Satelite dish Vs antenna

mshewa2

Member
Oct 30, 2012
77
12
Jamani naomba kujuzwa nimenunua kigamuzi cha star timez afu nina dish kwangu naweza kuunganidha kwa dish badala ya antena?
 
Hapo huna ujanja. Utalazimika kutumia ki-antenna kidogo kilichokuja na dekoda (indoor attenna) au nenda maduka ya Startimes ununue antenna ya kuweka nje.

Startimes hawajaanza kurusha matangazo yao kwa kutumia dish.
 
Jamani naomba kujuzwa nimenunua kigamuzi cha star timez afu nina dish kwangu naweza kuunganidha kwa dish badala ya antena?

Ndiyo inawezekana na mimi nimeunganisha hivyo. Kwenye receiver ninayotumia for Sat kuna LNB IN na LNB OUT, kwenye receiver ya Startimes kuna RF IN na LOOP OUT.

Unaunganishaje?

Cable inayotoka kwny dish inaingia kama kawaida kwenye receiver yake kupitia LNB IN. Sasa itabidi uwe na kipande kingine kifupi cha cable ambacho kitatoka kwenye Sat receiver kupitia tundu la LNB OUT na kuingia kwenye receiver ya Startimes kupitia tundu la RF IN.

Cha muhimu hicho kipande cha cable utakachounganishia kiwe na zile Pin zake (zinauzwa kati ya sh 1000-1500) husika. Namaanisha ile inayotoka kwenye sat receiver (LNB OUT) na inayoingia kwenye receiver ya Startimes (RF IN).

Nilijaribu na nikafanikiwa siku 4 zilizopita. Sat receiver ninayotumia ni Qsat. Nilijaribu kufanya hivyo ili nipate local channels.

Pia kuna jamaa zangu wana receiver ya Startimes na wanatumia dish la GTV (iliyofilisika miaka ile) na wanapata matangazo. Give it a try.
 
Mkuu ilonga, tafadhari fafanua vizuri maana nijuavyo mimi star times receiver yao ina tuner tu kama tv za zamani, sasa ilo dish kutoka ktk hiyo DVB inatumika kama signal ya antena au input signal ya sattelite receiver? Hao star times wapo katika masafa ya MHS je channels gani tofauti unazozipata tofauti na zile za star times? na je dish linaelekea wapi?
 
Last edited by a moderator:
ilonga tunasubiri ufafanuzi.

Sent from my GT-I9192 using Tapatalk
 
Oh okay, dish inatumika kama antena ya kawaida kupata channels za Star Times, not otherwise
 
ilonga tunasubiri ufafanuzi.

Sent from my GT-I9192 using Tapatalk

Dish linatumika kama antena mkuu kwa kupata chaneli za starTimes not otherwise, kama mleta mada alimaanisha kutumia receiver ya Startimes kupata channels kama za DSTV, sikumaanisha hilo. Nadhani nimeeleweka.
 
Back
Top Bottom