Selasini akanusha uzushi uliosambazwa

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Kuna mhuni kaja hapa atakuwa ni magamba huyu na kusambaza eti baba yake Selasini katutoka ..Selasin mwenyewe kajibu hivi.
[h=6]Pamoja na Shukrani zangu kwa Waheshimiwa Wabunge,Mawaziri,na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana nami leo katika msiba ya marehemu Mama yangu... Nimeshitishwa sana na Uzushi uliosambazwa kwenye mtandao wa Jamii Forums kuwa Mke wangu na Baba yangu Mzazi nao wamefariki!... Kiukweli huu mtandao si tu unapoteza maana ya THE GREAT THINKERS bali unakuwa wa kihuni!..... Ni mtandao gani huu ambao hauwezi kuth


ibitisha taarifa kabla ya kuziandika public?...

Mtandao unaoandika uzushi wa kuzulia wengine vifo visivyokuwepo ni Mtandao wa ajabu!... Binafsi naomba kuwapa pole waliopata taarifa hizi (Wengine wameniandikia Inbox).. Naomba kuwajulisha kuwa Mke wangu na Baba yangu bado wanaendelea na Matibabu... Tuendelee kuwaombea wapone warejee kwenye majukumu yao kama kawaida!...

Nawatakia Usiku Mwema Ndugu zangu, Mungu awabariki.

Joseph Selasini
Mb. Rombo
Chadema.
[/h]
ndio kaiponda JF inawezekana hajui maana ya forums ....
 
mzushi huyu aloleta thread hata mm kanikera sana nilinataka ku'report abuse kwa mods bahati nzuri imeshaondolewa, ila huyu selasini kaniudhi kuiponda JF ilihali hata huko FB angeweza kujitokeza mhuni yeyote na kuanzisha thread kama hiyo, pia nimeshangazwa na yeye kutembelea hapa JF na bado kashindwa kukanusha huo uzushi kwenye thread husika, sijui ana chuki na JF?
 
Mimi najiuliza Invisible aliweza kuleta uzi wa ajali ya mbunge huyo lakini uzushi huu akashindwa kuuthibitisha kwa kuzingatia unyeti wa habari yenyewe.
 
mhe,pole na yote najua taarifa hizi zinaumiza kwani wapenzi wako na hasa wapenzi wa CHADEMA tunakuombea mara kwa mara,hata sie tulipopata taarifa hiizi nilipatwa na huzun mara mbili
Nikija kwa upande wa pili,umeikosea Jamiiforums sana kwa kauli kama hiyo kama itakua ni kweli bas utabidi uwatake radhi.Najua wewe ni mwingoni mwa viongozi makini naamini unatambua uwanja kama huu ni mpana kila mtu ana uhuru wa kutoa taarifa lakin mara tu ikizibitika si kweli hatua kali huwa zinachukuliwa,pia kumbuka mtandao huu huu ndio ulikua wa kwanza kutuhabarisha juu ya matatizo yaliokupata.Naomba uendelee kupuuza na kujitokeza haraka kukemea hoja za kizush za hawa magamba.Mungu akutie nguvu
 
Selasini acha mambo ya kikuda..ingawa umefiwa..ulishindwa nini kukanusha hii habari hapa hapa..acha umamluki..jf ni user generated forums!!!
 
Mh Selasini kwanza nikupe pole kwa Ajali na kwa matukio mengine yote yaliyotokana na ajali husika. Nimesikitishwa tu ni jinsi gani mtu mwenye upeo kama wako unavyoshindwa kuelewa maana ya forum. Maneno hayo ungekuwa umemshushia wenye blog kidogo ningekuelewa lakini sio kwa Forum kama hii ambayo more than 90% are Anonymous IDs and are free to post anything. hiyo ndio maana ya dare to speak openly. Ulichotakiwa kufanya ni kukanusha taarifa hizo na kuweka taarifa sahihi na si kutukejeli maana hadi umejua hiyo habari ilikuwa humu JF haikosi hata wewe ni member au you regularly popin. Mwisho nakukaribisha sana JF kama walivyo wanasiasa wenzio akina Zitto,JJ Mnyika, Dr Slaa etc. Ujue tu hapa hakifichwi kitu. Na taarifa ikigundulika ni ya udaku itawekwa inakopaswa la itaondolewa.
 
mkuu Ruhazwe umenena vema....kukujulisha tu kamanda wetu Selasini...kuna tofauti ya blog na forum....zaidi ya yote....niwatakie wagonjwa afya njema.....
 
kuna haja ya JF kuwa na editorial board ambao watahakiki uhalisia wa sensitive information kabla ya kuziruhusu kuwa published hapa
la sivo kila mtu atakurupuka na kuandika anavojisikia, si ajabu lengo lao ni kkuharubu sifa ya JF.
majukwaa haya ya SIASA na habari mchanganyiko yawe na hizo taratibu na zitekelezwe.
 
