Sasa ndio Nimejua chanzo cha kupigwa Marufuku "Bunge Live" na Mikutano Ya Kisiasa

Chama kisichokuwa na hata mwelekeo leo katika matamko ya press conference zake. Jengeni hoja mwache kubwatuka ovyo.
Kama hakina mwelekeo kwa nini magu anakosa usingizi? Sirro anahangaika nao? Polepole anahaha kusema asiyoyajua? MaRc namaDC hawaelewi wafanye nini kwa hiki chama kwani position zao ziko at stake?
Hayo mawazo yako ukiyatoa mbele ya Kinana anaweza kukuzaba kibao bure!
 
Ukiacha kutumia akili madhara yake lazima uishi bila fikra za ndani za kujua mambo kwa weredi!!
 
Pamoja na uliyoyasema LAKINI haki za watumishi hazikugandamizwa kama ilivyo sasa! mishahara iliongezwa kila mwaka, annual increment ilipatikana, NINI kitanifanya niamini uhalali wa yanayofanyka sasa na serikali hii iwapo haki zinagandamizwa?

Maswali yako ni mazuri lakini,ukimuuliza mtu anayekulatu kulala na kwendachooni bila kufanya kazi kwakua anatumia kiinuamgongo cha babayake hamtaelewana
 
Kuwe na interview kabla ya kuingia.
Hilo jambo lilishauriwa siku nyingi sana hasa baada ya aliyekuwa Katibu wa propaganda wa Lumumba yule aliyenyooshewa mguu wa kuku kuunda kikosi kazi. Kikosi hicho kijulikanacho kama Buk7 ndicho kilichoharibu JF kwani kilikuwa zoazoa na kilileta humu ndani watu ambao sio GT's .
Leo tunashuhudia mada za hovyo sana wakati wakongwe waliijenga JF hadi ikapata members mashuhuri na wakiingia kwa majina yao na kujibu hoja au mijadala bila woga. Ulifika wakati watu walikuwa wanamshauri Mkwere ajiunge kama verified user tupate kusemezana humu. Lakini kwa hali kama hii ya sasa ( kujaa waduanzi) hata Mtu wa kawaida kama Chakaza kuja kama verified user ni kutaka kuvunjiwa heshima tuu
 
Kama hakina mwelekeo kwa nini magu anakosa usingizi? Sirro anahangaika nao? Polepole anahaha kusema asiyoyajua? MaRc namaDC hawaelewi wafanye nini kwa hiki chama kwani position zao ziko at stake?
Hayo mawazo yako ukiyatoa mbele ya Kinana anaweza kukuzaba kibao bure!

Muongeze huyo mleta mada labda atabadili kamtazamo kidogo kuelekea maisha bora na usawa
 
na ndiyo maana wazungu wanatuona malofa ,ndiyo maana walitucolonize kwa sababu walituona ni mazuzu.linapokuja swala la kitaifa bhuwezi kuona mzungu akimpinga rais wake.lakini mwaafrica mweusi anakuwa mtetezi wa mkoloni .ndo maana africa haiwezi kusonga mbele
Wewe wa wapi sijui...Wamarekani waliandamana siku kumi na tatu kupinga vita dhidi ya Iraq wakati wa utawala wa Bush.Kumbuka kua wezi ni ccm sio wazungu.Lakini pia ni jambo la ajabu leo hii mnawasema wazungu kua maadui wetu huku hao hao ndio wanakupa ata panadol na net za kuzuia mbu wa malaria

