Sauna, Bodaboda vinavyosababisha Ugumba

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Vijana hususani wanaume wallo kwenye umri wanaotarajia kupata watoto, wameshauriwa kupunguza au kuacha kabisa matumizi ya kuoga katika sauna ikielezwa kuwa kiwango cha joto kwenye bafu hilo ni moja ya sababu za ugumba.

Kadhalika, madereva wa bodaboda wakiwamo waende-sha vyombo vya moto mbalim-bali kwa muda mrefu, ambavyo injini yake ipo jirani na mfumo wa uzazi wa mwanaume, wamo hatarini.


Sauna ni bafu la mvuke kwenye chumba kidogo au jengo lililosanifiwa kama sehemu ya kupata joto la mvuke, ambao huweza kuwa mkavu au wenye maji maji, na huwa na kiwango cha joto 150 ° F hadi 195 ° F (65 °hadi 90°C).

Bingwa wa Uzazi na Ma-gonjwa ya Wanawake kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Belinda Balandya, alitoa tahadhari hiyo hivi karibuni, jijini Dar es Salaam, kwenye semina kuhusu afya, iliiyoandaliwa na Wakfu wa Merck Foundation, ambayo ni tawi la Merck KGaA la Ujerumani.

Alisema kuna sababu tofauti zinazosababisha wenza wanaotarajia kupata mtoto, kuchukua kipindi cha mwaka mmoja bila matarajio, kuwa hali hiyo kitaalamu hutafsiriwa kuwa ni ugumba.

Vilevile, alisema mara kadhaa suala la ugumba jamii hudhani limeegemea kwa wanawake pekee na kwamba elimu duni ni sababu ya tatizo hilo, akilitaja huchangia pia na wanaume.

"Dawa za kupulizia kwenye mboga na zikaliwa ndani ya muda mfupi, kuliko inavyoshauriwa kuna uhusiano na tatizo la ugumba. Dereva bodaboda, wanaooga kwa sauna wanaohitaji watoto wanashauriwa kuwa makini iwapo bado ni vijana wanaohitaji watoto.

"Kundi hilo (dereva) lipo hatarini kwa kuwa hukaa juu ya injini (ya pikipiki) kwa muda mrefu na joto kali kwa saa nyingi na wanaotumia sauna ambao umri wao bado vijana wanashauriwa kutumia 'shower' (maji ya bomba la mvua) kuliko kukaa kwenye sauna muda mrefu," alisema Dk. Belinda akiongeza:

"Nilikuwa na client (mgonjwa) mmoja ambaye alipata ajali akiwa anaendesha gari, alikuwa na presha sana na hakukubali hapo awali, hadi baadaye alipokubali kuanza matibabu." Akifafanua zaidi kuhusu ugumba, Dk. Belinda alisema, tatizo hilo huwafanya wanaokumbwa nalo kuwa na msongo, jinsi zote, kwa kuwa baadhi ya jamii huwanyanyapaa, hasa mwanamke kunyanyapaliwa kutokana na kutopata ujauzito.

"Sio wanawake tu ambao wana tatizo hili. Wanaume pia mfano kama anavaa boxer (nguo ya ndani) na sehemu ya maumbile ya viungo vya uzazi wa kiume kubanwa sana ni tatizo alisema Dkt Belinda.​
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom