Umoja wa watafuta ajira (TJS) leo umetoa kauli ya kufanya maandamano ya amani kwenda Ikulu ili kuomba kauli sahihi kuhusu ajira kutoka serikalini.
Hatua hii imekuja baada ya kutokea kwa mkanganyiko mkubwa kuhusu suala hilo la ajira. Mwanzoni Rais alisema baada ya miezi miwili. Badae waziri Simbachawene akasema hakuna ajira mwaka huu. Mwanzoni mwa wiki hii (Jumanne) waziri Kairuki ambaye yuko ofisi moja na Simbachawene alisema ajira mpaka hapo umma utakapotaarifiwa..
Hivyo basi TJS wameona kuna kauli nyingi za kukanganyika, na kwa hali hiyo wameandaa maandamano makubwa yatakayofanyika tarehe 13. 09.2016. Maandamano hayo yataanzia Buguruni via Kariakoo~Lumumba~Ohio~Ifm mpaka Ikulu...
Ni wito kwa vijana wote ambao wanatafuta ajira, ambao walijiajiri na wamejiajiri ila mambo hayakwenda vizuri kujitokeza kwa wingi wenu... Ili kwa pamoja tukamuona Mh. Rais wetu mpendwa ili tupate majibu ya kina!