Seif Tumekusikia; Sasa jiuzulu na iondoe CUF kwenye SUK!

Muungano wa nini?
  • Wana bendera yao
  • Wana Rais wao
  • Wana wimbo wa taifa lao
  • Tulivyo mazezeta tunadhani ni ule muungano wa mwanzo!
  • Mbunge anawakilisha kama watu 150 tu wakati bara mbunge anawakilisha maeru ya watu
  • Wazanzibar wanasomeshwa bure na pesa ya muungano wakati wa bara mnapewa kama mkopo
  • Hivi tumelogwa?
Nawashauri vunjeni muungano waache kula vya muungano bure

haya. Jussa-chogo. Hongera
 
Hakika Mzee Mwanakijiji huyo unae mpa ushauri alishajiingiza kwenye ndoa ambayo hawezi kuivunja na bado ana penda ndoa yake!
 
Last edited by a moderator:
Seif unaweza kumlinganisha na mlinzi aliyejifunga mwenyewe goli, tena kwa kisigino, katika harakati za kuokoa. Mashabiki itabidi wamzomee sasa. Lakini zaidi wachezaji wenzake inabidi wamlaumu. Timu tayari iko nyuma kwa goli moja, ingawa mchezo unaendelea-kila la kheir kwa timu ya gnu.
 
jussa na seif ni wanafini. wazanzibar wamezoea kubebwa ndio maana wanapiga kelele tu ili watanganyika wawaamulie kuvunja muungano.vunjeni wazanzibar cha moto mtakiona kwani ufa kwenu upo isipokuwa muungano unawalinda. mshukuruni nyerere na karume waliona mbali
 
seif na jussa ndio walioua cuf ikakosa nguvu kwa uroho wa madaraka
 
Tulipata kumsikia Seif Sharrif Hamad akidai Zenj ijitenge na iwe taifa kamili, huru na kiti chake katika Umoja wa Mataifa.

Wakati nchi za Afrika Mashariki za Tz, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi zinaungana na kutaka kuwa Shirikisho kubwa lenye watu zaidi ya 150 milioni na soko linalovutia mitaji na miradi ya kiuchumi mikubwa, kuna "viongozi" wa aina hii miongoni mwetu. Watatukwamisha hawa!!!!!!

Vinchi vidogo vitaweza kupiga hatua za kimaendeleo kwa nadra sana. Hata viongozi wao wakitaka kuchangia miswada kule U.N., wajumbe wengine ndio wanapata nafasi ya kutoka nje kunywa kahawa, na wengine huvua vinasa sauti vyao na kuendelea kutayarisha hotuba za michango yao.

Mwakilishi wa China, Urusi, America au Brazil akinyoosha mkono kutaka kuchangia, ukumbi unakuwa kimya kumsikiliza. Wale waliotoka nje wanarudi. Seif aelewe hivyo.

Kwa bahati nzuri viongozi wetu wa sasa wanaona mbali . Sio tu tuwe na umoja na ushirikiano wa kisiasa na kiuchumi, bali tukaribishe nchi jirani tuwe muungano mkubwa zaidi.

Waasisi wa nchi zetu walitaka hata Umoja wa Afrika . Mwenyezi Mungu alaze roho zao mahala pema peponi.
 
[/CENTER]

1) SUK imo katika ilani ya CUF 2010 - 2015. Kwa hiyo Seif kuendelea kuwemo kwenye serikali ni kutekeleza ilani ya chama chake

2) Harakati za sasa ni za kisiasa zaidi ndio maana wazo lako la viongozi kujiuzulu halaina mantiki

3) Unawashauri vipi CHADEMA na vyama vingine wanaotaka serikali tatu pia? Watoke kwenye bunge la Jamhuri na wawavue madaraka viongozi wote wa CDM Zanzibar kwenye nafasi zao?

mfumo wa serikali tatu, sasa ni wenye waumini kote. Kuna serkali tatu(ndani ya moja) kuelekea moja. Kuna serikali tatu kuelekea kwenye Muungano wa Mkataba. Na kuna serikali tatu kuelekea kwenye shirikisho la majimbo. Ukiangalia manung'uniko ya jamaa zangu kule wengi wao ni wale wanaopigia chapuo.tatu (ndani ya moja) kuelekea kwenye moja.
 