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kufungia bunge kumezuia upotoshaji wa malengo ya serikali kutuletea maendeleo ambao ungefanywa na wapinga maendeleo wa taifa letu "at massive level" - Wewe fikiria kuna upotoshaji na kubeza juhudi za serikali humu JF ambao sisi wengine tunaweza kuchambua na kuona mchele ni upi na chuya ni nini! Lakini kama bunge linge achiwa live kuna watu wengi wange weza kurubuniwa na hao maadui wa taifa wa ndani na ingekuwa siyo rahisi kuendelea kuleta maendeleo. Imagine mbunge - MwifwaJF-Expert Member asimame aulize swali hili bungeni!:
"Jamani Bombardier itaachiwa lini, maana Lumumba wamepata kichaa".
Au Mbunge ObumaJF-Expert Member anasimama na kusema haya :
"Kwa kweli hili jukwaa limekuwa na watu wajinga mno. Mleta uzi ni miongoni mwao". Wasikilizaji na watazamaji wengine kama bunge ni live watawaiga hawa watu (wabunge) na kuona ni role model na wao wataanza kufanya kama wao- hivyo ile mbiu ya "HAPA KAZI TU" hawataweza kuikubali. Lakini kwa sababu bunge siyo live wanaopotoshwa siyo wengi na taifa linazidi kunyooka!

Mkuu;
Kwanza nikupongeze kwa kutoa mawazo muruwa kabisa. Ila nina ka swali kidogo; Wewe umeona maendeleo gani yameletwa kwa kulifungia bunge live?? Nashukuru tunazungumza tu sisi humu jf. Hivyo hebu mwaga hapa jf maendeleo au endeleo limoja tu lililoletwa na kulifungia bunge live. Moja tu sitaki mengi hivyo niambie ni lileee.
Pili, HAPA KAZI TUU. Imeonekana wapi?? Tumetumbua wazembeeee hadi damu ikatoka badala ya usaha. Halafu??!! Haya, Tumeziba mianya ya rushwa za kodi, kweli tulitangaziwa makusanyo meengi, leo mbona hamtangazi tena?? Sasa angelitokea mbunge flani akauliza swali hili, serekali ingelijibu??
Swali hilo kwa kuwa lingelikosa jibu, si tiyari tungelimuona huyo mbunge kuwa ni adui wa taifa kwa sababu tu ameuliza swali la kweli ambalo sasa serekali imeshindwa kulitolea jibu??
Tungeliweka bunge live, lakini maswali yawe ni yale yenye ukweli na uwazi sio ya kubuni tu. Jiulize, Je, ni kweli tunadaiwa nahayo makampuni yaliyoteka ndege yetu kule Canada?? Kama ndivyo, je kosa lipo wapi la muuliza swali bungeni??
Sio kila swali ni baya au lina nia mbaya. Tukiulizwa kitu cha kweli tusichukie.
Mimi ningelijibu tu hivi; Ndio ndege yetu imetekwa kwa sababu ya deni, ila tunafanya harakati za kupatana na mdai wetu aiachilie tumalizane kistaarab. Ni jibu murua kabisa kwani ni lazima tutamalizana naye ndege yetu iachiliwe.
Hakuna uadui au kutokuwa mzalendo hapo. Kuwa mzalendo sio kuukataa ukweli
 
Cha ajabu kwenye hiyo mikutano hizo ziara zinazoitwa ni kukagua na kuxindua miradi ya maendeleo jamaa. Akilitumia jukwaa hilo kufanya kampeni na kuwananga wapinzani. Mara ooh mlikosea kuchagua, Mara msifanye makosa safari ijayo n.k.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hakuna juha kama anayesema leo ni jana!! Unapowaita wapinzani kuwa ni waongo na wasio na uzalendo bila kuwapa nafasi wajitetee kumbuka wasikilizaji huchoka maneno yako na kujua kuwa kumbe unawaogopa unao wasema. Mtz wa leo sio yule wa kutishwa na picha za Rwanda na Burundi za mauaji ya halaiki.
 
Tuliona wakati bunge ilipokuwa live jinsi baadhi ya wabunge walivyokuwa kichefuchefu mpaka kutia aibu. Majuzi tu tumeona mbunge akimwita spika FALA. Kupiga marufuku imesaidia kuficha jinsi wabunge wanavyo mis behave.

Shukrani mkuu. Sasa wabunge wana "biheivu" vizuri sana baada ya kufungiwa bunge live. Hivyo, tunawaona wakiswekwa ndani tunafaidi nini?? Kuna endeleo gani limepatikana tangu kufungiwa bunge live?? Litaje kwa jina tu. Sitaki utaje mengi taja moja tu. Ni ajira zimefumuka, ni bei ya sukari imeshuka au ni petroli imeshuka??
Nadhani huyo mbunge alikosa neno lingine na kwa sababu ya muda mfupi alopewa, akawahisha hilo ,neno Fala.
 
