kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,509
- 7,319
Serikali hii awamu ya 6 waachane na kurekebisha mfumo wa elimu maana hawana nia nzuri. Kuna watu wanafikiri kufa magufuli wamepata ushindi na ili kuua fikra za kimagufuli ni kupitia elimu. Awamu hii waache mpango kama walivyoukuta. Hebu fikiri combination zaidi ya 60 ni za kazi gani. Mimi sio mtaalam wa elimu lakini inatustaajabisha. Hasa pale tunaona combination za masomo ya dini mambo ambayo ni imani za watu binafsi. Katiba yetu hairuhusu serikali kujihusisha na mambo ya dini yeyote ile.View attachment 2941239
Siyo siri, wengi tumeshtushwa na msimamo wa sera za elimu kuanza kukumbatia udini.
Waziri Mchengerwa katoa taarifa ya masomo yanayofadiliwa KISERIKALI, masomo au Combination(Tahsusi) ambazo nyingine ni za dini.
Katika hizo combination masomo ya Kiislamu na kuna Divinity vile vile.
Sera hizi zinataka na vikao vipi vya Chama CCM, Wadau wa Elimu, au wananchi kushirikishwa, mabadiliko katika elimu yametokana na nini na kwa ridhaa ya nani?
Serkali haipaswi kuingilia katika Kueneza Dini kwa Njia yoyote ile Ni kinyume cha Katiba..