Semina Za Ndani.

Mangisandy

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
2,652
2,272
Napenda kusema napendezwa sana na kazi inayofanywa CDM, bungeni na nje ya bunge kupitia mikutano na maandamano. Maandamano na mikutano hii pamoja na ujasiri wanaonesha wabunge wa Chadema bunguni bila kusahau ushindi ktk uchaguzi mdogo Arumeru, ni chachu kubwa kuwafungua watu macho. Utendaji huo wa CDM umefanya watu wengi waone ubutu wa ccm, lakini pia ari ya kufanya mabadiliko.
Lakini mimi naona hayo peke yake halitoshi kufanya mabadili tunayotaka Tz! Nawaomba cdm wafanye semina za ndani, kuandaa wasimamizi/mawakala makini ili 2015 wasiibiwe. Waandaye viongozi ngazi zote kwa kuanza kuwekeza sera zake kwa kutoa mafunzo ya semina fupi fupi nchi nzima. CDM iandae watu wanao weza kuhamasisha, umuhimu wa kujiandikisha, kupiga kura na kuwakataa watu wanaotaka uongozi kwa masilai yao, hasa hawa MAGAMBA. Wengi wamehamasika na wanataka mabadiliko lakini hawajui hayo mabadiliko yatafanyikaje na ata CDM yenyewe hawaijui wala malengo yake.
Mwito wangu kwa Silaa, Mbowe, Lema, Zitto na wengineo, msibaki bungeni au kwenye mikutano na maandamano tuu, toweni elimu ya mnachotaka kufanya. Msilewe ushindi kidogo wa Arumeru au kuvua wachache magamba na kuwavalisha kombati! Kazi ni kubwa, pigeni kazi sana, msilale!
M4C ...
 
Back
Top Bottom