Sera za Marekani na China: Changu changu chako changu, ukanda mmoja njia moja (protectionism policy)

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
950
2,866
SERA ZA MAREKANI NA CHINA: CHANGU CHANGU CHAKO CHANGU,UKANDA MMOJA NJIA MOJA (PROTECTIONISM POLICY)

Leo12:25hrs 26/09/2021

Kila mtu analinda cha kwake sisi tu huku Tanzania tuna dharau vya kwetu hata panadol tunataka za kenya tukienda dukani,Watanzania tunadharau lugha yetu ya Kiswahili lakini Kiswahili ndio kinatutambulisha duniani kwa kubeba utamaduni wetu,Tupende vya kwetu sio kupenda kiingereza cha mzungu kinachobeba utamaduni wa mzungu! China ni nchi iliyotembea peke yake kwa muda mrefu,inatumia lugha yake ya Kichina inayobeba Utamaduni wake na imepata maendeleo makubwa kuifikia Marekani,Miaka 50 iliyopita China ilikuwa sawa tu na Tanzania,Wachina ndio waliotufundisha kushona viraka kwenye nguo zetu walipokuja kujenga reli ya Tazara,wameshona viraka hadi wamejua kushona nguo kamili,na leo wanatuuzia sisi pamba kali,wakati wakishona nguo zao viraka,daima hawakuomba nguo mpya Marekani au Urusi zilizokuwa Nchi tajiri wakati huo,Wao Wachina hawakuomba pesa za mikopo,Mao Zedong aliomba teknolojia (Transfer of technology),

Mao Zedong aliwaamsha Wachina saa kumi na mbili asubuhi kufanya kazi,aliyechelewa alifungwa jela na asiyekuja aliuawa kwa risasi, kwenye kuwahi,Leo Mchina anafika eneo la tukio saa moja kabla ya tukio ili kuepuka kuchelewa, hii ni faida aliyowaachia Mao Zedong, Moto wa Mao Zedong unafanana sana na Moto wa John Pombe Magufuli,naamini Watanzania wameachiwa vingi vya kuendeleza kutoka kwa Hayati Rais John Pombe Magufuli.Wachina hawakuwa na sauti kwenye Umoja wa Mataifa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndiye aliyekwenda kuwasemea Wachina pale Umoja wa Mataifa ilipoitenga China kama sio sehemu ya Dunia,hivi leo China ni kubwa kuliko Tanzania, sio tu kubwa kuliko Tanzania bali China ni kubwa kuliko Marekani, nitakuelezea hapo chini,walikufa Wachina Milioni 60 ili kuipata China ya sasa,nani aliyeibadili China masikini kuwa China tajiri? Ni Mao Zedong huyu namfananisha na John Pombe Magufuli,laiti John Pombe Magufuli angepata kutawala miaka 30 basi angefanya aliyofanya Mao Zedong kuibadili Tanzania masikini kuwa Tanzania tajiri, hivi leo China inajitosheleza,unaweza kufanya chochote duniani hata kumtetemesha Marekani,Google play store ya Marekani sasa imepigwa marufuku kule China,Wachina wanatumia application stores zao na ni popular;-

1. Myapp ya tencent
2. Baidu app store
3. Xaiomi Phone store
4. 360

Zipo application store nyingi tu ambapo kwa raia wa china atapata application za kutosha tena zikiwa na mbadala wa popular app popular zote kuanzia facebook mpaka google maps.

Nchi zimejiimarisha na zina mifumo imara ya kijamii, kisiasa, kiuchumi,ili kulinda cha kwetu kama afanyavyo Marekani, Urusi, China, India, Uingereza na Rwanda basi, kukuza uchumi wa Viwanda, Uzalendo wetu uanzie kwenye kupenda vya kwetu kwanza na kama vibovu tukatoe maoni kwa wazalishaji wetu tuwachane nini chakufanya sasa kibaya zaidi customer care ya company za bongo hawana hata utamaduni wa kuzunguka masokoni kuchukua maoni (feedback) kwa wateja wao juu ya ubora wa bidhaa zao. Leo nitakuangazia kwenye Sera ya Changu Changu, Chako Changu "what's mine is mine and what's yours is negotiable" inayofanywa na Marekani na China inayotekeleza Sera ya Ukanda mmoja njia moja.