Tushukuru mungu sana tena sana kwamba watajwa wako hai na wanaendelea na matibabu.

Hata hivyo MODs naomba mtusaidie kulinda heshma ya hili jukwaa. Walau toeni statement moja ili ikumbushe kila mtumiaji wa hili jukwaa kwamba wanatakiwa wazingatie nini. Najua kuna rules somewhere lakini issue statement then tuendelee.
Lakini ebu kuweni wakali kidogo.
 
Mtamlaumu Selasini, lakini makosa ya kwetu. Msiba hauuliziwi hadharani, ukifanya hivyo ni sawa na kuutangaza. Ni mbaya saidi kama haupo.
 
kuna haja ya JF kuwa na editorial board ambao watahakiki uhalisia wa sensitive information kabla ya kuziruhusu kuwa published hapa
la sivo kila mtu atakurupuka na kuandika anavojisikia, si ajabu lengo lao ni kkuharubu sifa ya JF.
majukwaa haya ya SIASA na habari mchanganyiko yawe na hizo taratibu na zitekelezwe.

Mkuu naona unaongeza gharama zisizo na msingi wewe member 10's thousands utawaocontrol vipi, pia utaondoa ile nadharia ya real-time, nafikili kuna haja ya member kufahamishwa matumizi ya kitufe "report abuse" si tu kwa maneno machafu hata kwa taarifa nyeti zitakapopostiwa ili ziweze kuthibitishwa, kwa kutumia mtindo huu ni sisi member ndio tutarahisisha zoezi kuliko wao kupitia kila post kabla ya kuiruhusu.
 
Nitawashangaa mods kama Asango hajapigwa ban kwa habari za uzushi.
Kupigwa ban pia haitoshi, inatakiwa mtu afutwe usajili kabisa, ama kupigwa faini.
 
wewe selasini acha ukuda. hii ni forum sio blog. na zinapostiwa habari tofauti hata wewe ukiwa mod huwezi kuzimonitor kwa wakati mmoja. ndo maana iliondolewa baada ya kuonekana. Ungemkashifu huyo mbaya wako aliye leta habari za uongo sio mtandao wetu pendwa. hata hivyo mtu kufa kitu cha kawaida japo kinatisha. pole kwa machungu uliyo kumbana nayo. wanajf sio malaika.
 
Aksante Mh Selasini na wewe kwa kuona mapungufu yaliyoanza kujitokeza ndani JF, Kwa mtu mtu na ambaye si mnafiki anauona ukweli kwamba JF imeanza kupoteza maana yake na kama hao wanaojiita Mode hawataacha kulala basi yatatimia.
 
Aliyeleta uzushi huo bila kuwa na hakika hata mimi namlaumu sana, kuna habari za uzushi ambazo zinaweza kuvumilika lakini sio hili la kifo LAKINI tukija kwa ndugu yetu selasini hapa naye amechemka kukandya JF labda kama hana uelewa mzuri kuhusu forums! ilitakiwa aje na habari ya kukanusha halafu wengine tungeendelea kumlaani huyo mzushi.
Humu ndani ya jf,CHADEMA, CCM, watu binafsi makampuni n.k huwa wanazushiwa mambo mbalimbali lakini huwa wanajitokeza wahusika, makada, mashabiki, wajuvi n.k ili kukanusha uzushi huo na maisha yanaendelea! POLE SANA MHESHIMIWA hizi ndo forums inabidi u-cope nazo!
 
Jamaa kaamua kuzushia wenzake vifo kasahau kuwa na yeye ni marehemu mtarajiwa...pole sana Mbunge Selasini, huyu ni muhuni tu alioleta huu ujinga hana uhusiano wowote na JF...usirudie tena kuponda JF wape pole wagonjwa.
 
Selasini pole kwa matatizo mkuu wangu.
Lakini umewezaje kupata habari ya uzushi toka jf na kwenda kuikanusha kwenye mtandao wa kipumbavu wa fb?
Kwanini usiwe registered humu jf ili upate up date na sie tukapata up date?
For your information, and to be honest hii habari ingepostiwa jf isingefutwa au kuondolewa. Ili ujue huu ni mtandao wa great thinkers umeona habari yenyewe ishaondolewa humu.
Acha kula chabo mtu mzima jiunge jf ufaidi uhondo!
 
Back
Top Bottom