satellite
JF-Expert Member
- Nov 18, 2010
- 616
- 166
Kazi ya Producer sio kutengeneza script na wala si lazima awe mwandishi ingawaje ni kweli pia kwamba wapo ma-producer wengi ambao ni waandishi wa script vile vile kama huyo JJ Abram.
Script inaweza kuandikwa na Chige as screenwriter ikafikishwa kwa JJ Abram as Producer na yeye ndie akaunda production team na akateua director. Script kutoka kwa Chige ikishatua kwa JJ Abram, yeye ataipeleka production department ambako itafumuliwa na kutengenezwa production/shooting script! Hii production script inaweza kuchukua yote niliyoyaandika au inaweza kuongeza na kupunguza baadhi...! More often than not, production/shooting script haiandikwi na Producer bali na Director akishirikiana na Cinematographer. Kazi ya Cinematographer hapo inakuwa description of technical issues... that's camera movement ambayo, professionally si kazi ya mwandishi/screenwriter ingawaje nimeona script nyingi za Kibongo Screenwriters wanaandika/wana-include camera movements kwenye script zao. Mwandishi ukijaza ma-camera movements kwenye script yako kisha ukaifikisha Hollywood, wala hakuna atakayeisoma!
Hata hivyo, pamoja na yote hayo bado kazi kubwa inakuwa tayari imefanywa na mwandishi! Wakati mwandishi atakuwa ameandika, kwa mfano feature film kwa miezi mitatu na zaidi, shooting script inaweza kuwa imeandikwa ndani ya wiki moja! Na hata ukija kwenye series, the same applies.
Yeah I do agree with above points