Samwel Sitta: Wa kuogopwa urais 2015 ni Dr. Slaa tu

sita aache mbwembwe,hivi anadhani hao viongozi wa ccm wilaya na mikoa watatetea chama chao kwa hoja zipi?mfano,nikisema mh.sitta alienguliwa kuwa spika wa bunge kwa nguvu ya mafisadi wanaomzidi kete.
nani anaweza kupinga,au kutetea kuwa sita lichoka kuwa spika ndiyo maana akacha??wakati tuliona wote kwa macho yetu huyu jaamaa alivyoathirika na hicho kitendo,naona maumuvu yanapungua anaanza kubwabwaja!!!
ndiyo,hivyo hakuna mtu,awe kiongozi kuanzia srerikali kuu,hata yeye sitta mwenyewe,anaye weza kujibu hoja zinazotolewa na cdm,maana ni ukweli,uhalisia wa tanzania na mfumo kandamizi wa uongozi.kama kuna gamba yeyote anabisha mie ninaushahidi mdogo tu.baada ya cdm kufanya mkutani jangwani,magamba chini ya nape walijaribu kujibu wakaambulia kujiaibisha wenyewe na wengine toka hapo tunawaona waimba taarabu hata kama tulikuwa na imani nao japo kidogo.kwangu mimi toka siku ile kitu kinaitwa "magufuli"ni mzee wa mipasho.
 
Tumshukuru Sita kwa kukubali hadharani kuwa Chadema ni tishio kwa Urais 2015. Na tunatakiwa tumpongeze huyu bwana ana kauli tamu sana. Juzi huko Igunga ndoo yeye anayewakataza wenzie kukataa rufaa kwani anaona. Tukipata watu kama akina sita wengi watatusaidia sana kubadili utawala bila vurugu zozote kwani CCM itakupokuwa imeshindwa atatusaidia kuwaelekeza wenzake kukubali matokeo. Si mnajua CCM ni vinga'ang'anizi na hawajijui kabisaaa kuwa huku nje hakuna anayewataka
 
Kumbe ni kweli "Mgema akisifiwa Tembo hulitia maji"; Poor Sitta has crossed the threshold!

Mzee wa "Kasi na Viwango" kwishneee! ameshindwa kupambana na mafisadi sasa ameamua kujiunga nao, anatumia tumbo kufikiri!

Pole Magreth, we expected better than this from Samuel; we are dissapointed, Going personal is stooping too low, and does not augur well for the man of your stature!
 
but kuna ukweli hapo...cdm hawana experience ya kiuongozi kama ccm...but at the same time kila kitu kina mwanzo..hamna mtu anazaliwa anajua kila kitu bali tunafundishwa

tatizo watu humu tuna ushabiki sana.........ukikubaliana na kauli ya Sita utapungukiwa nini?sana sana kwa mtu uliekomaa kisiasa itakujenga.........mimi ni cdm damu ila kauliya Sita in aukweli ndani yake.........CCM ina watu na personality zao ingawa ndio hao wanaongoza kwa ufisadi.......chadema has to work out na ifungue room for more matured people waingie mle ndani.........haina maan akuwa na vijana tu mle ndani tena wenye complicated marital status
 
Huyu Mzee 6 kuna wakati anakuwa na point na huwa namkubali sana..Ila kuna siku akiamua kuongea vapour/uzushi huwa anapitiliza. Sasa naanza kuamini anaugua ule ugonjwa wa ukosefu wa madaraka na hekima.
 
Kweli ukizeeka sam time unarudi mtoto!
samwel sita bado una mawazo mgando sana! Kwani ukiwa mpiga disko kuna tatizo gani? Mbona madagaska Raisi alikuwa mpiga disko!
Wewe mzee ni dhaifu,
unaelekea kusiko sasa.
 
tatizo watu humu tuna ushabiki sana.........ukikubaliana na kauli ya Sita utapungukiwa nini?sana sana kwa mtu uliekomaa kisiasa itakujenga.........mimi ni cdm damu ila kauliya Sita in aukweli ndani yake.........CCM ina watu na personality zao ingawa ndio hao wanaongoza kwa ufisadi.......chadema has to work out na ifungue room for more matured people waingie mle ndani.........haina maan akuwa na vijana tu mle ndani tena wenye complicated marital status

Marital status in development issues..!!! najaribu kufikiria 'r' yake..ila kuna ukweli wake.
 
Nimeshangazwa na habari kwenye gazetu la mwananchi toleo la leo lenye kichwa cha habari SITTA: TISHIO LA URAISI CHADEMA NI DR SLAA TU.

Ni wazi kuwa mheshimiwa sitta amefilisika kimawazo. Anajua fika kuwa ndani ya CDM kuna watu wenye uzoefu lukuki wa kiuongozi ndo maana hata yeye amekuwa akifanya vikao vya siri na viongozi waandamizi wa CDM ili ikiwezekana 2015 ahamie CDM.