Tanganyika lilikufa jina tu lakini imo ndani ya Tanzania. Zanzibar lipo jina lakini yenyewe haipo. Ndio maana ya kutafuta ni Zanzibar tu.

nawe Wacha ubishi. Sasa si ndiyo manake tunambiwa ileze j tume nini unataka kiingie katika katiba kuimarisha uwepo wa zanzibar ndani ya Muungano. Wewe unataka kuvunja huo muungano na kuanza kusaka mikataba ya nini sasa?
 
Tanganyika lilikufa jina tu lakini imo ndani ya Tanzania. Zanzibar lipo jina lakini yenyewe haipo. Ndio maana ya kutafuta ni Zanzibar tu.

nawe Wacha ubishi. Sasa si ndiyo manake tunambiwa ileze j tume nini unataka kiingie katika katiba kuimarisha uwepo wa zanzibar ndani ya Muungano. Wewe unataka kuvunja huo muungano na kuanza kusaka mikataba ya nini sasa?
 
hoja ya Maalim Seif kujiuzulu haina mashiko maana hakuna uhusiano wa nafasi yake kama makamu wa rais na maoni yake juu ya Muungano! kumbuka msingi wa kuunda SUK ilikuwa ni kuondoa tofauti za kijamii katika jamii yote ya wazanzibar lakini haikuwa na maana kuwa CUF wanaachana na sera na itikadi yao na kuwa sehemu ya CCM! na pia kumbukeni ndani ya CCM yenyewe kuna wanachama wengi tu ambao ni waumini wa Muungano wa Mkataba mifano michache ni Amani Karume, Shemhuna, Salmini hata Shein mwenyewe ni ule uoga wake tu wakuogopa kivuli cha CCM maana anafikiri akisema wazi wazi juu ya imani yake kwa muungano wa mkataba yapampata yaliyompata mzee Jumbe wakati ule wa Nyerere! amini Usiamini Muungano wa mkataba ndio msimamo wa wazanzibar walio wengi!
 
Kati ya wanasiasa wanafiki ulimwenguni ni Seif, yeye anafanyakazi kwenye imani hii lakini anaamini imani nyingine. Kukosa reasoning ya kutosha kwa watu wetu kunawafanya wachezewe na wanasiasa
 
Mzee Mwanakijiji, mara nyingi unapotoa hoja kuhusu Zanzibar na uhuru wake, basi hoja zako zinakuwa zakitoto kupita maelezo. Inafikia wakati unajiuliza, hivi huyu anaejenga hoja hii ndie yule yule Mzee Mwanakijiji nnae soma makala zake? Hivi ndie huyu mchambuzi wa mambo ya siasa? Mbona kwenye hoja hii ana "reason" kama mtoto wa darasa la 2?!

Ila kiukweli ushabiki na chuki humfanya mtu akapoteza uwezo wake wa ku "reason" na kujenga hoja! Ushabiki na chuki humfanya mtu, nyekundu akaiona nyeupe! Ushabiki na chuki humfanya mtu akawa kipofu, kiziwi na bubu! Kwa sababu hizo sishangai unapojenga hoja ya kipuuzi kama hii.

Just ni ku "conscioutize" kuhusu mapambano katika siasa! Unaweza kupambana ukiwa nje ya system au ukiwa ndani ya system, kinacho matter ni kujipambanua nini unapigania na kwanini na kwa faida ya nani. Sababu kuwa kwenye system hakukufanyi uwe zombie (Karume anawaita SAMAKI),bado unatakiwa uwe na uhuru wa kufikiri, kuhoji na kushauri! Uhuru wa kuseme kile unachokiamini kwa mustakabali mwema wa Taifa na watu wake.

Maalim Seif ameshapambana akiwa njen ya system, aliweka wazi wazi (sera ya CUF) uwepo wa serkali tatu! Lakini sera lazima iakisi mahitaji ya kisiasa, kiuchumi na kijjografia ya wakati husika, hivi sasa sera hiyo ya serkali tatu kwa mtazamo wa CUF haikizi tena matakwa, inayofaa ni MKATABA, anapambana akiwa ndani ya system!

