Sasa ndio nimejua kwanini Nyerere alisema CCM ni ya wakulima na wafanyakazi na sio wafanyabiashara

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,299
Mungu ampe pumziko la milele Hayati Kipenzi cha Watanganyika, Baba wa Taifa hili, Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Huyu baba alikuwa ni maono kwani alijua jambo litatokea na kweli hutokea. Wakati anaanzisha CCM, alisema hiki chama ni cha wakulima na wafanyakazi na sio wafanyabiashara. Kuwatenga wafanyabiashara kulikuwa ni kuwaweka kando na siasa kwani uwepo wao kwenye siasa madhara yake ni makubwa na ndiyo yanayotokea kwa sasa kwani wamekiteka chama na maamuzi yote ya chama yanawategemea wafanyabiashara hao. Kutokana na wao kuwa na fedha nyingi, wamekuwa wanapata ubunge na nafasi nyeti ndani ya chama, serikali, na bungeni.

Tumeshuhudia wabunge wafanyabiashara jinsi wanavyoupigia debe mkataba wa DP World bila kujali maslahi ya taifa kutokana na wao kupewa choo na DP World. Walipewa mwaliko wa kutembelea kampuni ya DP World huko Dubai kwa gharama za kampuni hiyo, kitendo ambacho ni cha aibu kwani ni rushwa ya mchana. Najiuliza, kwani ilikuwa ni lazima wabunge kwenda Dubai? Kwanini walienda?

Endapo tutaendelea kuwatanguliza wanasiasa, hasa wabunge, katika miradi mikubwa, hakika nchi itaingia kwenye migogoro mikubwa na hatutakuwa na uwezo wa kuwaadhibu hao wabunge.
 
TANGANYIKA TUMEROGWA NA ALIYETUROGA NAE KAROGWA SIJUI ITAKUWAJE MASIKINI NCHI YETU TANGANYIKA
 
Bogus treaty, bogus treaty, Serikali ya Tanganyika imesaini mkataba wa kilagaibna Serikali ya Dubai, wa kinyonyaji, wa kifisadi. Rushwa ni adui wa haki, rushwa inaipasua dola. Nchi hii inanuka rushwa, mlungula uliowezesha mkataba huu kusainiwa wa kuinyonya Tanganyika.
 
Back
Top Bottom