Selasini akanusha uzushi uliosambazwa

Mmmh hili tatizo la habari za uzushi linahitaji kutazamwa upya, huku kwetu nikiwapa. Taarifa za mtandaoni huwa wanauliza source nikitamka ni jf basi nakuwa nimekata kiu yao sasa naanza kupata woga baada ya viwavi kuvamia jamvini. TAFADHALI MODS SHUGHULIKIENI HILI JAMBO
 
Nafikili kuna haja ya kubadilisha mifumo ya kujisajili ili kuidentify watu na hatua za kisheria ziwe zinachukuliwa kwa watu wanaosambaza uzushi kama huu.

Pole sana mh.

Mbona wote tunafahamika, labda kama kuna mtu hatumii kabisa facebook kwenye computer anayotumia kwa JF
 
Jamaa kaamua kuzushia wenzake vifo kasahau kuwa na yeye ni marehemu mtarajiwa...pole sana Mbunge Selasini, huyu ni muhuni tu alioleta huu ujinga hana uhusiano wowote na JF...usirudie tena kuponda JF wape pole wagonjwa.

aiseeeeeeeee kumbe na wewe mida mingine huwa unaongea baada ya kufikiri eeeehhh,off course umenikosha gamba........
 
pole selasini lakini tokea uungane na shibuda kudai nyongeza ya posho nilipoteza imani na wewe..ugua pole
 
Poleni sana Mh na ndugu zako , kwa pamoja tunatoa salaam nyingi za pole, lakini kumbukeni mtandao huu na chama chako humu ndani kuna watu hawahaupendwi kabisa na inawezekana kabisa wakatuni nafasi hii kufanya lolote juu yako, chukulia ni sehemu ya maisha
 
Huwezi kuthibitisha kila kinachoandikwa ni kazi ngumu mnoo. Kama kukiwa na uzuri ni bora watu wafanye kama alivyofanya mheshimiwa kukanusha halafu tunasonga mbele.
 
From great thinkers to great lossers...enyi mnaojiita ma mode jf itawafia mikononi mwenu..hata huyu mwenzenu anawalalamikia...!!!!

Mkuu lady cassandra nadhani tatizo siyo MODS tatizo ni sisi watumiaji wa mtandao. Mtu unaweza kuanzisha thread na kuitupa hewani sidhani kwamba hiyo thread/post yako inakuwa verified kwanza na MODS kabla ya kwenda hewani. Nadhani MODS wanaziona post/thread baadaye. Wanajitahidi sana kuzifuta thread ambazo hazina mashiko. Inabidi sisi watumiaji wa huu mtandao tuwe responsible tusianzishe mambo ya kizushi bila kuwa na uhakika. Kama ni kufa kwa mtandao ni sisi tutakaouua na si MODS.

Kwa MODS tafadhali chukue hatua kali sana kwa watu kama huyo aliyeleta habari za kizushi na wengine wenye matusi. Ni afadhali JF ikabaki na wanachama wachache kuliko lundo la watu wanaoihujumu JF kwa kuleta thread za hovyo.
 
Last edited by a moderator:
kuna mhuni kaja hapa atakuwa ni magamba huyu na kusambaza eti baba yake selasini katutoka ..selasin mwenyewe kajibu hivi.

Ndio kaiponda jf inawezekana hajui maana ya forums ....
mheshimiwa 30 tutake radhi kabisa wana jamii forum maana -jamii forum sio inayopost vitu ila ni mtu binafsi so usitudharaulishie mtandao wetu .laumu mtu binafsi.kingine pole kwa maswahibu yaliyokukuta na pia nashukuru kujua huwa unapita pita humu jamii forums najua utakua ulikaona kale kapost kakukunyang'anya jimbo 2015,fanyia kazi wananchi wa rombo wamekuchoka usituangushe wana cdm.wewe utakuwa ni mbunge wa kwanza kutuangusha natutanukuu kuwa wewe ni mj......a wa millenium.
 
Huwezi kuthibitisha kila kinachoandikwa ni kazi ngumu mnoo. Kama kukiwa na uzuri ni bora watu wafanye kama alivyofanya mheshimiwa kukanusha halafu tunasonga mbele.
Unafikiria ni watu wote hawana kazi za kufanya ili wawepo hapa masaa 24 kukanusha tetesi wanazozushiwa? Hili suala la kudhibiti thread za uzushi kama hizi ni suala la members wote wakiongozwa na JF moderators. Inabidi uongozi wa JF uwe mkali na uchukue hatua kwa member yeyote atakayeleta habari za uzushi kama hizi. Wa-rectify rules na ikibidi wa-expose identity za members wanaochafua hali ya hewa kwenye hii forum ili wachukuliwe hatua.
 
Selasini

Sikujua kama upeo wako wa Kufikiri unaishia kwenye hiyo Pua yako.

Naomba ujue kuwa Jamii forum ni tofauti na facebook na hivyo unatakiwa kufikiri mbele zaidi ya pua yako kutambua hili.

Inaonekana ww si member wa Jamii Forum, ungelikuwa member ungepata updates zoote na si kukurupuka na kuanza kuukashifu

Siku zote kabdla ya kuongeza dhibitisha kwanza uwe na uhakika
 
kuna haja ya JF kuwa na editorial board ambao watahakiki uhalisia wa sensitive information kabla ya kuziruhusu kuwa published hapa
la sivo kila mtu atakurupuka na kuandika anavojisikia, si ajabu lengo lao ni kkuharubu sifa ya JF.
majukwaa haya ya SIASA na habari mchanganyiko yawe na hizo taratibu na zitekelezwe.

Nadhani kuna kitu cha namna hiyo hapa Jukwaa la siasa. Hili ndilo jukwaa lenye mods wengi kuliko lolote lile, sasa nashangaa habari nzito kama hiyo ilipitaje bila kukaguliwa uhalisia wake na mods. Lakini pia sisi wachangiaji tuna wajibu wa kuripoti habari ambayo tunaona inashusha hadhi ya jukwaa!
 
Ila mwanadamu kukosea ni sehemu ya maisha yake na wala mtu alaumiwi na kuonekana ana upeo mdogo kwakufanya kosa la kwanza. Naomba tumuone 30 katukosea maana kama anajua muundo wa forum asingeandika alivyoandika, pili aliyempa taarifa angemmalizia kuwa linalofanyika na jinsi yakumaliza sidhani kama angefunguka hivi.

Pia 30 aelewe hapa JF tukiamua kuweka CV zetu asingeweza kufungua maneno anayofungua huko fb, na aelewe akichafuliwa JF ni kwamba amechafuliwa mpaka mbinguni maana huku kuna kuanzia mesenja wa ofisini kwetu mpaka rais wake wa sasa JK na wa 2015 W.Slaa, zaidi wako mawaziri wasasa na wale wa 2015. Aelewe tupo wenye fani mbalimbali kuanzia secretary wake, injinia,daktari, wanasheria na ambao anawafikiria kwa ubongo wake, hivyo aje huku apate changamoto yakutosha aachane na fb ya ndio mzee huku wanakung'ong'a.

Sina la kumsema namuheshimu na nampa pole kwa yaliyomkuta na aelewe jambo kama hili laweza kutokea kwa yeyote, ni bora akajifuza kwa viongozi wake ambao wanasemwa vibaya na wanamjibu huyo mtu personaly. Kosa ni moja likirudiwa ndo tumuhukumu kwa kiasi chake.

Aelewe fb anayoona inampa nguvu ni wanafiki maana mtu anayekujua hawezi kukueleza ukweli, aje aungane na ma-ID fake ndo ajijue watu wanamuonaje
 
wewe selasini acha ukuda. hii ni forum sio blog. na zinapostiwa habari tofauti hata wewe ukiwa mod huwezi kuzimonitor kwa wakati mmoja. ndo maana iliondolewa baada ya kuonekana. Ungemkashifu huyo mbaya wako aliye leta habari za uongo sio mtandao wetu pendwa. hata hivyo mtu kufa kitu cha kawaida japo kinatisha. pole kwa machungu uliyo kumbana nayo. wanajf sio malaika.

Dubu taratibu....Huyu jamaa yupo kwenye wakati mgumu sana.....Hebu assume kuwa ni wewe.....anahitaji tu kuelimishwa kama wengine wanavyofanya na pia kuombwa radhi kwa sababu amekosewa haki... Ni kweli amekosea kuiponda JF lakini hatuwezi kumrekebisha kwa kumtusi ilihali psychologically tunajua yupo kwenye wakati mgumu..
 
Nafikili kuna haja ya kubadilisha mifumo ya kujisajili ili kuidentify watu na hatua za kisheria ziwe zinachukuliwa kwa watu wanaosambaza uzushi kama huu.

Pole sana mh.

Mkuu rejea maudhui ya kitu kinachoitwa "forums" katika ulimwengu wa communication ndipo ama umuunge mkono Selasini au lah!
 
kwa matatizo yaliyompata ndugu yetu Mh. Selasin MP-hanabudi kusamehewa bure kwakweli; naona wengi mmemshupalia mkimtaka awatake radhi wana JF kwa maneno aliyoyatoa. sina shaka naye mwache kwanza atulize roho yake nina imani yuko makini tutaenda naye sawa tu:
Pole sana Mh. Selasini tuko pamoja
 
Back
Top Bottom