CUF hivi sasa ni mshiriki mwenza katika serkali ya kitaifa, iliyoundwa kwa matakwa ya Wazanzibar (hili unalijuwa, japo wajipa upofu), wazanzibar walioamuwa kwa njia ya kidemokrasia kupitia kura ya maoni, wazanzibar hao walijuwa fika kwamba sera za CUF zina tofautiana na CCM, hivyo basi walijuwa wazi kwamba misimamo ya Maalim Seif kwa baadhi ya mambo katika serkali hii itakuwa tofauti na ile ya CCM! Pamoja na kujuwa yote hayo, kwa ridhaa yao waliamuwa iwepo serkali hii ya kitaifa! Hivyo unaposema eti Seif atoke madarakani kwanza ndio adai Zanzibar huru, hapo unachemka, Seif hayupo madarakani kwa kupenda yeye tu, yupo kwa maamuzi ya Wazanzibar 64%, kujiondoa kwenye serkali hii ni kinyume na katiba ya Zanzibar, nikuwasaliti Wazanzibar! Lakini pia kuepo kwenye serkali hii hakumzuii kudai au kuendesha harakai zake za kudai Zanzibar huru!Hiyo ndo sera chama chake, na serkali hii ya kitaifa haizuii sera za vyama kutangazwa, na makubaliona ni sera ya chama chenye rais ndio itakayo fuatwa, lakini raisi akipenda ile sera anayoona nzuri ya mwenza wake ataichukuwa na kuifanyia kazi!

Mapambano ya siasa ya kudai haki yaweza kufanywa ukiwa ndani au nje ya system, kuwa ndani ya system hakuzuii wala kukuondoalea uhalali wa kudai unayoyaona yanafaa, ni juu ya mpambanaji ndo ataona akiwa wapi atafanikiwa, nje au ndani? Maalima ameona akiwa ndani atafanakiwa kwa haraka. Matunda unayona, anatangaza sera ya Zanzibar huru huku analindwa, na ving'ora anapigiwa! Angekuwa nje ya system, thubutu! pengine asingekuwa hai! Mapambano yanataka strategies kutokana wakati, adui, na mazingira! Hakuna njia moja ya kupambana, wala hakuna silaha moja ya kupambana! Kwa hiyo usilazimishe njia yako ya kupambana ukiwa nje ya system ndio njia pekee ya halali au bora (huo ni utoto na upuuzi)!

Mwanakijiji, labda punguza ushabiki (uumini wa wako juu ya Nyerere na yote aloyafanya) na upunguze chuki juu ya Wazanzibar wanaodai haki yao ya kujitawala, kwakufanya hivyo utaweza kufikiri kwa akili yako ya kawaida na utaweza kujenga hoja zenye mantiki, sio upuuzi huu uloweka hapa!

Ahsante
 
To be honest naipenda Zanzibar iwe huru wawe na uhuru wao kamili wajiamulie mambo yao wenyewe na sisi Tanganyika yetu Irudi tutakuwa kama Russia na Zanzibar ni Georgia tutaishi bega kwa bega TUTASHIRIKIANA KAMA KAWAIDA KIUCHUMI NA KIBIASHARA KAMA ILIVYO sOUTH AFRIKA NA LESOTHO

Zanzibar ikipata viongozi imara, ikajitenga na Tanganyika ndani ya miaka kumi Zanzibar itakuwa heaven, yenye uchumi imara kama Dubai, wahakikishe wanzuia immigrants na watangaze utalii ipasavyo na karafuu yao, hakika watapiga hatua kubwa sana
 
Naona nami nijitose katika kuchangia katika suala la muungano kwani naona wengi wetu tumekuwa misled na wakuu kwa miaka 48 na kufika hadi kutotambua hasa nini hasa azma ya muungano. Nasema hivi nikiwa na uhakika haya yanayoonekana kama matatizo katika muungano yamelelewa na CCM kwa kutokuwa wakweli na kuwa na udanganyifu katika shughuli nzima ya huu muungano. CCM ndio ilioulea muungano huu usiokwisha mashaka na kuushikilia kwa nguvu zote huku ikizuia watu kutoa maoni yao na hisia zao juu ya mfumo wa muungano wautakao.

kwa vyovyote unless uwe na mapenzi ya upofu au illiterate wa kupigiwa mfano huwezi kukaa ukasema mfumo huu wa muungano wa sasa wa nchi hizi mbili (regardless ya size na population yake) ni mzuri na wa kupigiwa mfano. Dhima ni kwa CCM kuhakikisha umoja unalindwa ikiwa muungano upo au hautakuwepo na ni dhima kubwa juu yao kwa kuwahadaa wananchi wakawa sasa wanageukiana wenyewe kwa wenyewe wakilumbana wakisahau udugu uliopo na amani ilioendesha taifa hili kwa miaka mingi. Hadaa kubwa katika mungano huu ni kwa watanganyika kuwekewa dhana na CCM as if union hii ni ya taifa moja la Tanzania huku ikiwahadaa wananchi kule visiwani kwa kuwaambia nyinyi muna nchi yenu na serikali yenu na maamuzi yenu ambayo sisi hatutaingilia "independence status katika nchi ndani ya nchi". Hivi kuna muungano uliodumu wa namna hii usio na malumbano kama yetu?