Shukrani mkuu. Sasa wabunge wana "biheivu" vizuri sana baada ya kufungiwa bunge live. Hivyo, tunawaona wakiswekwa ndani tunafaidi nini?? Kuna endeleo gani limepatikana tangu kufungiwa bunge live?? Litaje kwa jina tu. Sitaki utaje mengi taja moja tu. Ni ajira zimefumuka, ni bei ya sukari imeshuka au ni petroli imeshuka??
Nadhani huyo mbunge alikosa neno lingine na kwa sababu ya muda mfupi alopewa, akawahisha hilo ,neno Fala.
Mkuu kwa jinsi Rais Magufuli alivyokuta hali ya nchi ni lazima awe mkali sana, Tanzania ilikuwa inaishi kwa artificial economic maana yangu uchumi wa kudanganyana. Mfumo mzima wa nchi ulikuwa mbovu ndio maana CCM kwenye uchaguzi mkuu iliponea tundu la sindano. Katika mageuzi ya uchumi nchi yeyote yanakuja na maumivu yake tuwe na subira muda si mrefu hali ya maisha itarudi kwa mfumo wa kila mtu afanye kazi, ule utajiri wa haraka haraka unaenda Ukingoni. Vyama vya upinzani vina nafasi muhimu katika kumsaidia kiongozi huyu shupavu katika kipindi hiki kigumu badala yake vyama vya upinzani vimekuwa vikwazo katika kuleta mabadiliko hayo.
 
Daa! Uzi umewekewa Heading nzuri sana, lakin kilichoandikwa ni uzwazwa wa kiwango cha kufirika
Kuongelea suala la ndege kuzuiwa inatafsiriwa tofauti kabisa

Lakin nikuulize ndg mwandishi...
Kama mh. Lissu asingeongea habari ile, wewe unafikiri ungejua kupitia chanzo gani??
Na baada ya kujua hilo kupitia Lissu, umeathirika kwa kiwango gani??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mjibu hoja zake badala ya kum-attack personality yake. Kupishana mitazamo, maono, misimamo ni moja ya mambo yanatufanya tuitwe binadamu.
Kama hukubaliani na hoja zake; pambana kwa hoja
Nijibu nini mkuu, hivi ni vihoja sio hoja mkuu. Ukitaka kujibiwa ibua hoja yenye maslahi mapana ya nchi utajibiwa. Ukimjibu mjinga atajihesabia ni mwerevu ila ukimwambia ni mjinga kesho atakuja na hoja ya maana.Huwa sijibu ujinga mkuu kwani nina heshima zangu.
 
Mkuu kwa jinsi Rais Magufuli alivyokuta hali ya nchi ni lazima awe mkali sana, Tanzania ilikuwa inaishi kwa artificial economic maana yangu uchumi wa kudanganyana. Mfumo mzima wa nchi ulikuwa mbovu ndio maana CCM kwenye uchaguzi mkuu iliponea tundu la sindano. Katika mageuzi ya uchumi nchi yeyote yanakuja na maumivu yake tuwe na subira muda si mrefu hali ya maisha itarudi kwa mfumo wa kila mtu afanye kazi, ule utajiri wa haraka haraka unaenda Ukingoni. Vyama vya upinzani vina nafasi muhimu katika kumsaidia kiongozi huyu shupavu katika kipindi hiki kigumu badala yake vyama vya upinzani vimekuwa vikwazo katika kuleta mabadiliko hayo.
Unaweza kuwa na hisia chanya kabisa kwa nchi yako, lakin ukatafsirika vibaya
Wapinzani miaka yote wanaitaka nchi itoke kweny minyonyoro hii, lakin leo mnawaona sio wazalendo

Rais, (wakati huo akiwa waziri) alishiriki kupinga ripoti ya akina zitto na bomani iliyohusu upitiaji wa mikataba ya madini, lakin leo mnamuona shujaa na kumtunuku majina mengi ya kishujaa

Lakin tunasahau kuwa hawahawa wapinzani mnaowaita antipatriotism, ndio wanaowafanya mjue uozo uliomo serikalini.

