO NA MASHARTI YA MAREJESHO YA MIKOPO ELIMU YA JUU.

1. Tukishauri na kupendekeza kufutwa kwa Value Retention fee 6% ambayo tayari imefutwa na Mh.Rais.

2. Tukishauri kufutwa kwa Penalti /Adhabu ya 10% ,na hili pia tulilisisitiza juzi tarehe 2 /Mei /2021 katika mkutano wetu wa vyombo vya habari ,Leo hii tar 4 Mei Waziri wa Elimu ametoa maagizo nayo hii Penalti/Adhabu ya 10% ifutwe .

3. Tukishauri Makato ya 15% yarudi 8% au chini ya 8% . Bado halijafanyiwa kazi tunaendelea kuishauri serikali nayo hii ishushwe.

4. Tukishauri kufutwa kwa tozo ya 1% ya kugharamikia shughuli za Bodi (Loan Administration fee).Bado halijafanyiwa kazi tunaendelea kuishauri serikali nayo iondolewe.

Ngome ya vijana Act wazalendo tunaendelea kuishukuru na kuipongeza serikali kwa maamuzi haya,lakini pia tunapongeza jitihada za wabunge wote waliolisemea hili pia Mh.Khatibu Said Khaji wa act wazalendo ,Mh.Ester Matiko na wengine wote,bila kusahau wanaharakati pia ,Azaki , waandishi wa habari na wengine wote.

Ngome ya vijana Act wazalendo tutaendelea kusemea na kupigania maslahi ya vijana na makundi yote nchini bila kuchoka.

Imetolewa na,

Abdul Nondo.

Mwenyekiti wa Ngome ya vijana Act wazalendo Taifa

Tarehe 4,Mei,2021.

View attachment 1772955
hongereni sana Abdul. Nyie hangaikeni na shida za watu/watanzania. msiwe kama wale jamaa wengine ambao wao kazi yao ni matamko tu na matusi humu mitandaoni.
 
Back
Top Bottom