Katika miungano mengi ya dunia ya mfumo kama huu haukufikia mbali, mengi imepotea huku nchi zilioshi kama moja kuwa mahasimu waliouana na kuumizana kwa miaka na dahari na kuharibu hata hayo maendeleo madogo yaliokuwepo. Time imefika kuwauliza hasa wananchi wanasemaje juu ya sakata zima la muungano na mfumo gani utaufaa kwa wnaanchi na ndio maana katika hali hii ya utata ya sasa ingelipendeza huu mzizi wa fitina ukaondoshwa mara moja kwa kuitwa kura ya maoni wakaulizwa wadau wenyewe ambao ni wananchi wa zanzibar na tanganyika kujiamulia future ya muungano wao wautakao. Ni dhambi kubwa kuwahadaa wananchi na kuwaacha kati wakilumbana kwa faida ya wachache ambao kwao hakuna utu wa kuwasikiliza wananchi matakwa yao.

Haiwezekani baadhi yetu tumuone adui Mhe Hamad kwa kutaka muungano wa mkataba, ni haki yake kama mwananchi na laiti kama ile iitwayo serikali ya mapinduzi ya zanzibar ingelikuwa na kauli juu ya mfumo wa muungano ambao yeye angelikwenda kinyume nao basi ingelibidi kisheria, logic na ethical ajiuzulu lakini ukweli ni kwamba serikali yenyewe hata ya muungano haijaja na msimamo wowote hivyo ni kosa gani kwake hata ajiuzulu wakati kina Shein et al waendelee kubakia katika nafasi zao kwa kuulinda mfumo unaonekana hauko fit for purpose.

Mtazamo wa mwanakijiji katika mfumo wa mkataba ni wa kizushi uliojaa na kiburi cha kuwatia khofu hususan watanganyika kwamba huu ni kuvunja muungano, sasa tujiulize ikiwa muungano umekubali kikatiba lakini unaweza kuvunjwa kwa mmoja wa wadau kubadili katiba yake (kama ilivyo zanzibar sasa na mabadiliko yake ya katiba 2010) ambayo yako kinyume na katiba ya muungano kwa nini tusiwapigie kelele hawa watukufu tulionao madarakani waliobariki mabadiliko hayo hasa yakiwa yanakwenda kinyume kabisa na muungano wenyewe katika katiba? Msome article ya Tundu Lisu utafahamu nini hasa kilichomo katika mabadiliko ya katiba ya SMZ na namna gani yamevunja muungano kikatiba. Kweli kuna tafauti gani ya mkataba na katiba ikiwa yote hayo yanawezwa kubadilishwa pindipo moja hatawafiki la mwenziwe kama sasa na marekebisho ya katiba ya zanzibar 2010? Utavunja vipi muungano kwa kuwa na mikataba katika muliokubaliana lakini mukadumisha muungano katika katiba ambayo tayari imeshachezewa na kuvunjwa na pande ya pili?

Tuseme muungano wa jumuia za ulaya ni mbaya zaidi kuliko muungano huu wa sasa usio na muelekeo wala ukweli kwa wadau wenyewe hata tusiweze kuuadopt ikiwa ndio kauli ya mwisho ya wadau wenyewe ambao ni wnaanchi? Mambo mawili kayachanganya katika statement yake hapo juu la kwanza kutaka Hamad kuacha madaraka yake ndani ya SUK, kwangu mimi hakuna sababu hizo sababu hajaenda kinyume na ministerial code of conduct kwa kuwa suala la maoni ya mfumo wa muungano ndani ya serikali zote mbili zimetoa fursa ya free vote, mifano kama yake ipo tele, tuangalie kule northern ireland na sinn fein wakiwa ndio viongozi wakuu wa serikali ya stormont ikiwa na mfumo wa coalition na wale unionist lakini mpaka leo sera za sinn fein na agenda yao ni kujitoa katika muungano wa uingereza sio hata kuwa na mfumo wa kimkataba sasa la ajabu lipi? angalia hata huyo deputy first minister wao anajulikana kabisa kama alikuwa ni miongoni mwa makamanda wa IRA, hebu tusiropokwe tu na tusome kwanza katika mataifa mengine duniani.

La pili kusema kwamba wanaotaka muungano wa mkataba wanakusudia kuvunja muungano hebu naatazame hao anaowapigioa debe waliopitisha maazimio ndani ya mabadiliko ya sasa ya katiba ya zanzibar basi kisheria muungano na katiba yake imeshavunjwa na mbona bado tunao tunawenda nao huku katiba mbili zikiwa parallel na msingi mzima wa union.

Hizi nchi hazijawahi kuwa moja, huo ndio ukweli mchungu, huwezi kuwa na nchi moja huku kukawa na limitation katika part moja kwa nyengine. kama ni nchi moja iweje tuwe na part moja yenye katiba yake inayoainisha hata mipaka yake, kuwe na mahakama zake, vikosi vyake, na listi iko kubwa tu sasa hamuoni huu mfumo ni kiini macho kinachowanufaisha ccm na kuwatia chuki baina yenu wananchi?

Kwa kweli hoja zake hazina misingi kielimu wala logic, tuwe wakweli na kuwaacha wenye maoni tafauti waeleze wananchokitaka ila wa mwisho wa maamuzi ni wananchi wenyewe, hatuwezi kuendekeza ujinga tulioambukizwa na siasa za kihadaa na kuwacha ukweli kwamba mabadiliko tunayoyataka ya kwanza ni nguzo ya demokrasia ya kweli, freedom of speech na kutoa nafasi ya wananchi kuamua na kuhsehimu maamuzi yao. Tunaokaa tukapiga kelele tunasahau kwamba katika kujinasibisha na nationalism movemement kuna hatari ya kuchangia katika dhambi kuu ya kutufitinisha baina yetu na kututia katika janga la chuki mwishowe vita na mauaji ya wenyewe kwa wenyewe.

Imani yangu muungano ukiwepo usiwepo hatuwezi kufuta historia ya miaka 48 ya kusihi pamoja, kuoana na kuzaliana. Tuwasikilize wananchi wasemavyo, isiwe nongwa kwa kuyasikia tusioyapenda, tuache democrasia iamue juu ya hatima ya union hii iliojaa na vitimbwi.
 
Mimi ni Mtanganyika asilia. Nimefuatilia miahadhara ya UAMSHO mtandaoni, nimetembelea Zanzibar na kusiliza kule saiti wanasemaje, na sasa ukiwasilikiza watu kama Maalim Seif. Ninafikiri wakati umefika tukubaliane kwamba hii ndoa ina kila sababu ya kufika mwisho. Tanganyika ni kama dume linaona aibu kutoa talaka. Sasa kwa vile Zanzibar wanaomba Talaka (mutuwache tupumuwe) tuwaunge mkono katika harakati hizo wawe jamhuri huru. Nina uhakika undugu wetu na ushirikiano utaendelea kwa tija wakati kila mtu akiwa kwao kama ilivyo sasa hivi baina ya nchi za Afrika mashariki. Ninaunga mkono hoja ya UAMSHO alimradi wasitumie matusi na vigezo vya Dini kudai uhuru wa Zanzibar.
 
Huyu Seif ndio mwanzo wa Matatizo yaliyo mengi ya Wazanzibar maana haeleweki sasa kwa nini amefunga ndoa na CCM? Wazanzibar huyu mtu mwogopeni kama ukoma eti.

Seif anakuwa tatizo au mwanzo wa matatizo kama wewe ni CCM na pia kama ni muumini wa muungano wa mazingaombwe.

Tatizo kubwa la matatizo ya Zanzibar ni uchakachuaji wa kura za uchaguzi mkuu(ubadilishaji wa matokeo ya uchaguzi) unaofanywa na tume ya uchaguzi kuitangaza CCM kuwa ndio wameshinda huku ikiwa si siri kuwa vyombo vya dola hutumiwa na CCM kulazimisha tume kubadili matokeo.
Tokea uchaguzi wa 1995 CCM haijawahi kushinda uchaguzi mkuu Zanzibar. Hata huku Bara(Tanganyika) tunaelewa nini tume ya Lewis Makame na Kiravu imekuwa ikifanya.

link Documentary - Zanzibar, Tanzania - Nioneshe Njia (Kiswahili) 2/4 - YouTube

Matatizo mengi ya wazanzibari ni muungano wa kiini macho,mali ya CCM, ambao wanasema wataulinda kwa nguvu na "liwalo naliwe". Lakini sio kwa wazanzibari peke yao muungano kama ulivyo ni tatizo hata kwa watanganyika (wadanganyika,wabara). CCM wanatumia muungano kama "juju" yao kung'ang'ania madaraka.

