Rais Samia ongea na Waziri wa Ajira aongee na Sekretarieti ya ajira waache kutesa wadogo zetu

T-pain

Member
Nov 13, 2023
89
115
Kama uzi unavyosema hapo juu,

Rais Samia, kuna hawa watu wanaoendesha utaratibu mzima wa kutoa ajira kwa vijana wa Tanzania (secretariat ya ajira), hawa wamekuwa tatizo kwa vijana wanaojitafuta kwenye Secta ya Ajira.

Haiwezekani mtu afanye usahili alafu akae zaidi ya miezi sita wakati mwingine zaidi ya mwaka bila kujua matokeo kama kafulu,kafeli au yupo kwenye kanzi data.

Mtu kama kafeli aambiwe tu not selected for job kama kwenye aptitude test wanazofanya mtu ajue atafanya nini.

unakuta kijana yeye kila siku ni kuingia kwenye mtandao mpaka anamaliza mwaka kuangalia matokeo halafu matokeo yenyewe wanatoa wanavyojiskia wenyewe, yaani mtu akikosa jina lake itabidi asubiri mpaka mwezi wakati sahili zinzfanywa kila siku na matangazo yanatolewa kila siku Wakome.
 
Hii kweli aise nilifanya oral Tutorial assistant toka march mpaka leo hii kimya
wanatesa watu tu.mie kuna angu kafanya usaili mwaka sasa unaelekea hamna jibu lolote chaajabu kila siku anaitwa kwenye saili nyingine tunapoteza pesa tu..
 
Wakati mwingine unaweza kuwalaumu hao secretariat ya ajira kumbe tatizo lipo kwenye ufinyu wa bajeti kwa Idara/taasisi husika.

Maana wao Secretariat ya Ajira wanaendesha mchakato wa ajira kwa niaba.
 
Wakati mwingine siasa ina nguvu kuliko uhalisia, huwa wanafanya maigizo kuwa Serikali imetoa ajira kadha wa kadha ili Rais aonekane ana jali

Sababu tumeiweka siasa mbele kuliko uhalisia. Na siasa ndio inatumika kuwapamba wanasiasa wkt uhalisia sio

moja ya mahitaji ya watanzania ilikuwa siasa safi back in the day. In this modern era we dont need that
 
".........Suluhisho lishapatikana taasisi zishaanza kuajiri zenyewe, TRA wameanza sasa subirini kuitwa kwenye usaili wa NSSF"

Punguzeni kuwalaumu PSRS.
waifute tu iyo system kama wameshindwa kulifanyia kazi ilo alfu ajira zote ziwe zinatagazwa na mashirika kwa uwazi watu waanze kuapply ikiwezekana na kutembea na mahasha kabisa..
 
Kama uzi unavyosema hapo juu,

Rais Samia, kuna hawa watu wanaoendesha utaratibu mzima wa kutoa ajira kwa vijana wa Tanzania (secretariat ya ajira), hawa wamekuwa tatizo kwa vijana wanaojitafuta kwenye Secta ya Ajira.

Haiwezekani mtu afanye usahili alafu akae zaidi ya miezi sita wakati mwingine zaidi ya mwaka bila kujua matokeo kama kafulu,kafeli au yupo kwenye kanzi data.

Mtu kama kafeli aambiwe tu not selected for job kama kwenye aptitude test wanazofanya mtu ajue atafanya nini.

unakuta kijana yeye kila siku ni kuingia kwenye mtandao mpaka anamaliza mwaka kuangalia matokeo halafu matokeo yenyewe wanatoa wanavyojiskia wenyewe, yaani mtu akikosa jina lake itabidi asubiri mpaka mwezi wakati sahili zinzfanywa kila siku na matangazo yanatolewa kila siku Wakome.
Zamani ilikuwa tunalalmika kwa wakuu wa idara.

Baadaye ikaja tunalalamika kwa Katibu Mkuu wa Wizara

Baadaye Mawaziri wakachukua ujiko wa malalamiko

Waziri Mkuu akageuka mkombozi

Sasa tunapeleka kila lakamiko kwa Rais.

Kesho tujipange namna ya kuwasilisha malalamiko ya changamoto zetu kwa Mungu

Sisi tunageuzwa wajinga sana na hii CCM na viongozi wake
 
Sababu tumeiweka siasa mbele kuliko uhalisia. Na siasa ndio inatumika kuwapamba wanasiasa wkt uhalisia sio

moja ya mahitaji ya watanzania ilikuwa siasa safi back in the day. In this modern era we dont need that
Kuna mtu mmoja baada ya kuteuliwa kushika nafasi ya Kisiasa aliniambia njia sahihi ya yeye kuendelea kwenye ile nafasi ni kumsifu Mama hata akifanya jambo la kawaida.

Wameanzisha Umoja wao, yaani kila Mama akifanya chochote basi utaona wana-repost kwenye mitandao yao ya kijamii.

Uchawa pro-max 🙌
 
Uchawa pro-max

Ndio hali halisi kusifu tu. Huo muda wa ku deal na matatizo halisi ya mtanzania wataupata wapi? Something is wrong kwakweli
 
Back
Top Bottom