Sarah Simbaulanga: Mwanamke wa kwanza kuiba pesa ndefu katika historia ya benki zote nchini

Mwenye kumbukumbu juu ya kubadilishwa kwa fedha za Tanzania 1986 kutoka noti nyekundu na kuletwa noti ya kijani. Nini kilisababisha mabadiliko haya?
 
Simbaulanga na Maumba walitrend sana 80's. Cha ajabu saivi kina maumba wapo wengi sana lakini hawashughulikiwi!
Umeniwahi, nami nilitaka kumtaja huyo Fedhuli Athumani Maumba.

Pamoja na Simbaulanga ni kati ya majina yaliyovuma kwa walichokifanya...pia kuna wale jamaa walioteka Ndege wakitumia maembe, ila wao umaarufu wao ulikuwa wa pamoja, majina yao hayakuvuma sana, tukio ndio lilivuma zaidi ya wao.
 
Miaka Ile nilikuwa shule ya msingi, shule niliyosoma ilikuwa ya watoto wa viongo, ukikosa gazeti unawaambia wakusimulie walichosoma.
 
Kituko,
Hizo kesi zinafanana kwa dhima kuu ya mapenzi kupelekea uhalifu na hitimisho lao linafanana kwa kuwa wote walidakwa na mikono ya dola by then hapakuwa na teknolojia ila tulikua na maafisa usalama na makachero wa polisi walio iva.

Uzalendo ni km msingi wa ulinzi na usalama. Changamoto kubwa ni kuwa kesi zilionyesha maamuzi ya wanawake yamejaa hisia na hisia ziliwafanya ubongo wao ushindwe kutafakari vema.
 
Umeniwahi, nami nilitaka kumtaja huyo Fedhuli Athumani Maumba.

Pamoja na Simbaulanga ni kati ya majina yaliyovuma kwa walichokifanya...pia kuna wale jamaa walioteka Ndege wakitumia maembe, ila wao umaarufu wao ulikuwa wa pamoja, majina yao hayakuvuma sana, tukio ndio lilivuma zaidi ya wao.
Sawa sawa kabisa Mhenga Mwenzangu!
 
Sio mwanamke tu, kipindi kile kuiba pesa ilikuwa ni jambo la aibu, yaani watu walikuwa wanakushangaa na sio wanakuadmire sahizi mtu ukiiba watu wanakusifia (hawajui kwamba hizo ni pesa zao wenye),

Kweli akili zetu zipo kwenye reverse gear for some time now, tunazidi kuwa mazuzu as days goes on (mind evolution yetu ina-move from brightness to foolishness).
Ni pamoja na yako au
 
Hivi huyo Sarah Simbaulanga alikua mzima kweli? Tukio zima, kama ninavyoliona, lilifanywa na mtu ambaye uelewa wake wa dunia inayomzunguka ulikuwa mdogo sana, yaani mtu asiyeona hata nchi moja mbele ya pua yake! 😅
HALAFU, AJABU, WABONGO MAJUHA WANAMSIFIA! 😅
 
Huyu Sarah Martin Simbaulanga hivi alimaliza kifungo chake ? Maana ni mwanamke wa kwanza Tanzania kusikika kwenye vyombo vya habari kwa zaidi mwezi ...Mama aligoma sana
 
Naikumbuka sana hi kesi, nilikua nasoma darasa la tano na ilitokea nikiwa likizo, kaka yangu aliyekua ananilea alikuja na magazeti (sikumbuki majina ya yale magazeti) but weekend bro alileta magazeti (wakati huo yalikua moto kweli kweli ) Mzalendo na gazeti la Mfanyakazi lilikua linamilikiwa na JUWATA/sasa OTU ambao pia walikua wakimiliki banda ya Juwata Jazz band wana Msondo Ngoma.
 
Back
Top Bottom