Kampuni Kutoka China Kujenga Daraja la Dar- Zanzibar

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
44,227
50,958
Kampuni ya China Overseas Engineering Group imeonesha Nia ya kujenga Daraja la km 80 Kati ya Dar na Zanzibar,Naibu Waziri Kasekenya amesema Bungeni..

My Take
Kama Daraja hili litajengwa linaweza kutumia zaidi ya gharama za Kujenga SGR.

Swali Je Tunalihitaji Kwa Sasa? Kama Kuna ulazima wa Hilo daraja kujengwa ni Bora tujenge daraja across Lake Tanganyika tuifikie DRC.

=====

SERIKALI imeanza mazungumzo na Kampuni ya China Overseas Engineering Group Company (COVEC) ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika ujenzi wa daraja litakalo unganisha Tanzania Bara na Zanzibar.

Naibu Waziri wa Uchukuzi Godfrey Kasekenya amesema bungeni leo Aprili 28, 2023 kuwa Mazungumzo hayo yameanza Machi 11, 2023 na yalihusisha wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Sekta ya Ujenzi kwa upande wa Tanzania Bara na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa upande wa Zanzibar.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mwantum Dau Haji aliyetaka kujua mpango wa serikali kujenga daraja hilo, Naibu Waziri Kasekenya amesema bado mazungumzo yanaendelea na serikali inakusudia kujiridhisha na teknolojia zinazotumika katika ujenzi wa madaraja makubwa kabla ya kuanza ujenzi.

“Daraja hili litajengwa kwa kushirikiana na sekta binafsi kwa utaratibu wa PPP (Public-Private Partnership),” amesisitiza Kasekenya.

Habarileo UPDATES

Kampuni ya China Overseas Engineering Group imeonesha Nia ya kujenga Daraja la km 40 Kati ya Dar na Zanzibar,Naibu Waziri Kasekenya amesema Bungeni..

My Take
Kama Daraja hili litajengwa linaweza kutumia nusu ya gharama za Kujenga SGR.

Swali Je Tunalihitaji Kwa Sasa?

Ni kama ile ndoto ya cable to Mount Kilimanjaro another pipe dream in a country where they can’t even feed themselves what a waste of time and money
 
Kampuni ya China Overseas Engineering Group imeonesha Nia ya kujenga Daraja la km 40 Kati ya Dar na Zanzibar,Naibu Waziri Kasekenya amesema Bungeni..

My Take
Kama Daraja hili litajengwa linaweza kutumia nusu ya gharama za Kujenga SGR.

Swali Je Tunalihitaji Kwa Sasa?

Sio lazima kujenga madaraja kila mahali hizo gharama za daraja tungeboresha miundombinu ya usafiri majini zanzibar inapendeza sana kama tukiendelea kutumia boats ila napendekeza tuboreshe port za abiria ziwe za kisasa kabisa..
 
Serikali imeanza mazungumzo na Kampuni ya China Overseas Engineering Group Company (COVEC) ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika ujenzi wa daraja litakalo unganisha Tanzania Bara na Zanzibar.

Naibu Waziri wa Uchukuzi Godfrey Kasekenya amesema bungeni leo Aprili 28, 2023 kuwa Mazungumzo hayo yameanza Machi 11, 2023 na yalihusisha wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Sekta ya Ujenzi kwa upande wa Tanzania Bara na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa upande wa Zanzibar.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mwantum Dau Haji aliyetaka kujua mpango wa serikali kujenga daraja hilo, Naibu Waziri Kasekenya amesema bado mazungumzo yanaendelea na serikali inakusudia kujiridhisha na teknolojia zinazotumika katika ujenzi wa madaraja makubwa kabla ya kuanza ujenzi.

“Daraja hili litajengwa kwa kushirikiana na sekta binafsi kwa utaratibu wa PPP (Public-Private Partnership),” amesisitiza Kasekenya.

#HabarileoUPDATES
20230428_114920.jpg
 
Back
Top Bottom