Marekani haijawahi kuwa nchi yenye nia njema ya kulinda utaratibu wa kimataifa, badala yake, mara kwa mara inakwenda kinyume na utaratibu wa kimataifa na hata kukiuka sheria za kimataifa,mara nyingi Marekani imefanya hivyo kutetea maslahi yake yaliyowahi kutishiwa na Ujerumani, Urusi na hivi sasa China, Maendeleo ya China yameishangaza sana Marekani,Tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango zaidi ya miaka 40 iliyopita, wastani wa ukuaji wa uchumi wake kwa mwaka umefikia karibu asilimia 10, na watu milioni 800 nchini humo wamefanikiwa kuondokana na umaskini.

Maendeleo ya uchumi pia yameleta ongezeko la nguvu za kijeshi. Wachambuzi wengi wanaona kuwa, kama Marekani ikifanya vita na China barani Asia, China itapata ushindi, wanakalenga wanaamini kuwa, kufuatia ongezeko la uwezo wa kitaifa, China inajaribu kurekebisha utaratibu wa kimataifa, ikiwemo mfumo wa kiuchumi duniani, Kwa mfano, China imetoa pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, kuanzisha Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia, na Benki mpya ya Maendeleo ya BRICS, zaidi ya hayo, China pia inataka kurekebisha mfumo wa usalama duniani.

Ili kukabiliana na maendeleo ya China,Marekani imechukua hatua mbalimbali ngumu dhidi ya China, ikiwemo vizuizi dhidi ya makampuni ya teknolojia ya juu ya China, haswa Huawei, vita ya kibiashara, kupinga China katika masuala mengi yakiwemo Bahari ya Kusini, Taiwan, Hong Kong, Xinjiang, na utafutaji wa chanzo cha virusi vya Corona,Licha ya hayo, Marekani pia inajitahidi sana kuchochea nchi nyingine kupinga China kwa visingizio vya haki za binadamu, usalama, makabila madogo, na mfumo wa kisiasa.

Ni lazima Marekani itafakari kwa makini jinsi ya kukabiliana na maendeleo ya China, na mkakati wake mpya unapaswa kuzingatia zaidi “kujizuia na kutafuta maafikiano” badala ya “kupingana”. Hii ina maana kuwa, Marekani inatakiwa kukubali kwamba utaratibu wa kimataifa unaonesha mabadiliko ya nguvu duniani, na zaidi ya hayo, Marekani pia inapaswa kuheshimu kwa dhati sheria za kimataifa, na kutotumia nguvu ovyo, ili kupata uaminifu wa nchi nyingine.

-Ushindani usio sawa (Unequal Competition)

Top five ya company zinazotengeneza simu kwa wingi duniani ya kwanza ni samsung,huawei technologies,Apple, Vivo na Xiaomi

Hizo mbili ni za China ndio maana nasema hata apple wakiondoka china bado china ataendelea kufanya production ya simu zake za ndani anazo tengeneza mwenyewe zilizo base china

Apple aongoza kwa market share ya simu duniani japo miaka hii ya karibuni ndio alipitwa kwenye kutengeneza simu kwa wingi na huawei na Samsung

Apple's CEO alikiri kabisa soko la iPhone linaanza kuwa baya kwa sababu ya trade tension ya china na USA na kama siku Apple watabaniwa kule china,apple itapata hasara zaidi kuliko China

Wachina watapoteza ajira na apple watapoteza market yao kubwa zaidi duniani na revenue ya kutosha na hili gap la market ya china linazibwa na xiomi na huawei brands hawa jamaa wamefundishwa sana kupenda vya kwao.

-Huawei anaongoza kwa Uzalishaji wa simu nyingi duniani.

Unaweza ukawa unaongoza kwenye market share lakini usiongoze kwenye utengenezaji wa wingi wa bidhaa zako

Apple ana market share kubwa sana sababu ana revenue kubwa kuliko mobile maker wote duniani lakini sio kwamba yeye ndio mtengenezaji wa simu nyingi duniani,

Apple ana revenue kubwa sababu bei ya vifaa vyake ni kubwa kushinda hao maker wote waliobaki na ndio maana ana revenue kubwa

Apple kapitwa na hauwei kwa uzalishaji wa simu nyingi duniani ila hajapitwa kwenye "market share wala revenue".

