Serikali imefilisika hakuna pesa!

fedha zipo tena nyingi tu,isipokuwa priorities ndio tatizo kubwa yamsingi hayafanywi yasiyo ya msingi yanatumia pesa nyingi sana.
kuna maadhimisho ya muungano yanakuja je ni kiasi gani kimepangwa kutumika hapo je kiasi hicho na yote yatakayofanywa na namna yatakavyofanywa ni muhimu kiasi gani?
maadhimisho ya miaka hamsini ya uhuru wa nchi yetu yalitumia kiasi gani je yote yaliyofanyika yalikuwa yamsingi kuliko makaratasi na mipango mingine ya maendeleo nchini?
pesa zilizotumika kutoka serikalini katika msiba wa kanumba zilikuwa ni muhimu kiasi gani ukilinganisha na matatizo chungu nzima ya watanzania?
shida si pesa bali matumizi ya pesa hizo serikali haina pesa??????
nakataaaaaa kabisa
 
Hakuna ubishi kabisa kwamba serikali hii ya kisanii na badhirifu haina kabisa hela kwani imeshindwa kuheshimu commitments zake nyingi tu ikiwa ni pamoja na malipo ya pensheni ya wazee wastaafu ambao mara ya mwisho walilipwa January mwaka huu na kwa kadiri ya tangazo lao la awali walipaswa kulipwa baada ya miezi mitatu yaani mwanzoni mwa Aprili hii. Sasa ni zaidi ya nusu mwezi na malipo yameshindikana, serikali imeshindwa hata kuwasiliana nao na haijaeleweka kama mwezi ujao watalipwa au la! La ajabu wanaendelea na ubadhirifu hata wa kidogo kilichobaki. Tanzania ni nchi ya ajabu, serikali inakusanya kodi kwa machinga tu, mapapa yanaachwa na kupewa misamaha isiyo na mantiki yoyote, serikali inawahadaa wananchi wake kwamba eti imevunja rekodi kwa kukusanya kodi! Wakati huo huo Rais anabembea kwenye ndege akifanya safari zisizo na tija yoyote kama mbayuwayu.

Nitajie chinga anayelipa kodi.
 
Wakuu,kuna taarifa kuwa walimu wa shule za sekondari walioajiriwa hivi karibuni wameamua kurudi makwao kutokana na halmashauri husika kutokuwa na fungu la kuwalipa mishahara na marupurupu yao mengine. Mfano ni walimu waliopangiwa shule za Chunya mkoani Mbeya.

Hii ni taarifa mbaya sana. Lakini serikali yetu itakuwaje na fedha wakati huko TRA, Bandari, maliasili na kwingineko fedha nyingi zinaishia mikononi mwa wachache? Tanzania tunapiga kelele sana lakini mambo bado yako vile vile! Mungu atusaidie Tanzania.
 
Habari za kiinteligensia ni kuwa wameanza kuwaangukia Business Tycoon kama Bakhresa ili angalau atuokoe na aibu hii ata kwa kulipa mishahara baadhi ya sector
Tutafika
 


TANZANIA ZAIDI YA UIJUAVYO.

Shangaaa wafanyakazi wa Halmashauri hizo wanaishi na kusomesha watoto wao na hakuna hata mmoja alisha goma au kuandamana kudai malipo yao ndio TANZANIA hiiiii jamani,

Wachahche wetu wakidai haki twaaambiwa wanafanya vurugu hizi sera za woga zinatoka wapi tutakuja chanana mapanga humu ndani kila mmoja atakula na adui wake kwa jinsi alivyo muona kama alikuwa upande wa wanyonge au MAFISADISTANI



Tafadhali sana ndugu yangu hiyo para ya kwanza kama ungejua tunavyoishi sisi wafanyakazi wa halmashauri na wengi wao serikali kuu ungeelewa,basi tu tumeshakuwa watu wazima na familia zinatutegemea na ni wavumilivun lkn hali mbaya.suala la kuwapeleka shule watoto wetu wewe ulitegemea pamoja dhiki zetu watoto wasiende shule?tunabana ****** angalia salary slip zetu uone hao akina baypot na wenzao wanavyo kwangua mishahara yetu kwasababu ya mikopo,Nyooo.
 
Bora hata fedha zisipelekwe miradi ya halmashauri. Wanazitafuna tu, inatia kichefuchefu ukiangalia ripoti ya CAG.
 
Viongozi wa serikali inayoongozwa na Ccm, wote kwa pamoja wamechota pesa na kwenda
kuzichimbia kwenye mahandaki majumbani kwao na vijijini kwao, kwa uoga mkubwa
walionao wa kuondoka madarakani. Sisi tunatamka kama serikali imefilisika kwa sababu
wamekwangua akaunti zote za wizara kwenye bank na kuziacha tupu, wao wanaona
bora watanzania wafe lakini " Legal Tender " ziishie kwenye mahandaki.
 
Kuweni wapole. Serikali inachapisha manoti ya kutosha.
Soon zitamwagwa mtaani, kila mtu atajazwa mafweza na ugumu wa maisha utapungua.
 
Wakuu,kuna taarifa kuwa walimu wa shule za sekondari walioajiriwa hivi karibuni wameamua kurudi makwao kutokana na halmashauri husika kutokuwa na fungu la kuwalipa mishahara na marupurupu yao mengine. Mfano ni walimu waliopangiwa shule za Chunya mkoani Mbeya.
hata wilaya ya Kisarawe hali ipo hivyo,walianza na agizo kuwa shule ziwakopeshe na ikawa hivyo ila serikali haikurefund wala hata kuonesha muelekeo so imebidi walimu warudi makwao.
tumethubutu tumeweza na tunasonga mbele
 
kama hiyo ni kweli basi ni aibu kubwa kabisa kwa serikali hii ya msanii huyu. Izingatiwe wazee hawa walilitumikia taifa kwa uadilifu na uaminifu mkubwa na si haki hata kidogo kuwanyanyasa kama serikali inavyofanya. Ingefaa sasa wazee hawa waunge mkono harakati za mageuzi zinazoendelea sasa. Binaafsi nitakipigia kura chama chochote (isipokuwa ccm kwani ahadi zao nyingi huwa ahadi hewa) kitakachoahidi kwa dhati kuli address suala hili la wazee wastaafu kuchakachuliwa haki zao. Naona sasa serikali hii ya ccm inaugua laana iliyotolewa na vikongwe wa iliyokuwa east african community waliodhulumiwa na serikali hii hii ya wezi, vibaka na mafisadi.


"watanzania si mabwege tena" by dr h. Mwakyembe

mimi nasema watanzania ni mabwege. Maana katika hali ya kusikitisha kama hii utawakuta watanzania wamevaa kofia, fulano, na kanga za ccm huku wakiishangilia kama mazuzu. Sikuzote najiuliza hivi hawa watz sio mabwege kweli? Ni mabwege ***** bwegele
 
Hakika serikali ya CCM inaelekea kuanguka,hali ni mbya sna katika taasisi zake hususani Halmashauri kwani mpaka sasa mwaka wa fedha unakwisha(2011/12) fedha za miradi ya maendeleo kwa wananchi hazijafika ktk halmashauri cha kushangaza halmashauri hzo wameshaanda bajeti ya FY 2012/13 sasa sijui wanatwanga maji kwenye kinu,na cha kuckitisha kuna ofisi nyingi za serikali hakuna karatasi,wino,mafuta,karatasi n.k yaani ni ovyo mazingira magumu.

ILA JK YUKO BRAZIL
Prophet of doom
 
Back
Top Bottom