Nimemnukuu akimponda Kamanda Mbowe kuwa ana uzoefu wa kuendesha kumbi za muziki tu si kuongoza serikali. huu kwangu ni uendawazimu mwingine wa mzee Sitta, Kwani anajua fika kuwa chini ya uongozi imara kwa Mh Mbowe CDM kimekuwa chama imara kisichotetereka, kupitia busara, hekima na ubunifu wa Mbowe CDM inawanyima CCM usingizi ndo maana kila kukicha CCM hawachoki kukisema.

Nakumbuka wakati Reginald Mengi alipofiwa na Kaka yake mzee Elitira Mengi, mzee Sitta na wenzake 3 waliomba kukutana na Mbowe pale Aishi Hotel na moja ya mambo walioongea ni sitta na wenzake 3 kuhamia CDM uchaguzi ujao wa 2015 na kuhakikisha CCM inaondoka kabisa madarakani.
Mzee huyu ni opportunist wa kufa mtu!! alianza siku nyingi kutafuta urais na amefeli kabisa!! Hebu fikiria Chama cha Kijamii alichoanzisha wao na Nepi na mpendazoe akakimbia. Kwa CDM hili gamba baya sana!!
 
Mtanzania wa makini hawezi kuufanyia kazi maoni ya Six ( Speed and Standard) kwani hana la maana au la kiushawishi kwani ni dhaifu sana kuliko waliokwishwa itwa viongozi dhaifu.

Six alishindwa kabisa kuwahakishia watanzania yale aliyoyasema kwa uhakika lakini alipobanwa zaidi mpaka leo ameshindwa kututhibishia Watz nayo ni kama haya:

(i) Alifunga mjadala wa Richmond bila hata ya mtanzania yoyote kuwa na majibu ya Richmond ambayo aliiundia tume yeye mwenyewe na baadae kusababishia Wana-CCm mgawanyiko/mpasuko mkubwa kwa kuwachonganisha.
(ii) Aliwahi kuwatahadhalisha wabunge kuwa ukumbi wao umekewa chemical za ungaunga/kifupi ushirikina hivyo kuwaacha wabunge kuwa na wasiwasi hadi kupoteza zile points walizokuwa wameandaa kuchangia bungeni.
(iii) Six huyo huyo alishikia bango juu ya hali ya Mbunge Mwakyembe kwa kuwathibitishia Watz kuwa amehujumiwa kwa kulishwa sumu lakini mpaka leo ameogopa kwenda mahakamani kutoa ushahaidi wa jambo hilo.
(iv)Ni Six huyu aliyethibitishwa kuwa ni mwanzilishi wa CCJ lakini alipopatiwa ulaji alikanusha vibaya kuwa haijui.
(v)Six huyu kama Mtz mwingine amepokea taarifa kupitia vyombo vya habari kuwa Nchini Uswiss pesa zetu zimefichwa na mafisadi toka Tz,lakini anajifanya hajui ila anataka kutegemea Watz wengine ndio wataje hao mafisadi lakini wakati huo huo anataka Watz tumwone kama mpambanaji.
(vi) Ni Six huyu aliyekurupuka kutaka tupigane na Malawi wakati hata Amiri Jeshi hana mawazo ya namna hiyo kwa maana nyingine hajui wajibu wake kama Waziri wa Ushirikiano na mahusiano Afrika Mashariki alitakiwa awe wa kwanza kutafuta suluhu kabla ya kushawishi vita kama hatua za mwisho.
(vii) Ni Six huyu aliyekuwa anadharau akina mama kupitia msaidizi wakati akiwa spika wa speed and standard kwa kipindi chake kwa kumwamru kuwa huyu mama (Makinda) asije akafanya mambo ambayo yako juu yake mpaka yeye awepo ndani ya Bunge ,lakini cha ajabu huyu mama akaja kumbwaga kwenye kiti hicho cha u-spika.
(viii) Ni Six huyu huyu ambaye anajua kabisa uongozi kwa nafasi ya Urais haupimwi kwa kuwa na idadi ya watu kwa majina kwa kuwa walishapata kuwa viongozi lakini wengi wao wapo kwenye shutuma mbalimbali za ufisadi,unafiki kama alionao yeye na hata uroho wa kujilimbikizia mali,hebu kama kweli CCM ina hazina tupe majina hata matano tu unayoona ni clean halafu utupe nafasi tukuchambulie kwa mmoja wapo uone kama hata hata chembe ya uozo.
(ix) Six nakutahadharisha kuwa basi wapo viongozi kuwa Ma-Rais kwenye Nchi zao waliotokana na sifa mbalimbali
tofauti na anazojijua yeye,wanamichezo,Ma-DJ,wanajeshi n.k.
Hili la sifa kama ya kamanda Mbowe anayodai Six ,mbona kiongozi wa Madagasca alikuwa DJ na baadae leo hii ni Rais na anaongoza Nchi yake kwa umakini hapo anasemaje?