Tusiishie kuponda tu upinzani, wakati mwingine tuupongeze maana unatutoa gizani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nijibu nini mkuu, hivi ni vihoja sio hoja mkuu. Ukitaka kujibiwa ibua hoja yenye maslahi mapana ya nchi utajibiwa. Ukimjibu mjinga atajihesabia ni mwerevu ila ukimwambia ni mjinga kesho atakuja na hoja ya maana.Huwa sijibu ujinga mkuu kwani nina heshima zangu.
Huwezi kuwa na heshima wewe fedhuli
 
Wakati Rais Magufuli alipoingia madarakani mwaka 2015 alijua kuwa anaingia kwenye kazi ngumu sana katika kurekebisha hali ya nchi ilipokuwa imefikia.

Kwa ujumla watanzania walikuwa wamechoka na utawala wa CCM ilivyokuwa inaendesha nchi.

1. Matumizi mabaya ya fedha za serikali.
2. Ukusanyaji mbovu wa kodi za serikali
3. Demokrasia ilivyofikia hatua yakuwa ni biashara kwa viongozi kununua madaraka.
4. Mikataba mibovu iliyoiletea nchi hasara ya matrilioni.
5. Uhujumu mkubwa kwenye kampuni ya Tanesco kufikia hatua nchi kuwa na mgao wa umeme.
6. Kuuwawa kwa maelfu ya wanyama Tembo na kufikia hatua Tanzania kuwa kinara wa kusafirisha Pembe za Tembo Afrika.
7. Serikali kuchukua mikopo mikubwa na mikopo hiyo kuishia kwenye matumizi yasioeleweka.
8. Kiwango cha Elimu kushuka kiwango.

Hiyo hapo juu ni baadhi ya kero iliyokuwa ikiwagusa watanzania kwa ujumla, vyama vya upinzani vilionekana kama vikitetea masuala hayo juu kwenye majukwaa kiasi ambacho kwenye kampeni za ukawa kauli Mbiu ilikuwa Mabadiliko.

Cha kushangaza baada ya Rais Magufuli alipoingia madarakani alianza kwa haraka sana kutekeleza mabadiliko hayo vyama vya upinzani ndio zimekuwa kiasi kikubwa kikwazo dhidi ya mabadiliko hayo. Imefikia hatua viongozi wa upinzani kuita press conference na kuanza kuponda hatua anazozichukua Rais Magufuli dhidi ya mikataba mibovu leo kuna viongozi wa vyama vya upinzani wamefikia hatua ya kuwa watetezi na wasemaji wa makampuni haya ya kinyoyaji bila aibu. Juzi tumesikia kiongozi wa upinzani akiitisha press conference kufurahia kwa Ndege kuzuiwa huko Canada.

Katika nchi nyingi linapokuja masuala yanayohusu maslahi ya kitaifa huwa hakuna mambo ya vyama. Rais Magufuli alipoamua kupiga marufuku bunge live na mikutano ya kisiasa aligundua kuwa viongozi wengi wangetumia majukwaa haya kukwamisha juhudi zake.

Wapinzani wawe na subira mwaka 2020 watanzania wataamua.
Uharo wa bata unaleta humu kutuniksha uvundo
 
Huwezi kuwa na heshima wewe fedhuli
Kwanin mna-panic??
Tatizo lako umeongea very emotional.
Ulianza kwa nia njema, lakin ukaendelea na kumaliza emotionally

Unaweza kuulizwa:
Je, unatafsirije taarifa ya Lissu, na angalizo lake dhidi ya kuvunja mikataba ya madini kuwa ni kuwatetea wazungu?
Je, unaweza kutuambia kauli gani aliyoitoa Lissu dhidibya ndege iliyozuiliwa canada iliyokufanya useme alifurahia?
Au Je, Ni jambo gan la kifisadi ambalo magu amelitatua ambalo chanzo chake ni antipatriotism ya upinzani?

Ukiweza kujibu vizuri hapo, basi tutajua kuwa you are not emotional oriented one

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom