Samwel Sitta: Wa kuogopwa urais 2015 ni Dr. Slaa tu

Anazeeka vibaya,angeangalia kwanza Wilaya ya Urambo aliyoiongoza kwa miaka yote ina maendeleo gani, hivi ninavyoongea hiyo wilaya ni mojawapo ya Wilaya zilizo nyuma na maskini kabisa Tanzania, miundo mbinu mibovu na ina watu waliokata tamaa ya maisha,barabara hadi mjini vumbi tupu,na nyumba za nyasi hadi katikati ya mji.

Sioni cha kujivunia kwa uongozi wake. Ameongoza wilaya akiwa kama spika na hakuna hata tone la maendeleo alilopeleka.

Sasa shangaa mtu kama huyu ambaye hata jimbo limemshinda leo anafikiria urais.Napendekeza M4C mfike Urambo ili tukomboe ilo jimbo.
 
Hata kama wako wachache,Sitta hatakiwi kabisa CDM maana ni mnafiki,anafikiri hicho ni
kigezo cha kumfanya kupewa nafasi ya kuingia Chama Dume!!!NO
 
Muulize yeye mabona alishindwa na mwanamke (sio kuwa nawadharau wanawake hapana hata kidogo) ila kwa anavyojiona yeye, makinda asingelimshinda hata kama alisukiwa zengwe. Mpiganaji mashuhuri hata hilo zengwe angelilishinda. Jizee linazeeka vibaya.

Mr6 hata ukijitahidi vipi kuufukuzia u-Rais. "Watakupotezea" tena kwa kukumbusha kuwa 'safari hii ni zamu ya wanawake'. Umesahau ulivyoshindwa na bi-Kiroboto?
 
Huyo mbowe, slaa, zito, jj wala tundu siyo saizi yake, mtu ambaye anaweza kupima naye uwezo ni makinda hata yeye atamuacha kwa mbali ndiyo maana alipokuwa spika na makinda naibu wake Anna alipima uwezo wake na akamuona mwepesi tu ndiyo maana akandaa mazingira ya kumung'oa na kweli akang'oka. Uwezo wake apime na kina Maji marefu, lusinde na nchemba na wala siyo hao makamanda wa chadema. VIVA M4C
 
Kwa hiyo hizi ndizo kauli za mzee sitta? Anakoelekea siko kabisa. Wameona kuwa wameshindwa kuzuia m4c na sasa wanaleta propaganda za kejeli sio?
 
6 Kashindwa kusema ukweli,uongozi wa MBOWE cdm unawanyima usingizi wanaccm!hawakutarajia hii M4C
 
Sita inabidi ajue kuwa tulionao sasa hivi na wengine wengi wa CCM ni viongozi wanaoongoza kwenye wizi. Hawa hawatakiwi kabisa. Tanzania inahitaji viongozi wapya kabisa. Viongozi ambao siyo wezi. Mbona Rwanda wameweza kuongoza nchi wakati wote walikuwa wapya kabisa? Kwa nini Watanzania wasiweze?

Kaka angalia kauli zako za kufananisha...kagame na wenzake walikua wapya kabisa bila uzoefu mkubwa wa kiserikali, lakini Rwanda ni sawa na kuongoza mkoa mmoja wa Tz...Sitta yuko sawa kabisa, Rais ajaye wa Tz ukiachilia mbali elimu,uzalendo lazima awe na uzoefu wa kukabiliana na changamoto za taifa kwa wakati huu
 
Kwa hiyo hizi ndizo kauli za mzee sitta? Anakoelekea siko kabisa. Wameona kuwa wameshindwa kuzuia m4c na sasa wanaleta propaganda za kejeli sio?
 
Sitta kama ni mwanaume kweli asingekubali kugeuzwageuzwa namna hii na vijana wadogo kuliko yeye aloosaidia kuwaweka madarakani. Alikuwa KIONGOZI wa muhimili mmojawapo wa DOLA. Akapewa mtihani wa kubadili jinsia yake ili aendelee na Uspika. Akashindwa. Sasa hivi amepewa wizara ambayo ilipaswa kuwa IDARA tu ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Sitta amewaponza wengi kisha amewatupa na kuwasahau kabisa. Watu kama Selelii na yule bwana aliyeacha UBUNGE akaenda CCJ, Mpendazoe, hawawezi kumsahau Sitta. Sitta ni kigeugeu na fisadi wa kutupa huku akijifanya kupambana na mafisadi wenzake kwa sababu ya vyeo na madaraka.
 
Kama wewe ni CDM Ukisoma heading unaingia unacheka cheka,ukishasoma uzi unageuka mbogo kweli watu wanajua kuchezea watu.
 
Toka alipouzima kinyemela ule mjadala wa RICHMOND (mafisadi) bungeni, nikamtoa kabisa kwenye kundi la wapigania haki katika Taifa hili.
 
Anajiwekea mazingira mazuri ya kuhamia CDM ionekane hakuna viongozi wa kutosha ili apokolewe na kundi lake!
 
tusijibu kisiasa...huyu mzee naona yupo sahihi..mimi ni mwanaCDM..........lakini nakubaliana na uyu babu..Chadema inabidi tulitafakari ilo.......
 
Wakuu hebu twende sawa hapa acheni kumnanga mzee Sitta.

Anachokisema mzee Sitta ni sahihi kabisa kuwa kamanda Mbowe ana uzoefu wa kuchezesha Disco! Sio uwongo ni kweli tena kweli tupu isiyokuwa na shaka ndani yake.

1. Kwa ustadi wake ki dj kamanda mbowe ameongoza mdundo wa operation Sangara mara baada ya Zitto Kabwe kufukuzwa bungeni kwa inshu ya Buzwagi. Vipi magamba walicheza mziki ule au hawakucheza?! Mbowe ni dj mwenye uzoefu au sio?

2. Dj mbowe aliwaongoza makamanda wake wakafungulia mziki wenye sauti kubwa pale Mwembeyanga wakaimba chorus za list of shame huku Dr Slaa akitambaa na beat na kuwataja majina wahusika. Vipi mziki ule magamba waliucheza bila athari au walisikiliza tu midundo ya Jd Mbowe halafu mambo yakaisha?!

3. Dj mbowe alipo simamia hoja Dr Slaa agombee uraisi wakazunguka Tanzania nzima kumtambulisha na baadae akagombea. Vipi mziki waliucheza au waliendelea kukaa vitini wakistarehe huku wakinywa mvinyo?

4. Dj mbowe anavyo wapanga vijana wake Bungeni na kuwaongoza kuimba na kughani kusimamia hoja Bungeni kuhusu maslahi ya Tanzania, magamba wanacheza au hawachezi?

5. Mziki wa M4C vipi? Wanacheza au wamelala?

Mbowe ni DJ au sio Dj?
 
tusijibu kisiasa...huyu mzee naona yupo sahihi..mimi ni mwanaCDM..........lakini nakubaliana na uyu babu..Chadema inabidi tulitafakari ilo.......
Na wewe utakuwa upoupo tu ndani ya CHADEMA. Vichwa vyoote vile kwenye chama hiki Sitta anamwona Dr Slaa tu! Ametumia kigezo gani? Anaowaona majukwaani tu? Tuwe wakweli tu jamani. Sitta kwa Mbowe hauwalinganishi kwa lolote KIUONGOZI.
 
Nadhani kuna umuhimu wa kuitafakari vyema kauli ya sita. Hasa neno kuogopwa. Laweza kutumika kuogopwa kwa kuweza kuongoza au kutoweza kuongoza.
 
Makubwaaaaa.ngoja tuchukue nchi ndo watajua Kama tuna hazina ya vichwa chadema. Kwani nchi ilipopata uhuru tulikosa viongozi? Kumbe Sita siku nyingine anakuwa amechoka kiakili.
 
but kuna ukweli hapo...cdm hawana experience ya kiuongozi kama ccm...but at the same time kila kitu kina mwanzo..hamna mtu anazaliwa anajua kila kitu bali tunafundishwa
 
Wakuu hebu twende sawa hapa acheni kumnanga mzee Sitta.

Anachokisema mzee Sitta ni sahihi kabisa kuwa kamanda Mbowe ana uzoefu wa kuchezesha Disco! Sio uwongo ni kweli tena kweli tupu isiyokuwa na shaka ndani yake.

1. Kwa ustadi wake ki dj kamanda mbowe ameongoza mdundo wa operation Sangara mara baada ya Zitto Kabwe

kufukuzwa bungeni kwa inshu ya Buzwagi. Vipi magamba walicheza mziki ule au hawakucheza?! Mbowe ni dj mwenye uzoefu au sio?

2. Dj mbowe aliwaongoza makamanda wake wakafungulia mziki wenye sauti kubwa pale Mwembeyanga wakaimba chorus za list of shame huku Dr Slaa akitambaa na beat na kuwataja majina wahusika. Vipi mziki ule magamba waliucheza bila athari au walisikiliza tu midundo ya Jd Mbowe halafu mambo yakaisha?!

3. Dj mbowe alipo simamia hoja Dr Slaa agombee uraisi wakazunguka Tanzania nzima kumtambulisha na baadae akagombea. Vipi mziki waliucheza au waliendelea kukaa vitini wakistarehe huku wakinywa mvinyo?

4. Dj mbowe anavyo wapanga vijana wake Bungeni na kuwaongoza kuimba na kughani kusimamia hoja Bungeni kuhusu maslahi ya Tanzania, magamba wanacheza au hawachezi?

5. Mziki wa M4C vipi? Wanacheza au wamelala?

Mbowe ni DJ au sio Dj?

Una akilii....! Hebu chukua tano.
 
Back
Top Bottom