Sengerema: Fransico Kimasa Shejamabu ajiunga CHADEMA, Kugombea Ubunge

Haachi kunishangaza , hebu apunguze kasi.
Ukawani hakuna uroho wa madaraka fasta fasta namna hiyo.
Atulie chama na wananchi waamue.
 
Wana Sengerema na Chadema tuwe makini na watu wa aina hii. This is Shibuda type! Haiwezekani mtu anahamia Chadema na kutangaza nia ya kugombea ubunge!!!
Huyo apigwe chini.... Sasa kipindi Alphonse mawazo amekuja huko kukampeni alishindwa nn kujiunga? Na kwann atangaze ubunge wakat ss ndo tulojenga miziz ya chama letu huko?
 
Wale wanaojitoa dakika za mwisho na kuruhusu mafisadi kupita bila kupingwa

Huo ndio utakuwa wasiwasi wa wengi.Kuingia kwa nia ya kugombea tu ubunge mara nyingi hao wanakuwa mamluki wanaotumwa na chama tawala kuleta vurugu kwenye vyama vyenye nguvu au wanaojitoa dakika za mwisho na kutoa nafasi kwa mgombea wa chama tawala kupita bila kupingwa au kupata upinzani kidogo kwa vyama vidogo vitakavyoweka mgombea. Mifano ipo mingi na ukawa wawe makini sana. Kwani anajuaje kama ukawa walishapanga safu yao? Ina maana akikosa nafasi ya kugombea ataondoka mara moja huyo. Kwanini asipewe muda wa probation kuuona uaminifu na uwezo wake?
 
Hako kajimbo nasikia ukitaka kugombea ubunge shurti ujipange katika suala la kamati ya ufundi...
 

Mapokezi ya Fransico Kimasa Shejamabu (mwenye gwanda) akielekea katika viwanja vya shule ya msingi Pambalu wilayani Sengerema kuhutubia wananchi. (picha zote na Daniel Makaka wa MOblog, Sengerema).

Na Daniel Makaka, Sengerema.Aliyekuwa kada wa wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya Sengerema mkoani Mwanza Bw. Fransico Kimasa Shejamabu ametangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)ambacho amejiunga nacho.

Kauli hiyo ameitoa mjini hapa alipokuwa akiwahutubia maelfu ya wakazi wa wilaya Sengerema waliofika katika viwanja vya shule ya msingi Pambalu.Alisema yeye si mwanachama tena wa CCM na kwamba amekihama chama hicho kutokana na kukosa mvuto kwa kutokana na viongozi wake kuhusishwa na mambo ya kifisadi .

Bw. Shejamabu huku akishangiliwa aliwatangazia wananchi kuwa amekwisha weka nia ya kugombea ubunge jimbo la Sengerema kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hivyo kuwaomba wanasengerema kumuunga mkono yeye na chama chake ili kiwaletee maendeleo jimboni humo.

Mwanachama mmoja wa CHADEMA Bw. James Ndahihya alisema wanamshukuru Mungu kwa kumuelekeza kada huyo wa CCM kujiunga na chama cha ukombozi wa watanzania kwani sasa jimbo la Sengerema limepata mgombea ubunge.Bw. Shejamabu amesema ameingia Chadema kulikomboa jimbo la Sengerema .


njaa ya madaraka inawasumbua haooooo....
 
by ferre.g;
Geita Mkuu


Mkuu ferre.g Mwenyekiti Alphonce Mawazo atagombea jimbo la busanda, Geita wapo akina kamanda Ntinonu, Rogers, Upendo na wengine!
 
Last edited by a moderator:
Hako kajimbo nasikia ukitaka kugombea ubunge shurti ujipange katika suala la kamati ya ufundi...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom