September 13 maandamano makubwa kufanyika nchini; ni ya vijana wanaotafuta ajira

Kwani mmeambiwa kuajiriwa ni lazima? Serikalini nafasi zimejaa,maeneo ya kilimo yapo kibao nendeni mkajiajiri shambani
 
Nimeona juzi Kigoma wameandamana kufikisha ujumbe wao kutokana na mwekezaji kupewa ardhi ya wananchi, kisha nikaona huko Arusha juzi wakiandamana kupinga bomba kukatwa na mkandarasi wa barabara kwa siku kadhaa na wananchi kuachwa bila maji kwa muda mrefu.........kote, wananchi wameandamana kwa amani na kufikisha ujumbe wao. Hiyo Tanzania yetu tunayoijua.
 
Kwa hiyo vijana wooote wanataka waajiriwe na serikali! Hakuna hata mmoja wao wenye wazo la kujiajiri?

Kwa hii hali ya uchumi ukijiajiri utatusua kweli?.... Kama Landmark hotel kabadili kuwa hostel, Mimi muuza chips nitatoboa kweli?.... Enzi za Jakaya sawa not now...

Serikali ndio mwajiri Mkuu duniani kote... Pili, kwa sasa tumechoka nyimbo za kutumbua, tunataka mipango ya uchumi, ya kujenga viwanda ili vijana wapate ajira
 
Yani mkisubutu tu kuandamana mtakipata ambacho walitarajia kukipata wale ambao wangeandamana na ukuta wao
 
Umoja wa watafuta ajira (TJS) leo umetoa kauli ya kufanya maandamano ya amani kwenda Ikulu ili kuomba kauli sahihi kuhusu ajira kutoka serikalini.

Huo umoja wenu koko umesajiliwa kisheria? Nani kawasajili na ofisi zenu ziko wapi? Ukidakwa na polisi kwa uchochezi utaanza kujinyea kuwa unaonewa.TCRA na polisi mtu wenu huyo mkamateni mbaneni
 
Umoja wa watafuta ajira (TJS) leo umetoa kauli ya kufanya maandamano ya amani kwenda Ikulu ili kuomba kauli sahihi kuhusu ajira kutoka serikalini.

Hatua hii imekuja baada ya kutokea kwa mkanganyiko mkubwa kuhusu suala hilo la ajira. Mwanzoni Rais alisema baada ya miezi miwili. Badae waziri Simbachawene akasema hakuna ajira mwaka huu. Mwanzoni mwa wiki hii (Jumanne) waziri Kairuki ambaye yuko ofisi moja na Simbachawene alisema ajira mpaka hapo umma utakapotaarifiwa..

Hivyo basi TJS wameona kuna kauli nyingi za kukanganyika, na kwa hali hiyo wameandaa maandamano makubwa yatakayofanyika tarehe 13. 09.2016. Maandamano hayo yataanzia Buguruni via Kariakoo~Lumumba~Ohio~Ifm mpaka Ikulu...

Ni wito kwa vijana wote ambao wanatafuta ajira, ambao walijiajiri na wamejiajiri ila mambo hayakwenda vizuri kujitokeza kwa wingi wenu... Ili kwa pamoja tukamuona Mh. Rais wetu mpendwa ili tupate majibu ya kina!

Hawa lazima watazuiliwa kwa sababu wana mawazo ya kipinzani-pinzani.
 
Hayo maandamano wanaweza kuzuia bila sababu za msingi .Ajira zimesitishwa kutokana hali mbaya ya uchumi wetu.
 
Tanzania hii tulipofika maandamano ruksa nyumbani kwako tu- ukumbini hadi chumbani to and fro indefinitely.
 
if you can't do it today,what makes you think you can do it tomorrow.....
 
Back
Top Bottom