Nurdin moh'd
JF-Expert Member
- Nov 1, 2012
- 367
- 70
Waelimishe hao vichogo,bishara zao huku z'br ni sumu ya panya,mende,kunguni,viroboto,ukahaba,madanguro,ujambazi,watuache tupumueeee!Nguruvi3, ukitaka utumie akili yako vizuri katika kuangalia mambo na kujenga hoja, basi kwanza jaribu kuondoa chuki kwa hilo jambo husika! Ukijenga hoja zako kwenye misingi ya chuki tu kama ulivyofanya hapo juu, basi unasababisha watu waone the other side of you (Ujinga na upuuzi wako)!
Sasa nianze kuku elimisha kidogo! CDM hawakuwahi kuwa na sera ya serkali 3, hata ukikataa mpaka kesho, sera ya CDM ni majimbo, wakimaanisha nchi nzima (Tannganyika na Zanzibar) kutakuwa na serkali za majimbo na hizo serkali za majimbo zitakuwa chini ya central goverment (serkali kuu), ingawa hawakuweka wazi, kama Zanzibar itakuwa jimbo moja au 2 au 3, lakini haiwi nchi tena!
Hii sera ya serkali 3, imeibuka hivi karibuni, wala sio sera rasmi ya CDM! Bado wapo wahafidhina (kama Nassari) wanaokereketwa na ukabila na umajimbo wanaodai ARUSHA iwe nchi (ijitenge)!
CUF wao sera ya serkali 3 wameona haifai tena kwa mazingira ya sasa, sababu wameshaona kwamba kamwe uwepo wa serkali 3 hautakidhi matarajio na mipango ya Zanzibar katika kujikwamua kiuchumi na kisiasa! Hawaamini juu ya ushirika usio na mkataba na Tanganyika!
Naomba ukajifunze tofauti ya Muungano wa katiba na Muungano wa mkataba! Huu uliopo sasa ni muungano wa katiba! Wanaoudai CUF na Wazanzibar walio wengi ni Muungano wa mkataba!
Wazanzibar hawana hofu ya kuvunjika kwa Muungano, kama wewe unavyoona Tanganyika haifaidiki na muungano,ingawa unang'ang'ania huu muungano (hujawahi kudai kuuvunja muungano), basi wazanzibar ndo kabisa, hawaoni faida hata moja ya kuwepo huu muungano!
Eti wazanzibar wamejaa tele Tanganyika,muungano ukivunjika watarudi kwao! Ebo hoja ya kijinga kabisa! Kwani hao wachina walojaa tele hapo Tangayika, mpaka wengine wanajiuza usiku..achilia mbali wahindi waliofikia mpaka kuwahamisha kwenye nyumba zenu za serkali NHC, jee hao wapo hapo Tanganyika kwa sababu ya Muungano wa Tanganyika na China au Tangyika na India? Hivi wale waZanzibar walojaa tele pale London, Ottawa (Canada), Stockholm (Sweden), Burundi,Oman, USA, name it...jee nchi hizo zimeungana na ZANZIBAR?
Kama mnaardhi ya kuwapa waZANZIBAR bure, kwanini msiwape bure wale watanganyika wenzenu wanaouwana kwa mapanga huko bara kupigania ardhi? Eti bure, bure?! Wazanzibar waliopo hapo Tanganyika ndio wanaofanya nyinyi wafanyakazi wa serkali msiozalisha kitu zaidi ya ufisadi mupate mishahara yenu! Kupitia biashara zao halali, maduka na dalala , hoteli, viwanda,migahawa n.k, wanalipa kodi TRA, nyinyi mnapata mishahara yenu! Ukimuona mZanzibar mshukuru badala ya kuleta kiburi chako cha kipumbavu!
Dhahabu yenu mmehonga kwa wazungu wa Canada, Almasi mmegawa kwa makaburu afrika kusini, mbuga za wanyama mnauza vifaru, tembo na meno yake kwa wachina na waarabu, mlima kilimanjaro unaingiza mapato Kenya nyinyi mnaishia kuuangalia tu,gesi ya songo songo ufisadi mtupu....hakuna mnachopata kutoka katika mali ghafi zenu...maisha yenu yanategemea kodi za Wazanzibar ((Bakhresa et al), wahindi, na wachina! Hamna jeuri ya kuwafukuza waZanzibar, mtakufa njaa! K.koo itageuka sehemu ya wakabaji,wala unga na wauza uchi! Na hilo ndilo mnaloliogopa kuuvunja muungano! Mnaogopa waZanzibar watapata fursa kuendesha biashara kwao....! Lakini nikufahamishe tu, ukivunjika muungano wazanzibar wataishi na kufanya biashara Tanganyika kama wafanyavyo hivi sasa, huko Kenya, China, Msumbiji n.k!
Halafu unasema Zanzibar nje ya muungano itakuwa dhiki sana...we unaelimu ya unajimu (utabiri) kama marehemu Sheikh Yahaya eeh...?! Basi kama hufahamu, Zanzibar ilishawahi kuepo kabla ya Tangayika, tena ilikuwa ni nchi yenye maendeleo kuliko hata baadhi ya nchi za Ulaya na Mashariki ya mbali! Kwa mfano tu katika nchi za E.A Zanzibar ndo nchi ya kwanza kuwa na umeme, wakati huo Tangyika haipo (inaitwa mzizima)! Imeanza kuwa na TV ya rangi kabla ya hata Israel!, achilia mbali Tangyika iloanza kuona TV 1990!
Tayari au niendelee...