Mzee Mwanakijiji alishaandika makala siku za nyuma kulielezea hili na alisema amebaki peke yake katika kuutetea muungano.link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-watanganyika-ili-watoke-kwenye-muungano.html link2. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/336054-wapigania-uhuru-wa-zanzibar-waungwe-mkono.html link 3. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...tudai-serikali-moja-nchi-moja-taifa-moja.html

Pia Mchambuzi aliweka mada ya kuonesha "mazingaombwe/ukiini macho wa muungano" link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/334649-tundu-lissu-na-kiini-macho-cha-muungano.html

Kama ambavyo CCM imekuwa ikitugawia umaskini na ahadi hewa huku bara, ndio hivyo hivyo CCM wahafidhina wa Zanzibar wanavyotumia kauli za kulinda mapinduzi na muungano huku wakiwagawia wananchi wao ufukara.

Kama unapitia habari. Kuna wanaCCM ambao wanapotoa maoni kwa tume ya Warioba wanasema hata kama zitabakia serikali mbili basi wanataka mabadiliko makubwa ya kuipa Zanzibar nafasi ya kupumua. Je Moyo, Mansuri pia ni mwanzo wa matatizo ya wazanzibari?

Mimi naamini Seif kwa kuwemo katika GNU amepata nafasi ya kuitetea Zanzibar na maslahi ya Zanzibar ndani ya muungano. Lissu pia ni kama Seif link CHADEMA: Tanganyika irudi kwanza ndipo tuujadili Muungano - YouTube Badala ya kumuona Seif ni tatizo, mimi namuona kama mtu jasiri ambaye anataka kuunusuru muungano kuelekea kaburini. Ukisoma makala ya Mchambuzi utaelewa kuwa huu Muungano wa mazingaombwe uko kwenye self-destruction mode. Hata makala za M.MJJ pia zinaashiria kuwa Muungano unakwenda na maji. Unafikiri kwa M.MJJ kutoa rai kwa watanganyika(wabara) tudai serikali moja, nchi moja,taifa moja inamfanya yeye pia kuwa mwanzo(chanzo) cha matatizo ya watanganyika(wabara)/ watanzania?

Unafikiri kwa nini CHADEMA/ CUF wana sera ya muungano wa serikali tatu? Je kwa vyama hivi kutaka muungano wa serikali tatu kunavifanya viwe ndio mwanzo/chanzo cha matatizo ya watanzania?

CCM walikuwa wanajaribu kuzuia mjadala wa Muungano na mfumo/muundo wake kwa upana wake. Jaji Warioba alipata changamoto huko Zanzibar kuwa Katiba ya Muungano kwa Zanzibar inajikita katika Muungano na hivyo alijivisha mamlaka ya kuruhusu wananchi watoe maoni yao juu ya muungano kwa uwazi. Uhuru wa kutoa maoni ni kwa kila mtanzania. Tuvumilie maoni ambayo hatuyapendi au hayendani na maoni yetu...hilo ndio DOMO-krasia. Tusiwe na vichwa vya samaki(Karume alituasa). Kutoa maoni ni sehemu ya kutanua DOMO...domokrasia.
Hata wachina wameshaacha kuvaa sare..ni vyema kugonganisha maoni, wacha maoni yakinzane/ yapingane.

Watanganyika tuamke tudai haki ya Tanganyika ndani ya Muungano badala ya kuwaona wazanzibari kuwa ni "toto tundu". Au sisi tumeridhika na Muungano kama ulivyo? Kama hatufaidiki na muungano huu kwa nini tuko kimya?
 
Mwanakijiji, labda punguza ushabiki (uumini wa wako juu ya Nyerere na yote aloyafanya) na upunguze chuki juu ya Wazanzibar wanaodai haki yao ya kujitawala, kwakufanya hivyo utaweza kufikiri kwa akili yako ya kawaida na utaweza kujenga hoja zenye mantiki, sio upuuzi huu uloweka hapa!

Ahsante

Kweli unaamini serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar iliundwa kwa ridhaa ya Wazanzibari? Unafikiri iliundwa ili Wazanzibari wajitoe kwenye Muungano au iliundwa ili ipiganie muungano wa Mkataba?

Mbona hoja ni rahisi tu; kama CUF haiamini katika Muungano wa sasa ianze kwa kuwatoa wabunge wake kwenye Bunge la Muungano wa sasa? hii ni reasoning yenye makosa sana? Unaweza vipi kupinga Muungano wa sasa wakati unautumikia?
 
Back
Top Bottom