Serikali imeanza kujenga daraja jipya eneo la Wami mkoani Pwani

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Dodoma. Serikali imeanza kujenga daraja jipya eneo la Wami mkoani Pwani ili kuzuia ajali ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara.
tapatalk_1541783987330.jpeg

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eliasi Kwandikwa ameliambia Bunge leo Ijumaa Novemba 9, 2018 kuwa mkandarasi Power Construction Corporation kutoka China amekwisha saini mkataba toka Juni 28, 2018.

Kwandika ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la mbunge wa Hai (Chadema), Freeman Mbowe ambaye hakuwepo na swali hilo liliulizwa kwa niaba yake na Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini.

Mbowe ametaka kujua Daraja la Wami lilijengwa mwaka gani na kama Serikali haioni ajali zilizotokea hapo zinatokana na wembamba wa daraja na kuna mpango wa kupanua daraja hili sambamba na eneo lote la barabara la mteremko wa mto huo.

"Daraja la Wami lenye urefu wa mita 88.75 lililoko mkoa wa Pwani lilijengwa mwaka 1959 na ndicho kiungo cha kutoka Chalinze kwenda ukanda wa Kaskazini," amesema Kwandikwa

Amesema daraja hilo jipya litakuwa na urefu wa mita 513.5 na upana wa mita 11.85 na litajengwa umbali wa mita 670 pembeni mwa daraja la zamani.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri, kazi ya ujenzi wa daraja hilo utakuwa wa miezi 24 na litagharimu Sh67.8 bilioni.

Chanzo: Mwananchi

Daraja la Mto Wami kulikoni Serikali inalifumbia macho? Tunasubiri vifo ndio tukurupuke? - JamiiForums
 
Serikali imeanza kujenga daraja jipya eneo la Wami mkoani Pwani ili kuzuia ajali ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eliasi Kwandikwa ameliambia Bunge leo Ijumaa Novemba 9, 2018 kuwa mkandarasi Power Construction Corporation kutoka China amekwisha saini mkataba toka Juni 28, 2018.

Kwandika ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la mbunge wa Hai (Chadema), Freeman Mbowe ambaye hakuwepo na swali hilo liliulizwa kwa niaba yake na Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini.

Mbowe ametaka kujua Daraja la Wami lilijengwa mwaka gani na kama Serikali haioni ajali zilizotokea hapo zinatokana na wembamba wa daraja na kuna mpango wa kupanua daraja hili sambamba na eneo lote la barabara la mteremko wa mto huo.

"Daraja la Wami lenye urefu wa mita 88.75 lililoko mkoa wa Pwani lilijengwa mwaka 1959 na ndicho kiungo cha kutoka Chalinze kwenda ukanda wa Kaskazini," amesema Kwandikwa

Amesema daraja hilo jipya litakuwa na urefu wa mita 513.5 na upana wa mita 11.85 na litajengwa umbali wa mita 670 pembeni mwa daraja la zamani.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri, kazi ya ujenzi wa daraja hilo utakuwa wa miezi 24 na litagharimu Sh67.8 bilioni.

Pia, soma hoja hii Daraja la Mto Wami kulikoni Serikali inalifumbia macho? Tunasubiri vifo ndio tukurupuke? - JamiiForums
 
Wangesema serikari inatarajia kuanza ujenzi wa daraja la mto wami sio yaanza serikari ya tanzania kalio kweli.
 
asante sana jambo jema sana
Halafu Kuna mijitu inatujaza pumba humu ati serikali imesahau pande hizo Nadhani wametahayari sanaaaa
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Back
Top Bottom