Na hata hapa Bongo ambao naamini SIx anawaona kama hazina ya kuwa viongozi wengine fani zao walizo somea ni miziki
(Fani za Arts) hapo unasemaje?

USIWANDANYE WATZ TAYARI WEWE ULISHA-PROVE FAILURE SIKU NYINGI NA OLE WAO CCM WAJE WAKUPITISHE KUWA MGOMBEA WAO NDIO TUKUANIKE VIZURI.

JENGA CHAMA CHAKO ACHANA NA PEOPLBWANA.
 
Siasa ni mchezo unaotaka umakini wa juu hasa wakati wa kuzungumza hadharani, ni hapa majuzi Sitta kasema kila anayepewa nafasi ya kuongoza anafikiria atanufaikaje ('atatokaje'). Sasa leo anasema magamba ina zaidi ya watu 20 wanaofaa kuwa rais!
 
Sitta yupo katika ziara ya siku tano ya kiserikali mkoani Kagera kukagua miradi mbalimbali inayohusiana na mwingiliano wa uchumi na kijamii kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
No wonder nchi hii inazidi kuwa maskini, alichoongea Sitta ndio kazi za Serikali? Jitu kubwa zima linalipwa pesa za walipa kodi kwenda kuongea uharo.
 
tatizo watu humu tuna ushabiki sana.........ukikubaliana na kauli ya sita utapungukiwa nini?sana sana kwa mtu uliekomaa kisiasa itakujenga.........mimi ni cdm damu ila kauliya sita in aukweli ndani yake.........ccm ina watu na personality zao ingawa ndio hao wanaongoza kwa ufisadi.......chadema has to work out na ifungue room for more matured people waingie mle ndani.........haina maan akuwa na vijana tu mle ndani tena wenye complicated marital status

couldnt agree more!!
 
yani mnakaa kumjadili uyu dhaifu?? chama chake kilimuona dhaifu kabla sisi hatujaanza kumuona ndo mana wakampiga chini uspika..ebu tulia mzee wewe
 
sasa inaelekea viongozi wa ccm kama sita wameanza kuchoka na kukosa cha kuongea. wajaribu kufikiria namna ya kukiongoza chama chao waachane na Dk slaa na chadema.
 
huyu sitta anaeleweka yupo mguu ndani nje tokea wamnyime uspika.


Ndio maana anamsifia dr slaa ili apate huruma zake 2015 akiingia magogoni ni kweli ccm Ina watu makini Kama akina makinda, nape, mukama, lowasa, change, karamagi na rostam Tehe Tehe Tehe
 
Alikuja Nape, Mkapa, Lusinde,na wengineo lengo kukichafua chama lakini wananchi wakawajibu katika sanduku la kura kuwa hawadanganyiki.

Kwa sasa tusikubali uchaguzi 2015 bila kuwa na tume huru ya uchaguzi la sivo hawa wezi wa kura watazidi kuiba tena.

2015 itakula kwao na JK inavoonekana anataka kuacha historia ya kusaiini katiba mpya ili amalize kwa amani muhula wake na ajijengee heshima nje na ndani labda atafikiriwa kupewa uwakilishi na katibu wa UN
 
Kaka angalia kauli zako za kufananisha...kagame na wenzake walikua wapya kabisa bila uzoefu mkubwa wa kiserikali, lakini Rwanda ni sawa na kuongoza mkoa mmoja wa Tz...Sitta yuko sawa kabisa, Rais ajaye wa Tz ukiachilia mbali elimu,uzalendo lazima awe na uzoefu wa kukabiliana na changamoto za taifa kwa wakati huu

Nchi haitawaliwi kwa kujitwisha. Rwanda ni ndogo laini kubwa kuliko nchi nyingi za Ulaya kama Holland au Luxembourg. Belgium Kwa kufuata mantiki yako viongozi wa Tanzania wangeweza kutawala hizo nchi. Fyuuuu!

Viongozi wa Tanzania wa sasa hivi hata ukiwapa wilaya hawawezi kuiongoza vizuri kwani wanachokitaka wao ni kuiba tu na siyo kuongoza. Changamoto kubwa kwa wakati huu ni rushwa na wizi. Ni lazima taifa litafute mtu ambaye atafutilia mbali tatizo hili.
 
Huyu naye ana gonjwa la "multiple identities". Mara nyingine huwa hajitambua na anakosea kujua muda na hadhira iliyo mbele yake.
Ikitokea hivyo, mpuuzeni tu.
 
Back
Top Bottom