Nifafanue kidogo,ukichukua GDP peke yake kabla hujaweka PPP unakua hujaelezea uchumi vizuri wa nchi husika ndio maana hata IMF huwa wanaangalia uchumi uliobase kwenye nguvu ya manunuzi(purchasing power parity)

Kwa GDP peke yake USA ina global share ya 24% ila GDP based on PPP ambayo ni indicator iliyokomaa zaidi kwenye kuelezea uchumi wa nchi,According to IMF GDP based on PPP USA ana 17% ya global economy,

Wazungu wajanja mno wanatuchezea kwa kigezo cha uchumi ambao wanautwist na formular walizojitengenezea wao mwaka 2016 Marekani walivyozidiwa PPP na china wakabadili gear angani wakaanza kusema PPP sio kigezo kizuri cha kiashiria cha uchumi na wakati hapo mwanzoni ndio ilikua kigezo kikubwa kabisa chakuonyesha uchumi wa nchi husika,wakadai kigezo kizuri ni GDP na wala sio ile per capita kama zamani iliyokua,siku wakizidiwa GDP sijui itakuwaje,watachange tena gia angani,wanatupeleka peleka tu,Mimi ningeshauri hela tuchapishe wenyewe na thamani ipimwe kwa kuipala dhahabu hela hiyo,

Zamani kabisa ilikua ukiwa mtumiaji mkubwa wa nishati duniani wewe ndio unakua na kiashiria cha uchumi mkubwa na ulioimarika,baada ya Waafrika kuamka na kuimiriki nishati wakatoa hiyo thamani wakaiweka kwenye makaratasi,ni fitna juu ya fitna,karatasi tu eti lina thamani,sasa karatasi la dola na karatasi la shilingi lina tofauti gani?

-Marekani na Sera ya Changu Changu Cha nje Cha kwetu.

Marekani ina hifadhi kubwa ya mafuta ndani ya marekani,ikiyachimba basi inaweza kujitosheleza kwa miaka 50,lakini mafuta hayo hawajaanza kuyatumia,wao wanatumia mafuta ya nje ya Marekani,si hilo tu mfano,Bajeti ya Marekani ni Trillioni 200 kwa Mwaka,pesa hizo zipo Marekani lakini Marekani haitatumia pesa hizo, Marekani itatumia pesa kutoka nje ya Marekani,sio za mkopo,hapana,ni kutoka kwenye uwekezaji wake unaofanyika dunia nzima,Changu Changu,Cha kwako ni Cha kwetu,tumeona hivyo kwa Mataifa ya China, Ujerumani,Uingereza,Urusi,South Afrika,Rwanda na Uganda.Wanakalenga wanadai kuna mataifa wanaendeleza nchi zao kwa kuiba dhahabu za Kongo na kwenda kujenga uchumi wa nchi zao na kusaidia Wananchi wao.

Marekani imekuwa ikilinda na kuhifadhi vya kwake huku ikienda nje ya Marekani kutafuta mali,Marekani inapokutana na mpinzani kwenye biashara za nje inaweka vikwazo,kila mtu anayefanya biashara vizuri kwenye maslahi ya Marekani,basi Marekani anamuwekea vikwazo hapa inaonekana ameshindwa kufanya biashara ushindani umemshinda kwa kiasi kikubwa na nchi za ulaya zimeanza kumstukia,

Tuangazie mfano huu kujenga tu bomba la gas kutoka russia kwenda Germany hataki ili tu aje kuuza LNG yake ambayo ni very expensive kwa ulaya

Na Germany imesema haitakubali watajenga tu hilo bomba maana anajua faida zake na yule ndio powerhouse ya Europe na bomba kwa sasa lipo 70%

Juzi Italy imetangaza kujiunga na silk road project ya china ambayo inapunguza karibia nusu ya gharama za biashara kwa sasa marekani alivyosikia hivyo kaanza kumpiga mkwara Italy

One road,one belt (silk) ni muunganiko wa network za barabara,reli na meli na njia zingine za usafiri kuanzia china mpaka ulaya mpaka africa kwa hiyo itafikia kipindi utatoka na gari/train kutoka china mpaka ulaya mpaka africa hapo ita harakisha sana global trade kwa kiasi kikubwa sasa hapa marekani anaona wivu sana china atapata influence kubwa mno na faida pia,kila atakaye ingia kwenye hiyo project anampa vikwazo huko ni kutapa tapa aache watu wafanye biashara kama kashindwa ushindani akae pembeni au ajipange upya.

Marekani si kama tu inawatendea vibaya washirika wake wa Ulaya, bali pia inapuuza maslahi ya wenzi wake wengine. Kwa miaka 20, Marekani ilifanya vita nchini Afghanistan, mwishowe iligundua kuwa haiwezi kupata faida tena kutoka kwenye nchi hiyo, ikaamuru kuondoa vikosi vyake vyote nchini Afghanistan, bila kujali serikali ya nchi hiyo iliyoanzishwa chini ya msaada wa Marekani, na washirika wake waliotuma wanajeshi pia nchini Afghanistan. Kitendo hicho kilisababisha kuanguka kwa serikali ya Afghanistan mara moja, na usumbufu kwa wanajeshi wa nchi nyingine nchini humo.

Marekani imezoea “kuchoma kisu” washirika wake ghafla. Kama tabia nyingine nyingi za kushangaza za nchi hiyo, kitendo kama hiki pia kinatokana na ubinafsi na umwamba wake. Kama ncha pekee duniani, Marekani hufanya mambo yake bila kujali maslahi ya nchi nyingine, hata washirika wake. Hivyo nchi zinazoisaidia Marekani kupinga China, zikiwemo Lithuania, Uingereza na Australia, lazima zitafakari ikiwa Marekani itazichoma kisu ghalfa, kwani kutokana na maslahi, hakuna nchi ambayo Marekani haiwezi kuiacha.

Kila alicho nacho marekani kinaweza kupatikana kwingineko. Ni kiasi cha dunia kujipanga tu. Lakini marekani hawezi kukubali kuishi bila kufanya biashara ya dhuluma na nchi ingine. Patachimbika. Atafanya juu chini ahujumu zoezi hilo.

Akipata nchi mbili tatu za kufanya nazo biashara atatumia ndege za kivita na manowari za kijeshi kusindikiza meli na ndege zitakazo kuwa zina safirisha hizo bidhaa zake, Ole wako uwe kikwazo njiani,

Utajiri mkubwa wa karibu nchi yeyote unapatikana kwa kufanya biashara na nchi ingine, na hasa kwa kufaidika zaidi, yaani kwa kunyonya, Tanzania tumepigwa sana kwenye biashara hizi,tumetoa 97% tumepata 3%,Marekani hawezi kushamiri au hata kudumu bila kuchukua coltan, dhahabu na nk karibu na bure Kongo na kwingineko na kuuza bidhaa zake kote duniani,

-Tanzania tunahitaji sera ya "Vya Tanzania ni vya Tanzania na vya nje ya Tanzania ni vya kwetu".

Tanzania inahitaji kiongozi mfano wa Hayati Rais Daktari John Pombe Magufuli,ili tuweze kusema "Vya Tanzania ni vya Watanzania tu,na vya nje ya Tanzania ni vya kwetu". Tanzania inahitaji kuwa na hifadhi ya Dhahabu,Almasi, Tanzanite,Mafuta na madini mengine yote yanayopatikana Tanzania, Tanzania inahitaji kuwa na hifadhi ya rasilimali ya mbuga za Wanyama na tuwe na Wanyama wanaopatikana Tanzania tu, Tanzania tunatakiwa kuwa na share kubwa pamoja na udhibiti mkubwa kwenye kila International Macroeconomic variable kama vile kuwa na stock kubwa ya Mafuta, dhahabu, soko la fedha karibu zote duniani, viwanda vikubwa pamoja na FDI dunia nzima

Vitu hivyo vitatupa sisi Watanzania kinga tosha ya kutoadhibiwa na vikwazo kutoka mataifa makubwa,ili waje kusema kumwekea vikwazo Tanzania au kumtenga au kumfungia Tanzania ni kama kuufungia uchumi wa dunia nzima,kwa sababu hizo na nyingine, kuiwekea vikwazo Tanzania ije ifahamike kama kuufanyia subotage uchumi wa dunia,maana hakuna nchi itabaki salama.

Nashauri Tanzania itumie Dhahabu,Almasi na Tanzanite kuipaka kwenye pesa zake kama thamani ya fedha yake,wakati Marekani wanatumia monetary financing policy zaidi kwa kuprit peper notes na kusupply nje kwa kununua bidhaa hasa mafuta na bidhaa zingine maana pesa yake inaitajika kila kona ndio maana kodi ipo chini uwezi linganisha kwa mataifa mengine mfano Ujeruman kodi ipo juu,na ndio maana wao wanalipa pesa nying hasa ktk huduma na kuvutia expertise kwakuwa pesa wana print wenyewe ( Federal Reserve) Tanzania ichimbe ihifadhi mafuta yake yaliyo ardhini hata pale China itakapokuwa ndio mnunuaji mkubwa wa mafuta na kuanza kununua mafuta kwa kutumia pesa yake yuan hapo tutashinda vita siku za mbele miaka ishirini ijayo,

Je Tanzania hatuwezi kutengeneza vinywaji vyetu vikawa vitamu kuliko Cocacola,Je Watanzania hatuwezi kutengeneza magari yetu,Je Watanzania hatuwezi kuimarisha Bongo Movie na kucheza sinema zetu!?,Je Watanzania hatuwezi kutengeneza miziki wetu!?Je Watanzania hatuwezi kutengeneza nguo zetu!?,Je Watanzania hatuwezi kutengeneza mitambo yetu viwandani,n.k.basi.lakini haiamaanisha kuwa Tanzania ikiwekewa vikwazo itashindwa kuvumilia,kwa maana hata Cuba imevumilia,Irani imevumilia,Urussi imevumilia na China imevumilia na Leo hii China ni Taifa kubwa linaloogopwa na Marekani.

Zamani wazungu walikuwa wanatumia gold kama ndio njia yakufanya biashara kati ya taifa na taifa,Kutokana na matatizo ya gold ndipo pesa ilipo linganishwa thamani kwa gold.

Dollar ya Marekani ilipata kukubalika na dunia kama sehemu yao ya akiba ya taifa kutokana na Marekan kuwa na akiba kubwa ya Gold,lakini Marekani kuakikisha anakuwa monopoly katika biashara ya kimataifa kwa kufanya pesa yake inadominate ndipo walianzisha World Bank na IMF kwa picha ya Dunia.

Kifupi hadi sasa dollar ya Marekani imetawala 64% ya hazina kuu ya mataifa yote duniani(International reserve currency) ikiwa na maana mataifa mengi yameweka hakiba yao katika mfumo wa dollar,ikifuatiwa na Euro ambayo ina zaidi ya asilimia 20, British Pound, Yen Na Yuan ya china ambayo hadi sasa inamilik 1% ya international reserve.
Takwimu zinaonyesha kupaa kwa kasi ya pesa ya China na kushuka kwa pound na Dollar.

Mfano sasa Australia na China wameingia makubaliano ya kutumia Yuan ya china na kuacha kutumia dollar.

Kwa maelezo hayo ni kwamba kuiwekea vikwazo marekani kiuchumi ni kuacha kutumia dollar yake ambayo anaitumia kuendesha maisha yake ya kila siku jambo ambalo linahitaji muda kwa fedha zingine kupata world confidence, ndio maana china ameanza taratibu kulifanyia kazi kama mpinzani mkubwa wa Marekani.

Ndio maana trade balance ya Marekani utaona kunadeficit kubwa sana ila mambo yao yako poa maana yake wao supply ya dollar tu ambayo ipo kwenye benki ya duniani kote kunawawezesha wao kupata vyote wavitakavyo duniani.

Marekan inapo sema inaweka vikwazo kwa nchi fulani inamaana inacontrol supply ya dollar yake katika nchi husika na kukufanya ukose nguvu ya kufanya biashara pia kutumia nguvu za kijeshi kuzuia kuingia na kutoka kwa bidhaa na kutishia trade partner wako kuwa nae atamuwekea vikwazo hapo ndipo kila mtu anaogopa kupoteza hashima yake ambayo ipo kwa dollar.

Ila hili lilisha julikana ni tatizo, china ikiwa ndio nchi inayo ongoza kwa kuwa na Dollar Reserve kubwa ameanza kubadilisha na kuweka katika mfumo wa Yen ya Japan na Euro ili kupunguza stock ya Dollar,

Nimalizie kwa tafakari Jadidi juu ya nchi yetu ya Tanzania,Je tutampata wapi Kiongozi wa kusema "Vya Tanzania ni kwa ajili ya Watanzania tu na vya nje ya Tanzania ni vyetu wote" kwa maana hii ndio sera ya kila Taifa kubwa na mataifa yote ya kibepari,sisi hatuwezi kuendelea kukubali watu watumie vya kwetu halafu vya kwao vibaki vyao peke yao.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the effect of micro-financing on Poverty Reduction.
 
Back
Top Bottom