Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akitangaza Matokeo ya Sensa na Watu na Makazi ya Mwaka 2022 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma leo tarehe 31 Oktoba, 2022



Samia Suhuhu Hassan - Rais
Nataka niitangazie dunia kuwa Sensa ya watu na makazi ya 2022 imefuata vigezo vilivyowekwa na umoja wa mataifa.

Tumeandika historia kwa mara ya kwanza tangu tupate uhuru, tumeweza kupata idadi ya majengo yote pamoja na anwani za makazi.

Leo hii tumefika ukingoni mwa zoezi la sensa tulilofanya kwa ufanisi mkubwa. Sensa hii imefuata vigezo vyote vya kimataifa.

Kwa mamlaka niliyopewa na katiba ya JMT ya mwaka 1977, nawatangazia kuwa Tanzania ina idadi ya watu 61,741,120.

Watu 59,851,347 wapo Tanzanzia bara na 1,889,773 Tanzania zanzibar.

Wanawake wapo 31,687,990 sawa na asilimia 51 ya watu wote na wanaume ni 30,530,130 sawa na asilimia 49 ya watu wote.

Kati ya mwaka 2012 hadi 2022, ongezeko la watu ni 19,812,197 sawa na asilimia 3.2

Tanzania bara, mkoa wa DSM unaongoza kwa watu nchini, wapo 5,383,728 sawa na asilimia 8.7 ya watu wote nchini, na mkoa wa pili ni mwanza wenye wakazi 3,696,872 sawa na asilimia 6.

Idadi ya mejengo ni 14,348,372 ambapo Tanzania bara yapo 13,907,951 na Zanzibar yapo 440,421

Vituo vya kutolea huduma za afya vipo 10067 ambapo zahanati zipo 7889, vituo vya afya 1490 na hospitali 688.

Upande wa shule, zipo 25,626 ambapo shule za msingi zipo 19,769 na shule za sekondari zipo 5857

Makadirio yanaonesha kuwa hadi kufikia mwaka 2025 Tanzania itakuwa na watu 67,962,097 na hadi kufikia mwaka 2050 idadi itafikia 151,252,429.

Asanteni kwa kunisikiliza, Mungu aibariki nchi yetu, Mungu aibariki Afrika. Asanteni sana kwa kunisikiliza.
 
Naamini kutakuwa na takwimu sahihi kwa maendeleo na mgawanyo sahihi wa keki ya taifa. Kipindi cha mwendazake si ajabu takwimu zingepikwa ili tu chattel ionekane ina watu wengi. Ili iwe mkoa na hatimaye jiji.. (Apumzike panapo mstahili)

PS

Mkoa kama wa Mbeya, una wakazi wengi, una changia Pato la serikali kwa kiasi kikubwa. Ila hamna barabara "double road"

Miundombinu duni, mji haujapangika, ardhi wana pima viwanja halafu wanapotea.. Umeme, maji, barabara kazi kwa wanunuzi kukarabati, Rejea viwanja vya iduda, mbeya peak, isyesye.
 
Hivi angeitisha tu Press conference pale Ikulu kwa ajili ya kuutangazia umma kilichomo kwenye taarifa ya sensa akiambatana na maafisa wawili watatu wa takwimu na Msemaji wa ikulu KUNGEKUWA NA SHIDA GANI?

kulundika watu wote hao na kuwalipa per diem huku V8 zikiunguruma na tayari Taifa lina mahitaji meeengi sana ni kushindwa kufikiri vizuri.
 
Hivi angeitisha tu Press conference pale Ikulu kwa ajili ya kuutangazia umma kilichomo kwenye taarifa ya sensa akiambatana na maafisa wawili watatu wa takwimu na Msemaji wa ikulu KUNGEKUWA NA SHIDA GANI?.

kulundika watu wote hao na kuwalipa per diem huku V8 zikiunguruma na tayari Taifa lina mahitaji meeengi sana ni kushindwa kufikiri vizuri.
ccm niwezi tu
 
Hivi angeitisha tu Press conference pale Ikulu kwa ajili ya kuutangazia umma kilichomo kwenye taarifa ya sensa akiambatana na maafisa wawili watatu wa takwimu na Msemaji wa ikulu KUNGEKUWA NA SHIDA GANI?.

kulundika watu wote hao na kuwalipa per diem huku V8 zikiunguruma na tayari Taifa lina mahitaji meeengi sana ni kushindwa kufikiri vizuri.
THEY DON'T CARE
 
Hivi isingetosha tu kwa Msemaji wa Ikulu / Rais kuitisha Press Conference na kutupa Matokeo ya Sensa kisha Maisha yaendelee na Pesa iliyotengwa kwa Tukio / Hafla ya leo itumike kwa Mambo mengine Muhimu na ya Kidharula kwa Maendeleo ( Ustawi ) wa Watanzania na Tanzania yao?

Kuna wakati Watu wengine huwa wanatulazimisha akina GENTAMYCINE tuwadharau kwa kufanya Vitu ambavyo kwa Umasikini mkubwa uliopo kwa Watanzania wala hayakupaswa Kufanyika na hata Watu wenye Akili Kubwa kamwe wasingethubutu kufanya hivyo kwani Taifa linapoteza Pesa kwa Jambo la Kawaida sana..

Kasirikeni ila mkiharibu nitawasema.
 
Back
Top Bottom