Serikali iangalie utaratibu mzuri katika kusafirisha mafuta hasa kwenye majiji makubwa yenye msongamano.

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
May 11, 2015
23,369
54,771
Assalamu Aleikum, Tumsifu Yesu Kristo.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania................

Nina imani viongozi mbalimbali wa serikali na wizara mbalimbali ni wafuatiliaji wazuri wa JF hivyo maoni yangu yatawafikia kwa njia hii niliyochagua. Kwa mara kadhaa tumekuwa tukishuhudia msongamano wa magari ya mafuta hasa Dar es Salaam yakiwa barabarani yamesheheni mafuta yakisafirisha kwenda maeneo mbalimbali ya nchi.

Utaratibu huu kwangu mimi kuna muda nauona siyo utaratibu salama kwa raia na watumiaji wengine wa barabara. Katika jiji kama Dar es Salaam barabara nyingi huwa busy kuanzia saa 10 alfajiri hadi saa 6 usiku kwa nyakati hizo barabara nyingi hujumuisha magari mbalimbali na foleni kubwa ila cha kushangaza katikati ya foleni hizo unakuta kuna malori kadhaa yenye mafuta. Ni suala hatari sana, kwanini tusiweke utaratibu wa magari haya kutumia barabara nyakati ambazo idadi ya watu barabarani imepungua mfano kuanzia saa 6 usiku hadi saa 11 alfajiri ili magari haya yawe yanatumia muda huo kuondoka katika viunga vya jiji na kuelekea huko zinapotakiwa kwenda.

Kwenye sehemu ambazo zina msongamano wa magari na foleni ama majiji yenye foleni yaweke utaratibu mzuri wa kupitisha hayo magari yenye shehena ya mafuta kuliko kuacha kila muda gari likijisikia kupita linapita bila kujali usalama wa watu.

Najua hatuna uwezo wa kujenga barabara maalumu kwa ajili ya magari ya mizigo ila walau tuweke utaratibu wa kutoka kwa magari haya yenye mafuta yawe yanatumia barabara nyakati ambazo matumizi ya barabara si makubwa sana kwa raia.

Wizara ya uchukuzi na Wizara ya nishati angalieni hili mje na utaratibu mzuri ambao utakuwa na kipaumbele cha usalama kwa raia au watumiaji wengine wa barabara hasa kwenye mji yenye misongamano.
 
Yaani nikweli kabisa, unakuta upo kwenye gari ndogo, halafu gari za mafuta zimekuweka kati jamani huwa nawaza sana, wazo zuri sana, yangekuwa yana anza safari angalau hata saa 4- 5 usiku ingekuwa vizuri sana.
 
Kweli kabisa, magari haya yakianza kutoka saa 5 hadi saa 10 au saa 11 alfajiri yanakuwa hayapo mjini.

Kwenye miji isiyo na foleni wanaweza kuacha yakaendelea kupita ila mikoa yenye msongamano kama Dar waje na utaratibu rafiki na wenye kutazama zaidi madhara ikitokea gari limelipuka.
 
Yaani hapo Mandela road inakuwa nyeupe yanajiondokea tu
 
Yaani hapo Mandela road inakuwa nyeupe yanajiondokea tu
Mandela road ndiyo lango kuu la hayo magari ni suala ambalo tunaliona la kawaida ila hatari sana kwa usalama wa watumiaji wa barabara. Na pia hapo hapo kuna wale mateja wanakuwa wanafungua magari yaliyotupu kuchukua mabaki ya mafuta aiseeee.
 
Nahiyo barabara ilijengwa kwa ajili hayo malori kama sikosei, kuna siku waiba mafuta walijichanganya wakafungua gari ya majitaka naona dereva alifurahi kweli kupunguziwa safari
 
Nahiyo barabara ilijengwa kwa ajili hayo malori kama sikosei, kuna siku waiba mafuta walijichanganya wakafungua gari ya majitaka naona dereva alifurahi kweli kupunguziwa safari
Ulikuwa Buguruni mateja wakaamua kuchafua hali ya hewa.
 
Back
Top Bottom