Albedo
JF-Expert Member
- Feb 24, 2008
- 5,559
- 1,452
Daniel Mjema,Moshi
MBUNGE wa Jimbo la Simanjiro,Christopher Ole Sendeka (CCM) amemtetea mgombea Urais wa CCM, Jakaya Kikwete kuwa ni kinara wa vita ya ufisadi.
Alisema rais Kikwete ni kinara wa ufisadi na inavyoelezwa na viongozi wa vyama vya upinzani na kwamba wabunge wa upinzani walidandia hoja ya kashfa ya Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Sendeka alitoa kauli hiyo mjini Moshi jana katika eneo la uwanja wa kuoshea magari linalomilikiwa na Baraza la Wazee wa CCM Mkoa Kilimanjaro, katika mkutano wa kumnadi mgombea Ubunge Jimbo hilo, Justine Salakana.
Mbunge huyo mteule ambaye alikuwa mwiba mkali katika mjadala wa kashfa ya ufuaji umeme ya kampuni ya Richmond, alisema kumnyoshea kidole Kikwete na CCM kuwa hakijashughulikia mafisadi nchini si sahihi hata kidogo.Katika mikutano ya kampeni, baadhi ya wagombea wa upinzani wamekuwa wakimtuhumu Kikwete kwa kutochukua hatua madhubuti za kupambana na rushwa ikiwemo kutowachukulia hatua watuhumiwa muhimu wa ufisadi.
Wagombea hao akiwemo mgombea Urais wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amekuwa akimtuhumu Kikwete kwa kutowakamata wamiliki wa kampuni ya Kagoda iliyochota Sh40 bilioni za EPA na wale wa Deep Green Finance.
Jakaya Kikwete kwa mkono wake mwenyewe alimwandikia barua waziri wa fedha wakati huo Zakhia Meghji akimtaka aanzishe ukaguzi akaunti ya EPA, lakini bahati mbaya wapinzani wakainasa barua ile,alidai Sendeka.
Sendeka alidai kuwa baada ya wabunge wa upinzani kuinasa barua hiyo ndiyo, waliidaka hoja ya ufisadi na kuifanya ni yao kwao.
Kama kweli Kikwete angekuwa hachukii ufisadi angelivunja Baraza la Mawaziri na kukubali mawaziri wake kujiuzulu?, Vita ya ufisadi haikuanzishwa na wabunge wa Chadema wala CUF,alifafanua.
Alitumia mkutano huo uliohudhuriwa na mamia ya wanachama wa CCM na wananchi wa Jimbo hilo, kuwaomba wamchague Salakana na kuwataka kupuuza mbegu za chuki zinazopandikizwa asichaguliwe.
Akimnadi Salakana, Ole Sendeka alisema kama atachaguliwa, atakuwa kiungo muhimu kati yake na Rais wa awamu ya nne ambaye alisema hakuna shaka kwamba atafufua viwanda na kuongeza ajira kwa vijana.
Awali ilielezwa kuwa mkutano huo ungehutubiwa pia na Mgombea Ubunge Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela lakini hata hivyo hakutokea katika mkutano huo na hakuna sababu zozote zilizoelezwa kuhusu jambo hilo.
Source: Mwananchi