Sekretarieti ya Ajira iache kutesa wadogo zetu wanaotafuta ajira

T-pain

Member
Nov 13, 2023
89
115
Rais ongea na Waziri mwenye dhamana ya ajira aongee na hawa secretariet ya ajira waache kutesa wadogo zetu.

Kama uzi unavyosema hapo juu mheshimiwa Rais. Kuna hawa watu wanaoendesha utaratibu mzima wa kutoa ajira kwa vijana wa Tanzania (secretariat ya ajira), hawa wamekuwa tatizo kwa vijana wanaojitafuta kwenye sekta ya ajira.

Haiwezekani mtu afanye usahili halafu akae zaidi ya miezi sita wakati mwingine zaidi ya mwaka bila kujua matokeo kama kafulu, kafeli au yupo kwenye kanzi data.

Mtu kama kafeli aambiwe tu not selected for job kama kwenye aptitude test wanazofanya mtu ajue atafanya nini.

Unakuta kijana yeye kila siku ni kuingia kwenye mtandao mpaka anamaliza mwaka kuangalia matokeo halafu matokeo yenyewe wanatoa wanavyojiskia wenyewe, yaani mtu akikosa jina lake itabidi asubiri mpaka mwezi wakati sahili zinafanywa kila siku na matangazo yanatolewa kila siku.

Waache kupotezea madogo muda na gharama.
 
Back
Top Bottom